Hakuna nchi duniani kila mtu anahutubia taifa, ni Tanzania peke yake

CalvinKimaro

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
244
312
Ujio wa teknolojia mpya ya kupashana habari na kuchipuka siasa taka nchini Tanzania kumeibua jambo ambalo lisipotafutiwa dawa linaweza kuja kutuletea majanga nchini. Kuanzia 2015 kumezuka tabia ya watu kujifanya wanahutubia Taifa. Na katika hali ya kushangaza mwaka 2019 mtu mmoja alijifanya anahutubia taifa kwa kutanguliza wimbo wa Taifa!

Akamalizia tena kwa wimbo wa Taifa. Maana yake halisi watu hawa wanafanya "impersonation"! Wanajifanya wao ni wakuu wa nchi! Sheria ya habari ipo na inatamka wazi nani ndiye anaweza kuwahutubia raia wa Jamhuri inayoitwa JMT.

Mtu mwingine yoyote anahitaji kibali. Ndio maana mfano Dar Es Salaam pakawekwa sehemu maalum kwa yeyote mwenye tangazo. Unatakiwa uombe muda na upeleke script yako pale Maelezo ihakikiwe.

Ujio wa teknolojia umerahisisha watu kuhutubia lakini haujabadili sheria! NI vyema sasa kila anayetaka kufanya press conference kupitia tools mbalimbali awekewe utaratibu. Ama sivyo iko siku atajiamkia mtu atangaze nchi imepinduliwa au mkuu wa nchi amekufa!

Si Idara ya Maelezo bado ipo tena kila mkoa? Si TCRA ipo?

Unaweza kudai je mtu akiwa nje ya nchi? Itakuwa hufahamu Internet inafanyaje kazi! Hawa kina YouTube na wenzao wana miiko. Serikali inaweza kuwataarifu kuwa ikitokea mtu anahutubia wasimruhusu mpake wapate clearance TCRA.

Sisi hatutakuwa wa kwanza kufanya hivyo. Mifano mzuri ni China, Morocco, Japan. Kina Google na YouTube hawawezi kufanya mchezo na wao. Watafungiwa kabisa. Na hawa hawajali kelele za haki za binadamu. Kwao ustawi wa nchi zao ni muhimu kuliko Uhuru wa jitu moja kutukana nchi!

Serikali chukueni nafasi yenu katika hili. Haiwezekani raia wahutubiwe na kila mtu! Tena wahutubiwe kujengeana chuki! Kama Sheria husika ilishafutwa basi haraka rudisheni utaratibu wa kuhakiki hawa "maraisi" feki!

Watakuja sababisha balaa!

Hakuna nchi duniani mtu yoyote anahutubia Taifa! Mmewahi kusikia Kenya, Uganda, Marekani, UK?? Kwa nini Tanzania iwe holela hivi? Kwani YouTube, Google, Twitter na Facebook ziko Tanzania peke yake?

Mchelea mwana kulia hulia mwenyewe!
 
A leader of official opposition has that right. Usiandike vitu ambavyo hauna uelewa navyo. Umetoa mfano wa Kenya wakati haujui kwamba Raila Amolo Odinga siyo tu kwamba ame address the nation lakini pia akisema kesho watu wasiende kazini, basi hawaendi. Ufinyu wako wa maarifa usiuanike. ' Do not air your dirty laundry in public"
 
Huyu hajawahi kufika Kenya akasikia ile Salaam ya
1. Wakenya tialala....jibu TIALALA
2. Wakenya tibim TIBIM
3. Wakenya ryah RYAH
 
"I've been all over the world, my boy, and everywhere I go people tell me about the 'true gods', they all think they found the right one. The one true god is what's between a woman's legs."
 
Sasa hivi wanalumumba wengi wanakuja na Id mpya zenye majina ya kichaga hahaha
 
A leader of official opposition has that right. Usiandike vitu ambavyo hauna uelewa navyo. Umetoa mfano wa Kenya wakati haujui kwamba Raila Amolo Odinga siyo tu kwamba ame address the nation lakini pia akisema kesho watu wasiende kazini, basi hawaendi. Ufinyu wako wa maarifa usiuanike. ' Do not air your dirty laundry in public"
Nilitaka kutia neno, naona umemaliza kilakitu hapa.

Mleta maada hii amekosa akili kabisa kama jiwe tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaka umeajiabisha sana, ulichokiandika hapa hukijui na hauna details za kutosha. Next time usiwe mvivu, kabla hujaja kuanika upumbavu uliokuwa nao kachimbe kwanza uwe na madini ya kutosha
 
Sasa hivi wanalumumba wengi wanakuja na Id mpya zenye majina ya kichaga hahaha
Hopeless comment ever! Haya tuambie na wale wazee wa Machame waliomkataa Mwenyekiti wako wa maisha Mbowe Mugabe siyo wachaga au unafikiri wachaga wote wanakubali usani wa Mbowe?
IMG-20200513-WA0020.jpg
 
Back
Top Bottom