Hakuna Mwenye Lake Jambo - Muungano ni kama koti.

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Hizi kauli za kutishana ni kauli za kuwambia watoto wadogo kuwa usiende huko kuna duma ! Jamani zama hizi ni za liwalo na liwe ,jamaa wamebakiza siku zinazoisabika ,na pia kiumri kwa alivyotabiri Mtume wetu Muhammad kuwa umati wake kufika miaka mia ni mbinnde ,nikiwatizama wakuu wa CCM wengi wao wamo katika extra time ,baada ya miaka kumi watakuwa kama wapo akili zao zitakuwa za kuunga unga ,kwa maana weshazeeka ,sasa hii leo kuzuka na kauli za watakauchezea Muungano watakiona ,hii si kauli nzuri ni kauli tegemezi yenye kuashiria kikundi fulani kimejijenga na kuwa tayari kulindana ,ndio ile kauli ya jeshi litachukua nchi.

Sawa kabisa jeshi na lichukue nchi ,kwa karne hii ni nchi ngapi jeshi limechukua nchi ? Na nini kilichofuatilia ,je waliokuwa madarakani walirejea na kuendelea na ukiritimba ? Nijuavyo Jeshi linapochukua nchi huwa halipo tena kumlinda aliekuwepo madarakani ,bali ni kamatakamata hata waliokuwa madarakani nao huchanganyishwa na kuwekwa kwenye mkumbo ,hao wanaopalilia jeshi kuchukua nchi basi wajue na wao hawatakuwa salama lazima jeshi litawatia mkononi kwani yote ya jeshi kuchukua nchi yasingefikia kama si kutokana na utawala wao mbovu. Wao ndio wahusika nambari one.

Kuna miungano kibao imevunjika na imebaki kuwa historia na huu muungano uliojaa mizengwe wa Tanzania ambao kuna nchi imejificha kama nchi hiyo iitwayo Tanganyika haitajitokeza na kuwepo kama ilivyo Zanzibar basi Muungano utakuwa mashakani. Haiwezekani kuwepo na Muungano halafu nchi moja ijichomeke ,haina katiba,haina Raisi haina chochote kile imoimo tu ni sawa na ile mimea inayojiotea kwenye matawi na mashina ya miti ,ni nchi mnyonyaji kinachoingia kwenye Muungano inakuwa ndio ya mwanzo kushiba. Huu ni Unyonyaji ,nchi hii ni kupe na nduo maana maendeleo na majumba makubwa makubwa yameanza kuonekana Tanganyika kuliko Zanzibar.

Kama muasisi wa Muungano Mheshimiwa Abeid Aman Karume alisema muungano ni kama koti nyie waleo hamna la kutuambia muungano kwa kipimo kilichofikia ni koti linalotubana ,ili kumuenzi Mheshimiwa Karume ni kutumia hekima hio aliotuachia ,Je tutakuwa tunauchezea Muungano ?????
 
CCM baada ya kuona koti linavuliwa wameanza kulihusisha jeshi katika mambo yao na hawajui kuwa wananchi wanapoamua basi jeshi linabaki kulinda mali za nchi lakini sio kupambana na wananchi ,si polisi si jeshi hawana ruhusa ya kuuwa wananchi na angalizo ikiwa wananchi watakusanyika hadi kufikia elfu moja tu basi ujue hapo ni walioko madarakani watimue zao .na chukulia mikoa yote ya Tanzania kwa pamoja wanaamua kuiondoa Serikali ya Muungano na kuihuisha serikali au kuweka madai ya kuitaka serikali ya Tanganyika iwepo ,yaani hakuna cha kura ya maoni wala kura ya upofu ni TUNATAKA TANGANYIKA yetu ,hapo ndipo maccm watakapojua kuwa embe ntunda. Wasitishe watu kwani la Tanganyika si la mojammoja ni la umma.
 
Kwa sasa sidhani kama kuna muungano bali kuna hadithi ya muungano,na wanasiasa wasipoangalia basi hata hiyo hadithi itakwisha.
 
Back
Top Bottom