Haijilegezi

chamilo nicolous

JF-Expert Member
Mar 10, 2016
1,991
1,364
KAZA BUTI
Scandal; Ni nemo la kiingereza linalomaanisha tukio lilotendwa na mtu lililo kinyume na taratibu.Maranyingi tukio hili ufanywa kwa kificho na watu wachache wanaliibua au wanalifumania.
Skendo huwa ni mbaya Sana, Skendo zimemaliza watu, zimeharibu maisha ya watu na pia zimewafanya watu wawe maadui

Skendo inaweza kuwa kitu kimetendeka kweli au hakijatendeka. Epuka Skendo, kaa mbali a Skendo

NAMNA YA KUEPUKA

1- JIHESHIMU
- Mtu ye yote ambaye anajiheshimu siyo rahisi kumkuta na Skendo kwamba kafanya hivi, mara katenda haya, mara katembea na huyu. Kwahiyo ili ukwepe Skendo unapaswa kujiheshimu wewe mwenyewe. Skendo zitashindwa kutajwa juu yako kwasababu ya namna unavyojiweka wewe mwenyewe

2- CHAGUA WATU MAKINI WA KUAMBATANA NAO
-Tembea na watu wanao jielewa, watu ambao wanajua kipi kinatakiwa kufanywa, watu wenye malengo, watu ambao hupenda kujiheshimu. Watu makini hutasikia wakiwa wanahusishwa na Skendo Skendo, hutakuja kusikia Mara katembea na Fulani, Mara katukana, Mara kaiba, mara kapigana na mtu.

3- KUWA NA HOFU YA MUNGU
-Hofu ya Mungu hufanya kazi ya kuzuia watu wasifanye mambo yale ambayo kiuhalisia ni kwako kwa Mungu. Hofu hiyo itamwongoza mtu kutembea katika njia sahihi. Kumbe Sasa ili ukae mbali na Skendo omba Mungu akuzidishie hofu yake ndani yako

4- ITAMBUE THAMANI ULIYO NAYO KATIKA JAMII INAYOKUZUNGUKA
-Kitu kingine cha kufanya ili ukae mbali na Skendo ni wewe kuitambua thamani uliyo nayo katika maisha yako na katika maisha ya watu. Unatakiwa ujue kwa namna gani watu wanakutegemea? Kwa namna gani watu wanahitaji msaada wako, kwa namna gani watu wanasubiri uwe kiongozi ili shida zao zisemwe mahali pa juu? Ukiweza kuijua thamani yako nakwambia Skendo kwako sitakuwa stori tu

HASARA ZA SKENDO

1) Ni rahisi kufukuzwa kazi

2) Watu watapunguza kukuamini

3) Heshima yako itashuka

4) Kujiamini kwako mbele ya watu kutashuka na utaanza kuonekana ni mtu wa kawaida tu

5) Utaanza kujidharau wewe mwenyewe

Kaza_Buti_Maisha_ni_vita
 
Back
Top Bottom