Hali ni Tete, Mabomu Yameanza Kurushwa Tena Jijini Arusha

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,975
9,566
Polisi wanapiga mabomu ya machozi. Kuna gari limepigwa bomu mpaka limefumuka

===================================
UPDATES KUTOKA KWA MEMBERS WENGINE
===================================
Polisi wameanza kupiga mabomu wakati wabunge wa CHADEMA walipoanza kuhutubia maelfu kwa maelfu ya wafuasi wake. Hali ni mbaya sana hata watu wametelekeza magari na pikipiki zao, wabunge wote nao wamekimbia na mbaya zaidi wanapiga mabomu kila mahali.

Hali ni tete, mabomu yanarindima sana hali ni tete magari ya mevunjwa gari la Lissu laharibiwa, pikipiki zinavunjwa na polisi bila sababu. Hali tete, tegemeeni msiba mwingine

Wametumia risasi za moto kupiga watu, gari la Tundu Lissu limevunjwa vioo na jeshi la polisi. Wameumiza watu wengi sana! Hali ni mbaya sana!

Kufuatana na mgogoro wa serikali na wananchi wa Arusha, barabara inayounganisha kalolen na polisi central mpaka pale benki kuu arusha pamefungwa na inaonekana kuna pilikapilika nyingi central zinazoashiria hali si shwari Huku upande walipo wanaCHADEMA kukirindima mabomu...

Tahadhari wanaJF, msipite barabara hiyo kuanzia muda huu saa kumi na nusu ya tar 18 June 2013.

Kwa kweli hali ni ya hatari na wabunge kadhaa wa Chadema wameshikiliwa, polisi wanatumia nguvu kubwa kupita kiasi. Baadhi ya vyombo vya usafiri vilivyoachwa eneo la tukio polisi wanaviharibu kadiri wawezavyo. Usafiri wa abiria katika barabara ya Moshi-Arusha umesitishwa na hakuna gari zinazopita latika barabara hiyo. Majeruhi ni wengi na wamepelekwa hospitali.

Mabomu yalilipuliwa baada ya naibu mwenyekiti kuhitimisha kwa kuwaomba wananchi waliojikusanya eneo la Soweto waende ktk hospitali ya Mount Meru kwa ajili ya kwenda kuwaaga marehemu. Awali palitokea mabishano kati ya polisi na viongozi wa Chadema kuhusu mkusanyiko uliokuwapo hapo. Polisi walisema AICC wamekataa uwanja wao wa Soweto usitumike ktk shughuli yoyote. Bado vyombo vilivyoachwa uwanjani na wananchi vinaendelea kuharibiwa na polisi na baadhi ya wananchi wamejificha ktk fensi na baadhi ya nyumba zilizopo ktk uwanja huu.

WAKATI hali ikizidi kuwa mbaya jijini Arusha kufuatia mapambano ya raia na Jeshi la Polisi,Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema amelazimika kukimbilia kwa wachoma nyama ya Nguruwe, (kiti moto).

Lema ambaye alinusurika kupigwa na bomu lilorushwa na Askari wa Jeshi la Polisi na kuharibu gari lake alikuwa akijaribu kuwatuliza wananchi walioanza kukusanyika katika vikundu, wakijadii amri ya Serikali ya kukataza miili ya watu waliofariki Dunia katika shambulio la kigaidi isiagwe katika viwanja hivyo.

Kabla ya Lema kupigwa mabomu na kukimbilia kwa wachoma nyama ya nguruwe hao alikuwa akisema, "jaribuni kuvumilia tunajaribu kuwasiliana Serikali ya Mkoa, ili watupe kibali ya kuleta miili ya wapendwa wetu hapa, kuweni wastaarabu kwa sababu mbele yetu kuna wanausalama ambao wanalinda amani,ingawa kufa ni kufa tu, wenzetu wamesha kufa na sisi ipo siku tutakufa, lakini kila anayetangulia lazima tumzike kwa heshma zote"alisema Lema kabla ya kupigwa bomu na Polisi.

Kauli hiyo ilizidi kiwachefua Polisi ambao walishatangaza amri ya watu kutawanyika katika viwanja hivyo, kwa ajili kuweka hali ya usalama wa eneo hilo ambapo walisema kwamba hakutakuwa na suala la kuaga maiili ya watu hao katika eneo hilo.

Niko SELIAN HOSPITAL majeruhi ni wengi sana. Kijana mmoja utumbo uko nje na wengine wana majeraha ya risasi wamevunjwa mikono wengine miguu! This is TANZANIA !
 
Nipo Arusha, kuna taarifa zimezagaa mtaani huku Kijenge na Mwanama kwamba polisi anayetajwa na Mbowe ndiye aliyeua katika mkutano we Chadema Soweto Jumamosi, ni mtu aliyevalishwa nguo za polisi kimkakati ili kuchafua Jeshi la Polisi. Je hili limekaaje au ni propaganda tu za kisiasa?
 
Polisi wameanza kupiga mabomu wakati wabunge wa CHADEMA walipoanza kuhutubia maelfu kwa maelfu ya wafuasi wake. Hali ni mbaya sana hata watu wametelekeza magari na pikipiki zao, wabunge wote nao wamekimbia na mbaya zaidi wanapiga mabomu kila mahali.
 
Nambalapala,
Ushauri wako ungekuwa na maana zaidi ungeliuelekeza kwa kikwete na kwa IGP kuliko kwa Wabunge wa Chadema. Dunia ingelikuona una busara zaidi. Wananchi wanaomboleza, wanaenda kuwaombea wapendwa wao wewe unafikiria Polisi kutumia mabavu, sioni Kama kuna busara katika usemi wako. Wote wenye mawazo ya aina yako ni vema sasa wakaanza kufikiria na kupima dhamira zao. Ni nyie wenyewe siku zote mlikuwa mnazungumza kuhusiana na nchi jirani zilivyopoteza uvumilivu mpaka maelfu ya watu kupoteza maisha. Sasa mnayashabikia hayo hayo. Siku zote tumewaonya uvumilivu ukifika mwisho hakuna atakayepona. Mimi si nabii, lakini naona mnalazimisha Tanzania ifikie tusikopenda kufika. Kumbukeni Tunisia tukio la mtu mmoja tu kunyanyaswa na kujiua lilipelekea mabadiliko makubwa na kuiondoa Serikali. Wajinga wachache was na dhamira, kwa upuuzi tu wanashabikia matukio yanayoendelea. Ndugu zangu wenye mapenzi mema,Tunaanza na Mungu, Tuendelee na Mungu na Tumalizie na Mungu katika tukio kubwa la kuwaombea wapenzi wetu. Tupuuze wote wanaoleta ushabiki.

Mh.Dr.Slaa, hawa watu wamepigwa upofu kama Farao,HAWASIKII HATA KWA DAWA tutafika nchi yetu ya ahadi.Mungu anamakusudi yake kuwapa upofu.Watanzania tunakuombea maisha marefu na utukomboe tuko nyuma yako mkuu.Mwenye haki hajawahi achwa kamwe.
 
Mtu wangu wa karibu ananiambia mabomu ya machozi huko yanaria mbaya sana
 
upuuzi mwingine bhana, sasa aliefanya hivyo ni nani? CDM au CCM? Naona bado kuna gap hapa, tutulie kwanza CCM lazima wattotoka tu...sio kwa shari bali kwa HERI
 
fafanua mkuu, ikibidi tupia na picha. Nahisi Misri yako karibu. Tujuzeni kama vipi tuanze noma.
 
Hali ni tete, mabomu yanarindima sana hali ni tete magari ya mevunjwa gari la Lissu laharibiwa, pikipiki zinavunjwa na polisi bila sababu.

Hali tete, tegemeeni msiba mwingine
 
Polisi wameanza kupiga mabomu wakati wabunge wa CHADEMA walipoanza kuhutubia maelfu kwa maelfu ya wafuasi wake. Hali ni mbaya sana hata watu wametelekeza magari na pikipiki zao, wabunge wote nao wamekimbia na mbaya zaidi wanapiga mabomu kila mahali.
Ndo matokeo ya kuwa na Polisi na Watawala wasiotumia akili bali matumbo yao.Damn it ccm.
 
Back
Top Bottom