Hakuna sababu Usalama wa taifa kubadilisha mfumo.

Keylogger

Member
Oct 13, 2016
13
14
Kumbe m-pesa iligunduliwa kenya tena na kijana aliekua anafaya internship safaricom?? aaah... kumbe keyboard yangu nzima haya tuanzee

Tangu kipindi cha mwisho cha kikwete kulikua na malalamiko ya watu kuhitaji mfumo wa usalama wa taifa au TISS kubadilika lakini malalamiko hayo yameongezeka zaidi mwisho wa mwaka 2017, kama mtanzania wa kawaida ambae pia nahangaika tafuta senti ili walau niifurahishe hii minyoo sugu ilionipa kijitambi cha kiaiana,dah ila sijui hizi dawa za minyoo tamutamu nazo feki??

Asilimia kubwa ya watu wanaohitaji mabadiliko makubwa huwa wanatolea mfano KGB kwenda FSB(Federalnaya Sluzhba Bezopasnosti) ni kweli Russia walifanya hayo mabadiliko makubwa kupitia raisi wao
kipindi kile Boris Yeltsin lakini kitu ambacho tunasahau ni kuwa rais Boris Yeltsin alikua na kautata na shilika la ujasusi kipindi kile KGB hivyo ikabidi aifumue KGB na ukisoma vizur vitabu vuzur utaona alianza kwa kuigawa katika agencies ndogo ndogo lengo lake kuimaliza nguvu, kuna vitabu vingi vinaelezea mabadiliko haya ila Boris alimteua ndugu Vladimir Putin kuongoza FSB, Putin alikua anafanya kazi KGB hivyo alivyoingia kwenye urais aliendelea kuijenga FSB hadi hapo ilipofikia sababu anaijua FSB anaijua ndani na nje hadi pembeni pembeni.

Kikubwa cha uzi huu mimi sioni sababu ya usalama wa taifa kubadili mfumo wao mabadiliko haya makubwa tunayoyahitaji huwa yana madhara makubwa vile vile sasa leo mimi najaribu angalia sababu kama mbili hivi ambazo inabidi tukibadili yatatukuta:
kwanza ugaidi au uharifu utaongezeka, mashirika yote ya usalama yaliyojalibu kufanya mabadiliko makubwa basi uharifu uliongezeka ndugu yangu msomi Yericko Nyerere kumbuka kule Russia KGB ilibidi ifukuze baada ya agenti ambao iliona hawafai walivyo ingia mtaani walikua wanafanya uhalifu tu na wengine walikua wanatumiwa na wale mabosi wa urusi na ndio maana urusi inaongoza kwa magenge ya waharifu wenye ujuzi wa hali ya juu

Pili kuvuja kwa siri, katika kitu ambacho TISS inajitahidi ni kutunza siri na huwa hazivuji hovyo ila ikitokea mabadiliko lazima siri zitavuja ndio huwa zinavuja ila zile ambazo hazina madhara

"Right decision come from experience and experience come from mistake" hahah..hatari sana kingereza kimenyooka utafikiri sijasoma mwakanyege sekondari skuli, mabadiliko tunayoyataka ni ya kiuchumi sana sana, TISS tunaomba ione tatizo hili na kama inawezekana ijiongeze yenyewe iangalie jinsi ya kuongezea hata depatment kingine namna mnavyoajiri, Yaani watu wanaofanya kazi TISS wanajikuta wao ndo wenye akili kuliko watanzania wote ilihali ukweli ni vilaza ndo wengi ndio maana wanafanya makosa ya kizembe!
Kitu ambacho kinaleta utata ni hizi skendo za hapa karibuni ambazo Dr Modestus kipilimba anaoneka anahusika nazo za kule NIDA kuhusu vitambulisho duuh..
 
Back
Top Bottom