Hadithi ya Shangazi yake Nancy kwenye daladala ya Tabata

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Aug 6, 2020
3,529
6,533
Ndani ya daladala ya segerea kuelekea tabata kimanga,hali ya hewa ni mvua siku ya jana ya jumamosi.

Nimekaa siti ya kulia dirishani kabisa huku naperuzi mtandao pendwa kabisa jamii forums, baada ya abiria wa awali niliyekaa nae kushuka mara pap anakaa bimkubwa mmoja pembeni yangu.

Kama unavyojua watanzania huwa hatuna vikwazo au ugumu wa kuzungumza mawili matatu hata kama hatufahamiani, huu ni upendo tuliojaliwa kama taifa.

Ikabidi sasa nilog out mtandaoni ili niwe hadhiri na bimkubwa huyu, topic ikahama na bimkubwa akafunguka machache ambayo ndio sababu ya kuandika uzi huu ambayo yatatufunza au kuambulia chochote.

Bimkubwa alikuwa ametoka mkoa wa jirani kuja dar makhususi kabisa kwa ajili ya kushiriki kupokea mahari ya Nancy, ambaye ni mtoto wa kaka yake.

Na sababu kubwa kabisa iliyo msukuma kufanya hivyo ni kutokana na upendo wa baba yake Nancy ambaye ndio kaka wa bimkubwa huyu.

Bimkubwa anasema hakika ana ndugu zake wengi hapa dar lkn ambaye anamjali sana na kumsaidia katika changamoto zake mbali mbali ni huyo baba yake Nancy.

Bimkubwa anasema kuna kipindi mwanae aliumwa hapa dar lkn baba Nancy alisimamia show nzima mpaka mgonjwa huyo kupona hali bimkubwa akiwa mkoani na mambo yalienda sawa kabisa.

Bimkubwa akaendelea kusema hata kama kaka yake huyo angekuwa hana kitanda angekuwa tayar kwenda kulala chini kwa jinsi anavyo mthamini kama ndugu yake.

Hata kama ingekuwa ni kula chakula duni kabisa kwa kaka yake huyo ambaye ndio baba yake na Nancy angekula kwa amani na furaha yote.

Hapa ndo unakuja ule msemo maarufu Heri kula mboga ya majani kwa amani na furaha kuliko kula nyama kwa kusimangwa.

Ndugu zangu hakika kuonyesha upendo kwa watu wengine na kuwahurumia pamoja na kuwasaidia katika changamoto zao, kunaleta athari kubwa sana katika Maisha yao kuliko vile tunavyofikiria, tunapanda mbegu ambayo hugeuka mti mkubwa kama mbuyu ambao hautikisiki au kutetereka iwe mvua, upepo au tetemo la ardhi utakuwa imara siku Zote.

Hule msaada na upendo pamoja na huwahurumia wengine hubaki katika nyoyo zao siku zote katika maisha yao, huenda wanaweza wasikwambie lakini tambua kwamba hakika kuwapenda watu wengine, kuwasaidia na kuwahurumia hakuendi bure bali unawaachia athari kubwa sana katika maisha yao, na hata katika vitabu vya dini tunaambiwa Mkono wenye kutoa ni bora zaidi kuliko mkono unaopokea hivyo basi hata Mungu wa mbinguni atakulipa na atakubariki pia.

Nancy kama upo humu hope zoezi la mahari lilienda poa kabisa, nawatakia ndoa njema na mwalimu mwenzako kutoka kanda ya ziwa, nimefungua code hii ili kama upo humu basi ujue hii story ni sehemu ya maisha yenu, shangazi yenu anawapenda sana familia ya baba yako coz baba yako ni mtu mwema sana.

Wadau msiache kushow love kwa mtu yoyote yule hakika athari yake ni kubwa mno na inasemwa Karma huwa inalipa huko mbele ya Safari, hata kama wema hautarudi kwako basi kuna mmoja wa wanafamilia yako atakuja siku moja kupata malipo ya wema wako.

Ni hayo tu!
 
Kutoa/kusaidia ni jambo jema sana, hakuna kitu nikifanya moyo wangu unakuwa na furaha kama nikitoa msaada wa chochote kwa sababu najua nafanya hivyo kutoka moyoni.

Sipendi kumsaidia mtu alafu kuanza kuimba mapambio kumtangaza kuwa umemsaidia kama wafanyavyo wanasiasa na baadhi ya watu.
 
Nimekaa siti ya kulia dirishani kabisa huku naperuzi mtandao pendwa kabisa jamii forums,,,baada ya abiria wa awali niliyekaa nae kushuka mara pap anakaa bimkubwa mmoja pembeni yangu.

Kama unavyojua watanzania huwa hatuna vikwazo au ugumu wa kuzungumza mawili matatu hata kama hatufahamiani,, huu ni upendo tuliojaliwa kama taifa.

Ikabidi sasa nilog out mtandaoni ili niwe hadhiri na bimkubwa huyu,,,topic ikahama na bimkubwa akafunguka machache ambayo ndio sababu ya kuandika uzi huu ambayo yatatufunza au kuambulia chochote.

Bimkubwa alikuwa ametoka mkoa wa jirani kuja dar makhususi kabisa kwa ajili ya kushiriki kupokea mahari ya Nancy, ambaye ni mtoto wa kaka yake.

Na sababu kubwa kabisa iliyo msukuma kufanya hivyo ni kutokana na upendo wa baba yake Nancy ambaye ndio kaka wa bimkubwa huyu.

Bimkubwa anasema hakika ana ndugu zake wengi hapa dar lkn ambaye anamjali sana na kumsaidia katika changamoto zake mbali mbali ni huyo baba yake Nancy.

Bimkubwa anasema kuna kipindi mwanae aliumwa hapa dar lkn baba Nancy alisimamia show nzima mpaka mgonjwa huyo kupona hali bimkubwa akiwa mkoani na mambo yalienda sawa kabisa.

Bimkubwa akaendelea kusema hata kama kaka yake huyo angekuwa hana kitanda angekuwa tayar kwenda kulala chini kwa jinsi anavyo mthamini kama ndugu yake.

Hata kama ingekuwa ni kula chakula duni kabisa kwa kaka yake huyo ambaye ndio baba yake na Nancy angekula kwa amani na furaha yote.

Hapa ndo unakuja ule msemo maarufu Heri kula mboga ya majani kwa amani na furaha kuliko kula nyama kwa kusimangwa.

Ndugu zangu hakika kuonyesha upendo kwa watu wengine na kuwahurumia pamoja na kuwasaidia katika changamoto zao, kunaleta athari kubwa sana katika Maisha yao kuliko vile tunavyofikiria, tunapanda mbegu ambayo hugeuka mti mkubwa kama mbuyu ambao hautikisiki au kutetereka iwe mvua, upepo au tetemo la ardhi utakuwa imara siku Zote.

Hule msaada na upendo pamoja na huwahurumia wengine hubaki katika nyoyo zao siku zote katika maisha yao,,,,huenda wanaweza wasikwambie lakini tambua kwamba hakika kuwapenda watu wengine, kuwasaidia na kuwahurumia hakuendi bure bali unawaachia athari kubwa sana katika maisha yao,,,na hata katika vitabu vya dini tunaambiwa Mkono wenye kutoa ni bora zaidi kuliko mkono unaopokea hivyo basi hata Mungu wa mbinguni atakulipa na atakubariki pia.

Nancy kama upo humu hope zoezi la mahari lilienda poa kabisa, nawatakia ndoa njema na mwalimu mwenzako kutoka kanda ya ziwa,,,, nimefungua code hii ili kama upo humu basi ujue hii story ni sehemu ya maisha yenu,, shangazi yenu anawapenda sana familia ya baba yako coz baba yako ni mtu mwema sana.

Wadau msiache kushow love kwa mtu yoyote yule hakika athari yake ni kubwa mno na inasemwa Karma huwa inalipa huko mbele ya Safari,,,hata kama wema hautarudi kwako basi kuna mmoja wa wanafamilia yako atakuja siku moja kupata malipo ya wema wako.

Ni hayo tu!
Mkuu Asante kwa darsa😊😊
 
Kutoa/kusaidia ni jambo jema sana, hakuna kitu nikifanya moyo wangu unakuwa na furaha kama nikitoa msaada wa chochote kwa sababu najua nafanya hivyo kutoka moyoni.

Sipendi kumsaidia mtu alafu kuanza kuimba mapambio kumtangaza kuwa umemsaidia kama wafanyavyo wanasiasa na baadhi ya watu.
Vizur sana chief,, na hakika kuna feeling fulani mtu hupata baada ya kuwasaidia wengine

Na msaada wa kutangaza hata hupati malipo kwa Mungu
 
Ndani ya daladala ya segerea kuelekea tabata kimanga,hali ya hewa ni mvua siku ya jana ya jumamosi.

Nimekaa siti ya kulia dirishani kabisa huku naperuzi mtandao pendwa kabisa jamii forums, baada ya abiria wa awali niliyekaa nae kushuka mara pap anakaa bimkubwa mmoja pembeni yangu.

Kama unavyojua watanzania huwa hatuna vikwazo au ugumu wa kuzungumza mawili matatu hata kama hatufahamiani, huu ni upendo tuliojaliwa kama taifa.

Ikabidi sasa nilog out mtandaoni ili niwe hadhiri na bimkubwa huyu, topic ikahama na bimkubwa akafunguka machache ambayo ndio sababu ya kuandika uzi huu ambayo yatatufunza au kuambulia chochote.

Bimkubwa alikuwa ametoka mkoa wa jirani kuja dar makhususi kabisa kwa ajili ya kushiriki kupokea mahari ya Nancy, ambaye ni mtoto wa kaka yake.

Na sababu kubwa kabisa iliyo msukuma kufanya hivyo ni kutokana na upendo wa baba yake Nancy ambaye ndio kaka wa bimkubwa huyu.

Bimkubwa anasema hakika ana ndugu zake wengi hapa dar lkn ambaye anamjali sana na kumsaidia katika changamoto zake mbali mbali ni huyo baba yake Nancy.

Bimkubwa anasema kuna kipindi mwanae aliumwa hapa dar lkn baba Nancy alisimamia show nzima mpaka mgonjwa huyo kupona hali bimkubwa akiwa mkoani na mambo yalienda sawa kabisa.

Bimkubwa akaendelea kusema hata kama kaka yake huyo angekuwa hana kitanda angekuwa tayar kwenda kulala chini kwa jinsi anavyo mthamini kama ndugu yake.

Hata kama ingekuwa ni kula chakula duni kabisa kwa kaka yake huyo ambaye ndio baba yake na Nancy angekula kwa amani na furaha yote.

Hapa ndo unakuja ule msemo maarufu Heri kula mboga ya majani kwa amani na furaha kuliko kula nyama kwa kusimangwa.

Ndugu zangu hakika kuonyesha upendo kwa watu wengine na kuwahurumia pamoja na kuwasaidia katika changamoto zao, kunaleta athari kubwa sana katika Maisha yao kuliko vile tunavyofikiria, tunapanda mbegu ambayo hugeuka mti mkubwa kama mbuyu ambao hautikisiki au kutetereka iwe mvua, upepo au tetemo la ardhi utakuwa imara siku Zote.

Hule msaada na upendo pamoja na huwahurumia wengine hubaki katika nyoyo zao siku zote katika maisha yao, huenda wanaweza wasikwambie lakini tambua kwamba hakika kuwapenda watu wengine, kuwasaidia na kuwahurumia hakuendi bure bali unawaachia athari kubwa sana katika maisha yao, na hata katika vitabu vya dini tunaambiwa Mkono wenye kutoa ni bora zaidi kuliko mkono unaopokea hivyo basi hata Mungu wa mbinguni atakulipa na atakubariki pia.

Nancy kama upo humu hope zoezi la mahari lilienda poa kabisa, nawatakia ndoa njema na mwalimu mwenzako kutoka kanda ya ziwa, nimefungua code hii ili kama upo humu basi ujue hii story ni sehemu ya maisha yenu, shangazi yenu anawapenda sana familia ya baba yako coz baba yako ni mtu mwema sana.

Wadau msiache kushow love kwa mtu yoyote yule hakika athari yake ni kubwa mno na inasemwa Karma huwa inalipa huko mbele ya Safari, hata kama wema hautarudi kwako basi kuna mmoja wa wanafamilia yako atakuja siku moja kupata malipo ya wema wako.

Ni hayo tu!
mzee wa namna hiyo 😃
uko salama kamanda?
 
Back
Top Bottom