Hakuna kujiua hadi kieleweke (Born Alone, Die Alone)

Abu Haarith

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
314
165
Habari wakuu katika siku nimehuzunika ni leo nimekutana na machapisho zaidi ya matano watu wanatujuza kuwa wanataka kujitoa uhai wao kutokana na hali ngumu za maisha wanayopitia

Naandika makala hii kwa ubabe kidogo sababu ya kukata tamaa kwa wachache wenye kupitia magumu

Zingatio: Wewe unaekata tamaa, hii ni kwasababu unatamaa ya kuwafikia wale wa juu kina Bill gate na mifano yao wakati huo umesahau kuwa yupo kiumbe dhaifu mno kukuliko ambae hata sumni ya kuchukulia kandolo hana lakini wewe mola wako amekumilikisha 20kb za kuperuzi pamoja nasi.

Nasema haya sababu najua maumivu yake sio kwamba nimekurupuka kutoa maneno haya haka ni kahadithi ka maisha yangu kwa ufupi..

Nina miaka 21 mpaka sasa baba yangu ni kivuli tu. Tangu amefariki mama yangu mwaka 2009 nilishindwa kuendelea na shule nilikatisha masomo yangu nikiwa kidato cha pili 2010.

Nikaamua kutoka mkoani Moro na kuelekea Dar, nilifikia kwa mjomba wangu lakini sikupata muhula wa kupumzika. Mbinde na hali ngumu za maisha zilianza, ilifikia kipindi siku mbili kijana sijatia rizki kinywani, sina elimu ya kuniwezesha kupata kazi, nilibeba zege, nilifyatua tofari ili maisha yasonge tusubiri ya Mungu tu.

Mola ni mwema baada ya mihangaiko ya miaka mitatu na miezi kadhaa nikapata kibarua cha kuuza gesi na simu ambacho nilifanyiwa msaada na mama Erick ambaye alikuwa kama dada yangu. Nilikuwa nalipwa tsh 30,000 Kula juu yangu. Kutokana na hali ngumu niliyokuwa napitia ilinibidi nikubaliane na mazingira.

Mitihani haiishi, baada ya miezi 3 asubuhi wakati nafanya usafi nje ya ofisi yangu majira ya saa moja, naibiwa robo tatu ya pesa ya mauzo ya simu,gesi pamoja na vocha. Lakini bosi alinielewa kutokana na utetezi wa majirani bt alinifukuza kazi na kunipatia Mshahara wa mwisho Tsh 30000.

Nikarudi kwenye shida za mwanzo za kukosa kula hata siku mbili. Mwezi wa 10 Tarehe 2, 2013 nikaamua kuhama mkoa, nilikuja Arusha nilifikia msikitini Elerai majengo.

Kama unavyojua hapa niliomba hifadhi ya kulala tu, nilifika na pesa Tsh 42000 tu. Hii niliwaza itanisaidia misosi wakati nikijaribu kufanya harakati za kupata mfereji wa kuingizia pesa.

Mitihani ni mitihani tu ndugu zangu, nilitumia pesa hadi ilikwisha bila kupata sehemu ya kuingizia pesa lakini Mungu hamtupi mja wake nilikuja kukutana na jamaa niliyemfahamu kwa jina la Yusuph, alikuwa ni dereva wa daladala, nilimuelezea habari yangu mpaka kukutana nae ndipo aliponiambia atanipa ukonda. Sijawahi kuufanya kazi ya ukondakta nilijisemea tu shida zinafunza.

Asubuhi yake alinichukua, nilihisi raha baada ya kupata milo mitatu na kujipatia kipato cha Tsh 3000. Ilikwenda hali hii kwa kipindi kidogo mambo yalikwenda mrama hatukuwa tukipata pesa mno, ilifikia kipindi hata pesa ya mafuta haitimii. Yusuph aliamua kunitimua.

Hakika ng'ombe wa maskini hazai! Katika kipindi chote nilichokuwa nae nilijitunzia pesa hadi ikafka Tsh 70,000 lakini ilikwisha bila hata kuelewa maana baada ya kuacha na Yusuph nilishakuwa mwenyeji kidogo, nilikutana na jamaa mmoja nimemfahamu kama Tamim, alinihifadhi katika chumba chake, ilinibidi niwe nachangia pesa kwenye chakula na kodi hadi leo sijapata muamala wa maisha yangu na sijawahi kufikiria kujiua.

Nimeona niwakumbushe tu kuwa si kila anayecheka na kuchapisha humu mitandaoni yuko vema kimaisha, hapana, wengine tunafuata ule husemi kuwa umaridadi huficha umaskini.

Siku zote ili usikate tamaa muangalie mwenye shida zaidi yako. Hakuna kukata tamaa ndugu zangu. Hapa ni kuangalia na kujiuliza nani atamfunga ajira kengele!?
 
Well said. Unakuta kijana wa miaka 20 au 30 anataka kujiua kisa maisha magumu...!

Duc in Altum
 
Daaah!!...mkuu pole

Maisha sio vita ya woga ukitaka kushiba lazima usikombe mboga #Fareed
 
Maisha ni safari ndefu usikate tamaa Mungu anapokupa ugumu katika maisha kuna mengi ya kujifunza kujua jema na baya kujitafakari na vitu vingine vingi
 
Dah hongera kwa kuchagua kua mpambanaji.ndio aina ya watu wanaohitajika Tanzania
 
Back
Top Bottom