Kiwanda kikubwa kuliko vyote Afrika mashariki na kati na pengine cha pili Afrika kwa uzalishaji wa makaratasi 'MUFINDI PAPER MILLS' Kilichopo Mgololo wilaya ya Mufindi na mkoa wa Iringa Kimefungwa kwa muda usio julikana na vibarua 3100 kupewa likizo ya bila malipo huku wafanyakazi 503 wa kiwanda hicho kulipwa nusu mshahara.
Akiwa tangazia wafanya kazi wake Mkurugenzi mkuu wa kiwanda anaye fahamika kwa jina la MUHINDI amesema kiwanda kinakosa uwezo wa kuzalisha na kujiendesha kwa faida baada ya serekali kupandisha bei ya Magogo ambayo ndiyo malighafi kuu kwa kiwanda,alisema kabla ya kupandisha bei serekali ilipaswa kufanya Tafiti na kujiridhisha kabla ya kutoa uamuzi huu hivyo serekali ilikurupuka na kutumia ubabe katika maamuzi yake na wadau hawakushirikishwa na kwa kua soko la bidhaa zao lipo nje ya inchi kiwanda kinashindwa kushindana na viwanda vingine kwa kuwa wanalazimika kupandisha bei ya bidhaa zao huku wengine wakishusha bei! hivyo hakuna njia nyingine zaidi ya kukifunga kiwanda mpaka hapo watakapo fikia muafaka na serekali, na kuiomba serekali ipunguze ubabe!
Ikumbukwe kuwa Shamba la Miti la Sao hill lilianzishwa na JK Nyerere kwa minajili ya kuhudumia kiwanda hichi cha Makaratasi na pia kuzalisha Nguzo za umeme hapa inchini ambapo kiwanda cha Twico Mufindi kilipewa kazi ya kutengeneza Nguzo za umeme lakini Wizara ya Mali asili na utalii kupitia Shamba la miti la Sao hill lime acha kazi yake kuu na kujikita na shughuli za kugawa vibali kwa wachana mbao binafsi ambamo Inasadikika Rushwa ni sehemu ya Mtaji ya wafanya biashara hawa wa mbao.
Sasa kiwanda kimefungwa vibarua na wafanya kazi wanakosa mishahara sijui tunakwenda wapi na sera ya CCM ya maisha bora kwa kila Mtanzania.
My Take:eeeh! Mwenyezi Mungu ninaomba kura yangu iwe salama mwaka 2015.