haka katoto mi nakapendaga!

JOKATE ANAJIBU: Si kweli hata huyo mtu simfahamu kabisa.

Vipi kuhusu mtoto wa kigogo?
Jokate namfahamu kama mtangazaji na aliwahi kuongoza jopo la warembo waliopo kambini kule Paradise Bagamoyo mwaka jana, ana uhusiano na mtoto wa kigogo mmoja hapa nchini tena mtu mzito.
Mimi Luis wa Arusha 0713-747744

JOKATE ANAJIBU: Nilikuwa nikiandaa vipindi vya Vodacom, sikwenda Paradise kwa ajili ya kufundisha warembo. Sina uhusiano na mtoto wa kigogo.

Ni mwanamuziki wa kwaya
Jokate anaimba kwaya ya vijana, misa ya Kiingereza katika Kanisa la Mt. Petro, Oysterbay ni mnyenyekevu na mtulivu awapo kanisani. 0717-648664
JOKATE ANAJIBU: Ni kweli kabisa ni muimbaji mzuri wa kwaya. Yupo tayari kuingiza sauti Bongo Flava.

Jokate ni model wa ukweli na mtulivu sana hata kama ana uhusiano siyo ule wa kisifa ni mpole na mnyenyekevu, sijawahi kusikia skendo hata moja, napenda uingize voko kwenye wimbo wangu nitafute. 0713-413681
JOKATE ANAJIBU: Nipo tayari ila nataka niusikilize kwanza huo wimbo ndiyo tufanye kazi.

Alivyoonekana utotoni ni tofauti na sasa
Jokate ni msichana mrembo wa kweli aliyependa fani hiyo toka utotoni, watu tunaomfahamu tulimtabiria hilo kwa kuwa ni ‘smart' tangu utoto na alikuwa na kawaida ya kutembea kama miss akiwa na umri mdogo kabisa. Namfagilia kwa kujilinda na skendo, kwa jinsi alivyo wengi tulidhani angeongoza kwa skendo. Namshauri aendelee hivyo hivyo.
Mimi Linda wa Mikocheni 0716-722137

JOKATE ANAJIBU: Ni kweli nilikuwa nafuatilia urembo toka utoto na wengi waliokuwa karibu yangu walidhani hivyo na walijua nikibahatika kuwa mrembo nitakuwa mtu wa majivuno kwani wengi walikuwa wakiniambia lakini imekuwa tofauti.

Ni mpole, mpenda watu
Ninavyo mfahamu mimi Jokate ni mpenda watu, mpole na mnyenyekevu
Mimi Silagi wa Misungwi Mwanza 0759-052861
JOKATE ANAJIBU: Ni kweli napenda watu na sipendi kukerwa na ninajitahidi kumaliza tofauti na mtu yeyote niliyemkosea

Ndoto zake ni kuwa Rais wa kwanza mwanamke TZ
Ni msichana anayejiheshimu na anafahamu anafanya nini, anamapenzi sana na wazazi wake, na hilo linamfanya ajilinde na kutoharibu jina la ukoo wake, anapenda sana kuwa Rais wa kwanza mwanamke Tanzania.
JOKATE ANAJIBU: Ni kweli ni ndoto zangu ni kuwa Rais hata kama sio wa kwanza mwanamke Tanzania ila hilo lipo katika akili yangu Mungu akinijalia.

Vipi penzi lake na Kipanya?
Jokate ana uhusiano wa kimapenzi na Masoud Kipanya Mimi Dina wa Singida
0716-867536

JOKATE ANAJIBU: Si kweli, sina uhusiano na Masoud ila aliniita nikawe jaji wa Maisha Plus, hakuna kingine zaidi ya kazi.

Ni mwanafunzi wa Loyola High School
Aliwahi kusoma Loyola High School Mabibo na alikuwa mkali sana darasani 0719-222327
JOKATE ANAJIBU: Ni kweli kabisa

Ni mfano wa kuigwa na mastaa wengine
Ni mdada mzuri na mwenye tabia njema ni vigumu kwa super star kuwa na maadili yanayokubalika na jamii. Huyu ni mfano wa kuigwa. 0652-285746

JOKATE ANAJIBU: Nashukuru nyie ndiyo manaonitazama.

Jina lake ni muungano wa herufu za majina ya wazazi wake
Jokate jina lake limetokana na kuungana kwa majina ya wazazi wake, anachukua stashahada ya Political Science, ni mcheshi anayejiamini na mwenye akili sana, amesoma St.Anthony na alikuwa dada mkuu msaidizi na Loyola alikuwa Head Prefect 0718-381549

JOKATE ANAJIBU: Ni kweli jina langu limetokana na muungano wa jina la Bibi na Babu yangu waliomzaa mama yangu, ni kweli nachukua Stashahada ya Political Science.

Penzi lake na prodyuza vipi?
Ninavyomfahamu mimi Jokate amewahi kula uroda na producer wa bad number records, Chris Khaly na uhusiano wao bado unaendelea kwa siri juzi walikutwa wako pamoja.
0718-935359

JOKATE ANAJIBU: Simfahamu huyu mtu jamani, naomba nieleweke, si kweli kabisa.

Ni binti mchamungu
Ninavyomjua Jokate anapenda watu, anapenda kumcha Mungu yuko mstari wa mbele kwa mambo ya Mungu, kwa kweli binti anajiheshimu sana.
0713-640491

JOKATE ANAJIBU: Najitahidi kwa kweli kumuomba Mungu.

Eti asili yake ni Magole, Moro
Jokate anatokea Magole mkoani Morogoro. Mimi ni Salama wa Buguruni 0713-924996

JOKATE ANAJIBU: Si kweli natokea mkoani Ruvuma.

Ni kweli alikuwa girlfriend wa huyu?
Jokate alikuwa demu wangu lakini baada ya kuingia kwenye u-miss alinikana, ila ni msichana mpole sana ila anahasira na dharau. Mimi Elvc wa Sinza 0717-400909
JOKATE ANAJIBU: Nakuomba uwe na uthibitisho, ninauhakika sikufahamu kabisa.

Ni mwanamke shupavu anayejiamini
Ninavyomfahamu mimi Jokate ni msichana anayejiamini sana kwa kifupi ni shupavu na huwa hana analoliogopa ilimradi liwe linawezekana. Anaweza kuwa mama bora wa familia.
Mimi Othumani wa Iringa 0713-299636

JOKATE ANAJIBU: Nashukuru kwa kuniombea mazuri nami pia natamani kuwa mama bora wa familia.

Amewahi kutoka na FA?
Amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na MwanaFA, akamsaliti na kumtungia wimbo wa Bado Nipo Nipo. 0756-736096
JOKATE ANAJIBU: Si kweli, ila hata mimi niliwahi kusikia kutoka kwa rafiki zake na maneno hayo yakasambaa bila wenyewe kujua yametoka wapi, ila ni rafiki yangu wa kawaida tu.


Source: http://www.globalpublisherstz.com/2009/09/28/jokate_mwegelo_afafanua_uhusiano_wake_na_mwanafa.html

full.php
 
kama ulikuwepo kuna kenzie haka hapa yani hivi vitoto viwili vinansuuza roho vibaya ,naviota kila siku,sijui ntavipataje,usikute mapedeshee washaharibuharibu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom