Hali si njema kwenye Makampuni ya Mawasiliano, Serikali iamke kutoka kwenye Usingizi wa Pono

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
9,288
9,923
Miezi miwili iyopita tulisikia Kampuni ya Millicom International Cellular SA (MIC) inayomiliki Tigo na Zantel imetangazaa kuwa imeingia makubaliano na kampuni ya Axian kutoka nchini Madagascar kwa ajili ya kuuza kampuni zake mbili za Tigo na Zantel kwa bei ambayo haijawekwa wazi.

Mwezi mmoja baadaye nayo kampuni ya simu ya Vodacom ilimesema hakutakuwa na gawio kwa wanahisa katika kipindi cha mwaka wa fedha ulioishia Machi, 2021.

Sababu za kutotolewa kwa gawio hilo ni hasara ya Sh30 bilioni iliyopatikana katika kipindi hicho.

Kutokana na hasara iliyopatikana baada ya kulipa kodi, bodi ya Wakurugenzi imeamua kutopendekeza Gawio katika kipindi hicho cha mwaka wa fedha ulioishia Machi 31, 2021

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Vodacom, Hisham Hendi alisema hasara hiyo inatokana na namna Kodi ilivyokokotolewa na kusababisha kutozwa kiwango kikubwa tofauti na mwaka uliopita.

Pia alibainishwa suala la kufungwa kwa laini milioni 2.9 za wateja wao ambao hawakukamilisha Usajili liliathiri mapato na faida ya kampuni hiyo.

Ikumbukwe kuwa Katika kipindi cha mwaka wa fedha uliopita (ulioishia Machi, 2020) Vodacom ilipata faida halisi ya Sh45.76 bilioni ikipungua kutoka Sh90.76 bilioni iliyopatikana kwa mwaka ulioishia Machi, 2019.

Wakati hilo halijatulia, jana kampuni hiyo imetangaza kujitoa kudhamini ligi kuu ya Vodacom kwa msimu wa 2021/2022 kwa kile kilichoelewa kupata hasara ya sh30 bilioni.

Huko Airtel nako hali si shwari wiki iliyopita tumesikia Kampuni hiyo ya Airtel imeuza minara yake ya mawasiliano wanayo imiliki kwa Ubia na Kampuni mbili tofauti – SBA Communications Corp na Paradigm Infrastructure Ltd kwa $175 milioni (sawa na Sh400 bilioni).

Mpaka hapa haitaji elimu kubwa sana kujua hali ilivyo mbaya kwenye sekta hii ya mawasiliano inayoingizia nchi fedha nyingi.

Tunapoelekea itakuwa mbaya zaidi, leo wanauza Minara, kuacha udhamini wa ligi, kuuza kwa Kampuni, kesho tutasikia wamefunga wameondoka.

Hii sio ishara njema hata kidogo niitake Serikali kukaa na haya makampuni ya simu kuona jinsi gani ya kutatua hizi Changamoto haraka sana.

Naona kama Serikali imelala usingizi wa pono "Haijigusi" Sijasikia Mbunge yoyote akiongelea hili ili hali hizo fedha wanazolipana posho zinategemea kodi za haya Makampuni.

Pia, Soma:

Uchumi bado Umekaza? Vodacom yajiondoa kudhamini Ligi Kuu Tanzania Bara

Nini kimeikumba Airtel? Wameuza minara yake yote na kugeuka wapangaji!

 
178909098.jpg
 
Miezi miwili iliyopita tulisikia Kampuni ya Millicom International Cellular SA (MIC) inayomiliki Tigo na Zantel imetangazaa kuwa imeingia makubaliano na kampuni ya Axian kutoka nchini Madagascar kwa ajili ya kuuza kampuni zake mbili za Tigo na Zantel kwa bei ambayo haijaweka wazi.

Mwezi mmoja baadaye nayo kampuni ya simu ya Vodacom ilisema hakutakuwa na gawio kwa wanahisa katika kipindi cha mwaka wa fedha ulioishia Machi, 2021.

Sababu za kutotolewa kwa gawio hilo ni hasara ya Sh 30 bilioni iliyopatikana katika kipindi hicho.

Kutokana na hasara iliyopatikana baada ya kulipa kodi, bodi ya wakurugenzi imeamua kutopendekeza gawio katika kipindi hicho cha mwaka wa fedha ulioishia Machi 31, 2021

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Vodacom, Hisham Hendi alisema hasara hiyo inatokana na namna kodi ilivyokokotolewa na kusababisha kutozwa kiwango kikubwa tofauti na mwaka uliopita.

Pia alibainishwa suala la kufungwa kwa laini milioni 2.9 za wateja wao ambao hawakukamilisha usajili liliathiri mapato na faida ya kampuni hiyo.

Ikumbukwe kuwa Katika kipindi cha mwaka wa fedha uliopita (ulioishia Machi, 2020) Vodacom ilipata faida halisi ya Sh45.76 bilioni ikipungua kutoka Sh90.76 bilioni iliyopatikana kwa mwaka ulioishia Machi, 2019.

Wakati hilo halijatulia, jana kampuni hiyo imetangaza kujitoa kudhamini ligi kuu ya Vodacom kwa msimu wa 2021/2022 kwa kile kilichoelewa kupata hasara ya sh30 bilioni.

Huko Airtel nalo hali si shwari, wiki iliyopita tumesikia Kampuni hiyo ya Airtel imeuza minara yake ya mawasiliano wanayo imiliki kwa ubia na kampuni mbili tofauti – SBA Communications Corp na Paradigm Infrastructure Ltd kwa $175 milioni (sawa na Sh400 bilioni).

Mpaka hapa haitaji elimu kubwa sana kujua hali ikivyo mbaya kwenye sekta hii ya mawasiliano inayoingizia nchi fedha nyingi.

Tunapoelekea itakuwa mbaya zaidi, leo wanauza minara, kuacha udhamini wa ligi, kuuza kwa kampuni, kesho tutasikia wamefunga wameondoka.

Hii sio ishara njema hata kidogo niitake Serekali kukaa na haya makampuni ya simu kuona jinsi gani ya kutatua hizi changamoto haraka sana.

Naona kama serekali imelala usingizi wa pono "Haijigusi" Sjasikia Mbunge yoyote akiongela hili ili hali hizo fedha wanazolipana posho zinategemea kodi za haya makampuni.

Pia, Soma:

Uchumi bado Umekaza? Vodacom yajiondoa kudhamini Ligi Kuu Tanzania Bara

Nini kimeikumba Airtel? Wameuza minara yake yote na kugeuka wapangaji!

 
Kama wanaona Kodi imekokotolewa vibaya waende TRA kuongea nao waelewane kama Rais alivyoagiza waache kulalamika.
 
Dikteta mwendazake aliharibu hii Nchi na Sera zake za kibabe, next time CCM wawe makini kwenye uteuzi wa wagombea, wawashirikishe hata taasisi ya usalama wa Taifa kujua Historia ya mtu kiakili hadi kiasili yake Kama Ni Mtanzania kweli
 
Airtel inayumba sehemu zote iliyopo Afrika na wameshatangulia kuuza minara kwenye nchi nyinginezo, Tigo wameamua kuondoka Afrika nzima na wameshauza hisa zake nchini Ghana. Kampuni za simu zilimeenjoy high time kwa muda mrefu, ni muda kujiadjust kuendana na hali. Kama serikali ikifikiria wa kuwanasua nadhani waanze na wadau walio kwenye sekta ya Utalii ambao tangu covid ishamiri wako juu ya mawe.

Wakijaribu tena kuja na vifurushi vipya yatawakuta ya last time na mama hana msuli wa kuwakazia wananchi kama mtangulizi wake.
 
Back
Top Bottom