Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,173
Hakimu ajitoa kesi ya Mahalu
Imeandikwa na Regina Kumba; Tarehe: 28th March 2011 @ 22:55 Imesomwa na watu: 47; Jumla ya maoni: 0
HAKIMU aliyekuwa akisikiliza kesi ya uhujumu uchumi ya kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh bilioni mbili inayomkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu na Meneja Utawala na Fedha, Grace Martin, amejitoa kusikiliza kesi hiyo.
Hakimu huyo, Sivangilwa Mwangesi ametangaza uamuzi wake huo baada ya kuombwa na washtakiwa kufanya hivyo, kwa madai kuwa wanaamini hawatapata haki mbele yake.
Kesi hiyo itatajwa tena mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Aprili 28, na kupangiwa hakimu mwingine kwa ajili ya kusikilizwa.
Katika uamuzi wake, Hakimu Mwangesi alisema washtakiwa walikuwa na haki ya kufanya hivyo lakini walitakiwa kutoa sababu za msingi zinazoelezea mwenendo wa hakimu katika kesi na sio uamuzi wake wa kisheria.
Alisema ameamua kujitoa kwa sababu anaheshimu maono ya washtakiwa ingawa sababu zote zilizotolewa na wakili wa washtakiwa, Mabere Marando kwa niaba ya wateja wake, hazikuwa na msingi wowote.
Mwangesi alisema anashangaa kwa nini mawakili wa washtakiwa hao hawakuwasilisha ombi hilo mapema, kwa sababu inaonekana ni muda mrefu wamekuwa na hofu hiyo.
Machi 25 mwaka huu kesi hiyo ilipokwenda mahakamani hapo kwa ajili ya utetezi, wakili wa
washtakiwa Wakili Marando aliwasilisha ombi la wateja wake kutaka Hakimu Mwangesi ajitoe.
Marando alidai kuna wakati upande wa mashitaka waliiomba Mahakama iruhusu shahidi wao atoe ushahidi kwa njia ya video akiwa nchini Italia na Mahakama ikiwa Dar es Salaam, upande wa utetezi ukapinga na hakimu huyo akakubali pingamizi hilo.
Alidai Bunge lilipitisha Muswada kuruhusu ushahidi kwa njia ya video kuchukuliwa na mshitakiwa Mahalu akiwa kama mwanasheria, aliona kuwa uamuzi wa Mwangesi ulikuwa wa
makusudi.
Sababu nyingine ya kuomba hakimu huyo ajitoe, ni madai ya upande wa mashitaka kuwasilisha mahakamani mkataba wa mauzo uliokuwa ni kivuli, ambao ulipingwa na upande wa utetezi lakini hakimu huyo akapokea nyaraka hiyo kama kielelezo.