Hadithi za Alfu Lela Ulela

mangonifera indica

JF-Expert Member
Dec 2, 2017
845
1,462
HADITHI ZA ALIF LELA U LELA

HADITHI YA ALADINI NA TAA YA MSHUMAA WA AJABU

Hapo zamani katika nchi moja kulikuwepo na mshona nguo yaani fundi cherahani. Fundi huyu alifahamika kwa jina la Mustapha. Mustapha alikuwa na umri 17 toka aanze kati ya kushona. Amekuwa ni fundi maarufu na mwenye kuaminiwa. Mustapha alikuwa na kaka yeke aliyefariki zamani pindi alipokwenda nchi za jirani kibiashara na kuvamiwa na mabedui wa jangwani. Huwenda hii ndio ilikuwa sababu ya yeye kujikita kwenye ushonaji na kutofikiria biashara. Siku zote Mustapha aliwaonya watu wa karibu naye waachane na kuwaza biashra za mbali

Mustapha sasa ana miaka 58 akiwa na mke wake mpezi. Wote walioana wakiwa vijana na sasa wamezeheka wote bila wakiwa na mtoto wao mmoja na wa pekee. Mtoto wao alitambulika kwa jina la Aladin. Aladini alilelewa kwa upendo sana na wa hali ya juu. Huwenda ni kwa sababu kuwa Mustapha hakuwa na mtoto mwingine. Aladini hakujishughulisha na chochote katika uzalishaji wa mali. Alizoea kula na kulala kwa mama na baba. Na baba alikuwa akimsisitiza aladini asiwaze kabisa kufanya biashara. Huwenda ni kwa sababu ya yaliyomkuta kaka yake

Aladini hakumjuwa ndugu yeyote wa baba yake, na hali hii pia ni kwa mke wa mustapha ambaye hakumjuwa yeyote katika ndugu wa munewe. Ila amefahamu kuwa mumewe alikuwa na ndugu aliyefariki akiwa kwenye biashara. Aladini alikuwa ni mtoto mvivu na asiyefanya kazi. Aladini alikuwa n I mitu na mpenda michezo na ni mkomvi japo hakuwa na nguvu za kujitetea. Mji mzima ulimfahamu aladini kama mtoto mpumbavu na mtukutu. Aladini sikuzote alijivunua kuishi na wazazi wake, na hasa [ale anapohitaji kitu haraka wazazei wake humpatia. Aladini alimpenda sana baba yake na mama yake

Maisha siku zote yanaendelea hata kama wengine wanadhulumu n kudhulumiwa. Hata ikiwa wengine wana kufa na kufiwa huu haukuwa mwisho wa maisha na dunia. Na hali ndivyo ilivyokuwa kwa upande wa Aladini, baba yake alifariki ghafla. Wakati huo Aladini akiwa na umri wa Miaka 21. aladini mvivu, mgomvu na mtukutu sasa amefiwa na baba. Aladini ameachiwa ulezi wa kumlea mama yake aliyekuwa ni mzee. Kila akifikiria haya alijuta kuchesea umri wake, alilia sana hata kufikia kukufuru kwa maomboloezo yake. Watu walimfuata kumsi. Mazishi yalifanyika na hakuna hata ndugu wa Mustapha aliyekuja

Hatimaye siku za matanga zikaisha na watu wakaendelea na shughuli zao. Aladini kila akiangalia mashine ya baba ya kushonea hakuwa na majibu sahihi. Aladini hakuweza chochote. Mama yake alimtaka aladini aanze biashara kwa baba yake amewacha pesa nyigi. Aladini hakuna aliwezalo. Hatimaye mwezi ukaisha na aladini akasahau yote yaliyomkuta. Aladini hakuwacha mambo yake. Mama alifungua kaduka kadogo pale nyumbani. Kaduuka ka kuuza nguo. Mama alijitahidi kumnyoosha Aladini bila mafanikio. Hata akawaza bora angekuwepo ndugu wa Mustapha huenda Aladini angenyooka kwa kusemwa na mwanaume.

Siku moja Aladini akiwa katika pirika zake alikutana na mzee mmoja wa kiafrika. Mzee mrefu na mweui sana. Alikuwa na ndevu nyeupe sna zilizokuwa ndefu. Kijana alimuita Aladinina kumuuliza hivi ni kweli wewe ni mtoto wa Mustapha? Aladini akajibu “naam ni mimi” yule mzee akamkumbatia Aladini na kumbusu kwenye paji la uso. “mimi ni baba yako mdogo, nilipotea baada ya kuvamiwa nikiwa njiani kibiashara” Aladini hakuamini maana sikuzote alitambuwa kuwa baba yake mdogo amefariki. Mzee akamwambia aladini “nenda nyumbani mwambie mama nitakuja jioni” mzee akampatia Aladini pesa kiasi kidogo.

Aladini alikwenda mbia hadi kwa mama yake na kweda kutoa habari. Mama naye hakuamini kuwa mkombozi amekuja. Atakayenyoosha tabia ya aladini sasa kaja. Ijapokuwa hivyo lakini mama alikuwa na mashaka sana. Inakuwaje mtu tuliyejuwa amefariki yapata hata miaka 30 iliyopita na sasa amekuja. Ila jambo hili halikuchukuwa nafasi kwa mama huyu, kwa alikuwa na furaha kwa kupatikana mlezi wa Aladini. Mama aliandaa chakula kiuri na nyama kwa ajili ya mgeni. Vinywaji safi viliandaliwa.

Mgeni akawasili mida ya jioni, mama alifurahi sana baada ya kumtambuwa shemeji yake wa pekee. Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa. Baada ya chakula na mazungumzo ya hapa na pele mzee akamuuliza Aladini kuwa anajishughulisha na kitu gani. Aladini hakujibu kitu. Hapo mama akafunguka kuhusu utukutu na tabia ya Aladini. Ukweli ni kuwa mzee alitambuwa kila kitu kuhusu Aladini, na ukweli ni kuwa huyu si baba yake na aladini. Ila ni kuwa mzee ana kamchezo anataka akafanye katika familia hii ya mzee Mustapha. Mzee akamueleza Aladini kuwa atamfungulia duka kubwa na zuri katikati ya mji. Hatimaye usuku ukazidi na mzee akalala, na Aldini pia.

Asubuhi na mapema Mzee alipopata kifungua kinywa alimchukuwa Aladini kuelekea mtaani. Mzee alimnunulia Aladini nguo nzuri na za kisasa. Kisha akaanza kumuonesha maeneo yaliyo mazuri kwa kuanzisha biashara ya duka. Aladini alionekana kuvutiwa sana na mawazo ya baba yake mdogo. Aadini alijiulizwa kwa nini baba asingekuwa na mawazo kama ya huyu. Hapa aladini akapata jibu ni kwa sababu baba huyu ni mgfanyabiashara toka zamani. Aladini na baba yake walirejea nyumbani wakati wa usiku. Mama alifurahi sana kumuona mwanae yupo kwenye mavazi mazeuri ya kupendeza. Mama pia alifurahi kwa mawazo mapya ya kibiashra aliyopata mwanae.

Asubuhi mzeee na Aladini walipopata kifungua kinywa walitoka tena. Walianzi mitaani na kuangalia biashara za mtaani na uanza kufikiria ni biashra gani watauza. Kisha waenelea lutebea ne ya nji. Baba huyu alikuwa na maneno matamu sana. Niani alimsimulia Aladini hadithi nzuri sana na za kupendenza. (utakuja zipata hadithi hizi baada ya hadithi ya Aladini, ili tusirefushe kisa hiki). walikwenda nje ya mji hadi wakafika sehemu moja ya mapango. Aladini alikuwa ameshoka na alimtaka baba yeke warudi. Lakini kila anapotaka kusema huwa anasimuliwa hadith nzuri na kusahau.

Basi walipofika eneo hili mzee akamueleza Aladini kuwa hapa ndio mwish wetu hatutaendelea tena. Mzee akamuagiza aladini alete vikuni ili wawashe moto wachome viazi wapate kula. Aladini akaleta kuni na mzee aliwasha moto kwa kutumia poda flani aliyounyunyiza kwenye kuni baada ya kuzungumza maneno yasiyofahamika.
Aladini alishangaa na kuogopa. Mzee akamsihi Aladini asiogope kwani hayo aliyofnya ni urithi wa familia yao.

Kisha mzee akazungumza tena maneno flani na kuelekeza mkono kwenye majabali. Hapo hapo kukatokea mtetemo wa ardhi. Aladini akataka kukimbia mzee akamtandika kofi la uchogo na kumwambia “Tulia Aladini mwanangu, hupo chini kuna mali, mali hiyo hakuna yeyote anayeweza kuitoa ila wewe”. Aladini alishangaa sana na kufurahi baada ya kutajiwa mali. Mzee akanza kumpatia maelekezo Aladini namna ya kuitoa hiyo mali.

Tukutane kesho

INAENDELEA
👇👇👇👇👇

HADITHI ZA ALIF LELA U LELA

ALADINI KATIKA PANGO LA UTAJIRI

Mzee akampatia pete Aladini na akamueleza Aladini kuwa utaingia kwenye pango hili, usiguse chochote na elekea mbele zaidi. Utakutana na baraza kubwa sana, mbele yake kuna bostani la mauwa mazuri ya thamani. Katikati utakuta mshumaa. Uchukuwe kwa polepole uje nao.” kisha mzee akaendelea kuzungumza maneno na huku anazidi kukoleza moto kwa maneno yake, ardhi ikaadha utetemeka na Aladini akaanza kuingia. Mwanzoni Aladini alikuwa anaogopa lakini kadiri alivyozidi kuingia ndivyo uoga ulivyo mtoka. Kauli ya kutogusa chochote iliendelea kujirudia masikioni mwa Aladini.

Aladini aliendelea kungia katika pango lenyekiza. Baada ya kufika mbele alishangazwa sana kukuta kuna mwangaza asioujuwa nini chanzo chake. Baraza kubwa sana lililosakafiwa kwa madini ya kupendeza sana. Mchanganyika wa madini ulioonyesha sura nzuri sana. Barasa lilikuwa likiwaka kwa ubora wa mpangilio wa rangi zake. Aladini kijana mpumbavu wa mtaani leo yupo sehemu ya ajabu. Baraza liliwa zuri kwa sakafu na dari, ila hali hiyo haikumfanya Aladini asite kuendelea na safari yake.

Mbele kidogo Aladini akakuta bostani zuri sana. Bostani lwenye matnda na mauwa ya kupendeza. Aladini alishangwazwa sana kuona kuwa yale mauwa na matunda yalikuwa ni madini yanayong’aa na kuning’inia kwa mpangilio wa kupendeza. Madini ya Almasi kwenye mti wa mdizi, yamejipanga kwenye mkungu kama ni ndivi. Hali hii ilitengeneza sura ya ajabu sana na ya kupendeza. Midizi hii ya Almasi ilikuwa na rangi za kupishana zilizo nzuri. Haikuwacha kuwaka, na kuongeza mwangaza kwenye bustani hili.

Hali haikuwa kwenye midizi tu bali machungwa yalikuwa ni mawe ya dhahabu yenye kupangiliwa katika miduara yenye kumemeta na kutoa nuru ya kupendeza. Hakika Aladini alipatwa na jambo kubwa sana. Alitamani kuchuma tunda moja lamda aonje aone kama ni dhahabu kweli ana ni matunda tu. Ila kwa muonekano iliweza kuthibitisha kuwa ni dhahabu, kila tunda lilikuwa na rangi zke za kupendeza. Aladini alitamani siku moja aweze kuishi katika sehemu hii. Michungwa iliyojipanga vyema kwenue mistari ilifuatiwa na mauwa mazuri.

Mauwa haya nayo yalikuwa ni madini yenye rang tofauti tifauti za kupendeza. Aladini alishangazwa na kuona kuwa hata nyuki waliokuwa wakipepea kwenye ,auwa walikuwa ni dhahabu tupu. Aladini ilibidi aangalie vyema hapo akagunduwa kuwa mzinga wa nyuki uliopo jirani nao ni dhahabu tubu. Mwangaza mzuri ulikuwa ukiwaka katikati ya mzinga ule. Vitone vyenye rangi za kupendeza vilikuwa vikishuka kutoka kweye mzinga. Aladini masikini na njaa aliyo nayo alitamani kwenda kukinga ulimi. Ila sauti ya mzee ilijirisia “usiguse chochote”.

Hali haikuwa kwenye mauwa na nyuki pia Aladini alishuhudia kabati kubwa lililopo katikati ya bustani. Kabati ilo lilikuwa na bilauri nzuri na za kupendeza. Bilauri zenye maji yenye rangi ya fedha (silva). visahani vyenye rangi ya hudhurungi na mauwa ya kupendeza. Birika tati kubwa zenye rangi nzuri, maandishi ya kiarabu yaliyopangiliwa vyema yaliandikwa kwenye mabirika hayo. Aladini alishikwa na butwaa ana asijuwe nini afanye.

Aladini aliendelea mbele kidogo akakuta kuna meza lingine kubwa. Meza hilo lilikuwa na taa ya mchumaa. Taa hiyo ilikuwa ikiwaka bila kutoa moshi. Moto wake ulikuwa na rangi zenye kupishana na za kupendeza. Aladini aligunduwa kuwa mwanga wote unaopatikana humu ndani ulitokana na kamshumaa hako. Aladini akauendea mshumaa na kuunyakuwa kwa upole sana. Alipoushika mshumaa mwangaza wote pale ndani ukazima. Na rangi nzuri na ya kupendeza aliyokuwa akiiona ikageua kuwa kiza la kutisha.

Mwangaza mdogo uliotokana na pete yake ndio uliokuwa ukimsaidia. Aldini akaanza kutoka kwa araka na kwa umakini zaidi. Alipokaribia kutoka tu yule mzee akataka Aladini ampatie ule mshumaa kwa kuurusha. Aladini alikataa kwa sababu ya kuwa mpaka atoke salama ndipo ampatie. Jambo hili lilikuwa ni kinyume na alivyotarajia huyu mzee. Ukweli ni kuwa mzee alitaka amtumie Aladini kupata mshumaa kisha amuuwe humohumo. Mzee alivyoona hapa atakosa yote akaamuwa afunge pango ili aladini afio humohumo. Mzee bila ya kuchukuwa pete yake kwa Aladini alifunga pango kwa uchawi na kutimua zake. Na kumuacha Aladini kwenye pango lenye giza, akiwa na njaa kali. Aladini aliendelea kulia, kujuta na asiwe na njia ya kutoka nje.

Itaendelea...
 
mkuu....naweza zipata? maana ni mpenz sana wa hzi stor
Nashindwa zi-upload hapa maana mafaili ni makubwa. Nenda YouTube kuna channel inaitwa Swahili fairy tales utazikuta nyingi za kutosha.Hata kuzidownload unaweza maana kuna apps nyingi za kukuwezesha kupakua video za YouTube mfano Vidmate.
 
Back
Top Bottom