MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,976
Kama kweli jamii yetu inajiendesha na kusimama katika misingi ya haki na usawa, kwa nini inakuwa ni taboo au kiini macho pale inapogundulika mwanamke kuwa ana mahusiano na mwanaume zaidi ya mmoja. Kwa nini mwanamke asipewe haki sawa ya kuolewa na mwanaume zaidi ya mmoja.
Kama sivyo, basi na wanaume wasiruhusiwe kuwa na mwanamke zaidi ya mmoja au wasiwe na kasumba ya kuwa wao kuiba pembeni ni sawa na kwamba wanawake wako tayari kuwasamehe pindi wakigundulika lakini kwa mwanamke kufanya hivyo ni NO, NO, NO na talaka.
Kisa cha mwanamke anayeitwa Veronica Saleh 'Mama Kaela' anayeishi katika kijiji cha Ikandamoyo, jimbo la Katavi, kama ilivyolipotiwa katika gazeti la Habarileo kuolewa na wamaume wawili kinatufundisha jambo kuu na la msingi kuwa hili linawezekana katika jamii yetu. Kama haliwezekani basi lisiwezekane kwa wote (mwanaume na mwanamke).
Kama tunakubali binadamu ni sawa na haki kwa wote basi haki hiyo iwe ni sawa kwa binadamu wote.