Haileti maana mtu amekufa Mtwara muanze kuhangaika kusafirish mwili hadi Arusha, au mtu kafa Kagera muanze kuhangaika kupeleka mwili Mbeya

Ricky Blair

JF-Expert Member
Mar 13, 2023
391
873
MISIBA YA BONGO

Wawe Wakristo, Waislamu au hata wasio na dini rasmi ambao Watanzania tunapenda kuwaita Wapagani utadhani kitu kibaya, kitu kimoja ambacho kinatuunganisha kama binadamu wote popote ni Kifo na kwamba siku moja wote kitatubeba tukitofautiana Ratiba tu. Kuna ambao wanafariki wakiwa watoto wachanga bila hata kupita siku au wanaofariki siku chache, wiki au hata miezi kwa madhara tofauti mengi yao yanazuilika.

Wengine wanafariki wakiwa watoto wadogo bila kufika balehe, wengine vijana wadogo au wakubwa na wengine wa lika la kati kati na mwishowe wazee ambao binadamu wengi tunatumai tufie uko uzeeni ambapo miili yetu ishatuchoka na kutusaliti kama viungo vyetu vingine vyote na kwa ustaarabu wowote wa kuendelea kuishi muda huo unakuwa muafaka wa kuondoka na kwa jamii zingine hadi wanaruhusu wazee hao kuondoka kwa jinsi wanavyotaka kwa kusaidiwa na daktari;

Yaani kufa kwa kujidhania kwani hakuna maisha yaliyobaki ya maana kama mwili wako ushakuchoka na hii pia hutumika hata kwa wale wanaoumwa magonjwa sugu na haina tiba kama kansa na wakiteseka sana.

KIFO HAKIKWEPUKI

Basi sasa mpaka sasa tunajua kwamba Kifo ndo Mungu wetu pekee ambaye anatuunganisha binadamu wote; uwe unaamini kuna Mungu Mmoja kama wana wa Abraham wale wafuasi wa Uyuda, Ukristo au Uislamu au wale wanaoamini Miungu mingi kama Wahindi na watu wengi duniani kabla ya ujio wa Hadithi ya Mungu Mmoja au wale wanaobudu Asili na kila kilichokuwemo ndani yake iwe bahari, Sayari yenyewe, Porini na vinginevyo, na pia kuna wale tusioamini kuna Mungu au miungu yoyote na wote tunajua tutakufa ingawa tunatofautiana kwenye kuamini kinachofuata.

Kwa wasioamini kuna Mungu au Miungu wanaamini maisha yao yanaishia wakifa na basi yaani tunarudi kwenye asili kama ilivyokuwa zamani kabla hatujazaliwa yaani hatukuwepo na tunarudi kwenye kutokuwepo tena, hakuna kuhangaika wala mateso wala furaha huhisi kitu.

Kwa wale watu wa Mungu au miungu ndo wanaamini kuna maisha mengine baada ya kufa na wengine wa kuenda kuchomwa moto kwa dhambi zao duniani au peponi kwa tabia zao nzuri yote inategemea na uyo Mungu wao akiwa na mudi gani bila kuwachoma wote kwa sababu yoyote. Wengine kama Wahindi wanaamini ukifa unabadilika kuwa mtu mwingine au hata mdudu au kitu kingine chochote kiishiyo duniani na kuendelea na safari yako.

Ivyo basi wote hatukatai kwamba Kifo kipo, ivyo basi kwa nini Tanzania kama sio Afrika nzima kwa ujumla tumejaa na woga na au kutokubali kwamba kifo kipo na kitatuchukua muda wowote tupende au tusipende? Iwaje mtu anawaza kujenga nyumba, bima ya afya, kuweka pesa benki sijui kusafiri sijui nini lakini kwenye akili yake ameiziba kitu kimoja ambacho hakikwepuki; KIFO.

Kwa nchi masikini kama Tanzania na ujamaa wetu misiba, maharusi na sherehe nyingi zinatumaliza sana na watau hatutaki kuzifanyia kazi ipasavyo kwa hofu ya kuitwa mbaili, mchoyo au mbinafsi. Harusi inatakiwa kuwa kitu binafsi kati ya walengwa wawili tu na hata iyo ya kuwataarifu wazazi au ndugu ni ili wajue upo na nani ila hauhitaji baraka zao kwani kama nyie ni watu wazima mkishaamua imepita wapende wasipende na hata hii tamaduni ya mahali pia ife kwani hamna mtu anayemnunua mtu aliyeridhia; hakuna mtumwa hapa. Kwaiyo wanaweza kufunga ndoa ya kanisa, msikiti au ya serikali bila kualika makundi ya watu na kupoteza au kufanya watu wapoteze hela kwenye michango kwa furaha ya watu wawili tu.

Msiba pia iwe ivyo, mtoto akishazaliwa wazazi waweke akiba ya mara moja tu ya kifo kama ambavyo wao inabidi wajitaarishe kwa vifo vyao muda wowote kwani hatuna Ratiba rasmi ya Kifo. Tunaweza kutumai tufe wazeeni lakini kuna magonjwa, ajali, vita, ugaidi, majanga ya asilia na visa vya binadamu wenzetu hivyo lazima tuwe na akilia ya kujitaarisha muda wowote. Haileti maana tuna bima ya afya lakini hatuna bima ya kifo wakati tunajua Kifo hakikwepeki. Najua watu wengi sana wanaogopa kifo kwa sababu wote ambao hatujafa hatujui nini kinakuja zaidi ya hadithi tu tulizorithi tunaenda wapi au wapi ila bado ukweli upo pale pale kipo na tutapotea tu siku moja. Hivyo basi kuliko kuhangaika na hizi rambi rambi kila siku kila kona, kila ndugu au rafiki akifa kila mtu awe na bima yake ya kifo kwamba akifa popote azikwe iwe ndani ya nchi au nje ya nchi.

Haileti maana mtu amekufa Mtwara muanze kuhangaika kusafirish mwili hadi Arusha, au mtu kafa Kagera muanze kuhangaika kupeleka mwili Mbeya na hapo bado ukoo mzima usafiri na michango ya watu na uwalishe watu wote hapo wakati marehemu ameshakufa. Baada ya kupoteza pesa zaote izo kwa watu ambao ni maskini kabisa au wa hali ya kati ni kheri mtu mmoja ndugu wa karibu au ndugu wa karibu wasafiri na waende kumzikia uko kwani kwa wanaoamini Mungu iwe Uislamu au Ukristo Ardhi ni ile ile tu na anaweza kuzikiwa popote pale na kuuleta mwili alipozaliwa sijui haitomrudisha dunianiwala kujenga kaburi kubwa na picha yake haitoondoka ukweli kwamba hayupo tena.

PESA NYINGI ZINAPOTEA KWENYE MISIBA

Misiba mingi kama Harusi inakula sana watu hela ambazo hawana na hawana mbadala. Hata hayo majeneza pia sijui nini kujenga kaburi ni kupoteza hela bila maana kwani tukikubali mtu kashakufa na hata mumweke kwenye jeneza la dhahabu na kaburi la Almasi uyo marehemu ataoza na ataliwa na atarudishwa kwenye Ardhi tu. Mimi ningeshauri tuwazike tu kwenye ardhi yoyote ya karibu iliyopo kwenye halmashauri au hata nyumbani kama amefia uko na kupanda miti au maua na kumkumbuka kwa picha au digitali ambazo tunazo sasa kuliko kuhangaika na majeneza au makaburi wakati binadamu tukifa tunakuwa mbolea nzuri sana kwa mimea au miti na pia hii hali ya kujijengea makaburi ni hadithi za binadamu kujifanya wa maana sana kwenye asili.

Jiulize wanyama wangapi au wadudu wangapi wanakufa tu kila siku na wengine tunawaua kwa chakula au kwa raha tu na hawana makaburi kwaiyo sisi ni nani kutaka huo umaarufu na swaga.

Kama unaamini Mungu yupo haijalishi sana unazikwaje kwani utaenda uko na kukutana naye hata ukiliwa na mamba, kulipuliwa na bomu au kupotea kwenye matetemeko ya Ardhi mwili hauwezi kuupata ivyo mnaendelea tu na maisha. Ivyo sioni maana ya kwa mfano mtu kafia Brazil, Marekani au Ulaya watu wachangishane sijui milioni ishirini kuusafirisha huo mwili wakati ndugu mmoja anaweza kwenda kumzika kule kule tu( na hapo kama akipewa visa) asipopewa basi wamuachie wamzike tu kule, cha muhimu tuwe na makubaliano ya kimataifa pia mtu akifa popote kuwe na uwezekano wa kumzika popote kwani sio lazima kaburi na kama nilivyosema awali wote tutarudi kwenye asilia na wanaokufa au tutakaokufa bado tutakuwa wengi kuliko wanaondelea kuishi ivyo izo sehemu sijui za makaburi hazitotosha. Tuanze utamaduni wa kuzika sehemu asilia bila kuwekaweka majina na kujenga kaburi. Pili kufanya misiba mifupi na kwa walengwa wa moja kwa moja tu mfano Mama, Baba, Dada na Kaka kuliko ukoo wote na hapo tutaokoa pesa nyingi na muda kwani tunaweza kufarijiana kwa njia nyingi kuliko maigizo ya watu kuja kujiliza kwenye msiba usiowahusu hadi unakuta mwenye msiba ndo ambembeleze watu baki; hii si sawa.

Au unakuta watu wengine wanachukua nafasi hii ili waweze kula bure tu na mambo mengine.

Pia tunaweza kuiga utamaduni wa India, China au Japan ambapo takribani asilimia themanini hadi tisini na tisa wanachomwa moto na kuwekwa mabaki kwenye chupa kisha unabaki nayo nyumbani au unaweza kuitupa baharini. Hii itapunguza kero nyingi za uzikaji, majeneza na makaburi. Watu wengi wa dini za Abaraham wataipinga sana hii kwa kuona ni tamaduni za kipagani na ushetani kwani binadamu anatakiwa azikwe ili aende akutane na Mungu wake akiwa kama alivyo, ingawa wanajua ukienda kufukua siku chache mtu ashaoza na pia ukiwapa mifano ya waliokufa majini au kwenye bomu wanadai Mungu wao atawarudisha vizuri.

Sasa kama ndo ivyo basi waamini Mungu uyo uyo anaweza kuwarudisha watu waliochomwa kwani kama kaitengeneza dunia kutoka hamna kitu mpaka watu wote na asili yote basi atawarudisha na hao wengine. Wengine watadai kuchomwa moto inatisha; hawa watu bado wanadhani ukifa bado upo usingizini na utahisi yote yanayotokea; ila ukishakubali ukifa haupo tena yaani hata uchomwe kisu au uchomwe hutohisi kitu basi hamna cha kuogopa.

Tungekuwa na teknolojia iliyoendelea sana tungeweza kuacha wosia ili tukifa miili yetu ipelekwe mahabari itumike kama mafunzo kwa wanasayansi wengine au itolewe viungo vyote vinavyoweza kumsaidia aliyekuwa hai, ivyo sasa kwa wale wote tulio hai ni lazima tuseme tunataka tuzikwaje kwa wosia ambayo ukifa mwanasheria wako au serikali itatekeleza hata kama Familia yako haitaki ivyo ningeomba tuondoke au tuache wosia usio sababisha msongamano wa watu au michango kila kona na iwe ya haraka na uzikwe popote pale Tanzania au nje ya Tanzania.

Kwa mfano mie nikifa nishawaambia watu wangu wa karibu sitaki msiba, bali nichomwe na mabaki yangu yarushwe baharini, sitaki kaburi, jeneza au jina langu popte hata wakinizika wanizike popote karibu na wapande mti au maua kwishnei hayo mengine kama kuna Mungu au nini tutajua mbele kwa mbele. Asanteni sana.
 
Sasa wewe unawashangaa Hawa? Kuna jamii I think iko Ghana au Nigeria kama umefia mjini huko na kijijini kwenu hujajenga basi utawekwa hadi nyumba ijengwe na maiti yako iingizwe humo ndio safari ya kuzikwa ianze
 
Sasa wewe unawashangaa Hawa? Kuna jamii I think iko Ghana au Nigeria kama umefia mjini huko na kijijini kwenu hujajenga basi utawekwa hadi nyumba ijengwe na maiti yako iingizwe humo ndio safari ya kuzikwa ianze

Hii hata kwa wachaga ipo
 
Hii mada imechelewa kuletwa,ilitakiwa iletwe mwezi kama huu miaka miwili iliyopita, means yalikua ni makosa kutembeza ile kitu nchi nzima nhe!,ilikuwa iwe straight kinondoni cementry, no pale pamejaa...mabwepande
 
Umasimini naona unakusumbua. Sisi lazima tusafieishe Ili wale mlioshimdwa kueudi kijijini kwemu mpate lifti ya kwenda kusalimia

Notel kijinini kwetu ni 1500km kutoka jiki la mashoga Dar
 
Nadhani kuzikwa kwenu Kuna heshima na umuhimu especially kwa waliobaki. Ingawa kama hukujiandaa ni changamoto. Inabidi tumalizane na wewe kimjinimjini.
 
Kuacha kitu inaitwa tamaduni ni Kazi Sana
sema Mambo ya uzungu yanakua mengi Sana hadi yanaharibu maana asilia ya misiba yetu
 
Si unajua ukishakufa yote juu ya mwili wako na maziko yako ni kama watakavyoona au watakavyopenda wapendwa wako. Wanaweza wakaona kuchoma maiti moto ni jambo baya. Hivyo usiwape masharti sana. Waachie uhuru wao ndio wanaohusika na mwili wako siku ikifika.
 
Pamoja na kuandika utopolo mreefu ni hivi;

Watu wakifa, huungana na kuishi kimila, na Kuna lugha ya mama ile ya asili tuu ndio hutumika.

Ukizikwa kwenye koo, au kabila nyingine tofauti na walipolala wenzako, utaweweseka na kuteseka Sana maana utaishi katika urika wa wasio kutambua ki lugha na kitamaduni. Kumbuka hata kama ulijifunza baadhi ya lugha au tamaduni za sehemu nyingine na ukazikwa pake, ile inafutika unarudia ile ya asili yako. Kumbuka waliokuwa roho zao hazina ufahamu kama sisi ila wanaishi katika Hali Fulani ya uzezeta lakini Kuna fahamu Fulani wanakuwa nayo na wanaweza kurudi duniani pale kwenye asili Yao kiroho na kuona kinachoendelea.

Ukizikwa sehemu nyingine utaleta mateso, na mabalaa kwa wale ndugu wslioidhinisha su kushiriki kukuzika ughaibuni kwani Kila ukipata shida ,unahamishia noma kwa ndugu
 
Pamoja na kuandika utopolo mreefu ni hivi;

Watu wakifa, huungana na kuishi kimila, na Kuna lugha ya mama ile ya asili tuu ndio hutumika.

Ukizikwa kwenye koo, au kabila nyingine tofauti na walipolala wenzako, utaweweseka na kuteseka Sana maana utaishi katika urika wa wasio kutambua ki lugha na kitamaduni. Kumbuka hata kama ulijifunza baadhi ya lugha au tamaduni za sehemu nyingine na ukazikwa pake, ile inafutika unarudia ile ya asili yako. Kumbuka waliokuwa roho zao hazina ufahamu kama sisi ila wanaishi katika Hali Fulani ya uzezeta lakini Kuna fahamu Fulani wanakuwa nayo na wanaweza kurudi duniani pale kwenye asili Yao kiroho na kuona kinachoendelea.

Ukizikwa sehemu nyingine utaleta mateso, na mabalaa kwa wale ndugu wslioidhinisha su kushiriki kukuzika ughaibuni kwani Kila ukipata shida ,unahamishia noma kwa ndugu
Ukishakubali ukifa haupo tena; hayo mengine yote hayana maana
 
Kwa mfano mie nikifa nishawaambia watu wangu wa karibu sitaki msiba, bali nichomwe na mabaki yangu yarushwe baharini, sitaki kaburi, jeneza au jina langu popte hata wakinizika wanizike popote karibu na wapande mti au maua kwishnei hayo mengine kama kuna Mungu au nini tutajua mbele kwa mbele. Asanteni sana.
Wewe ukifa hutakuwa na maamuzi yo yote yale, walioko hai ndiyo wataamua nini cha kufanya.

Usisumbue watu kuwaambia wakuchome wakati kwetu hakuna utamaduni huo, itabidi wapate mabaniani ndiyo wakushughulikie.
 
Siwezi soma ujinga huo ujaona jamaa alifia ukreni mpiganaji wa urusi yule mfungwa serekali ya ukreni ilisafirisha kwenda maiti yake hadi urusi kisha urusi ukasafirisha hadi kwao tanzani nayo serkali ikasafirisha kwenda kwao mkoani kisha mkoani nao wakaupokea kwenda kijinn kwao kisha akazikwaa kwa maana hyo mwili wako ni wa dhamini san .wahindi pekee na wachina ndio usika popote

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom