Hadi sasa madiwani waliohama CHADEMA ni 60

Weka na gharama za kurudia chaguzi tuone tungejenga madarasa mangapi geita,mtera,iramba na chemba
 
Udikteta wa mbowe utaingamiza chadema.

Sasa hivi chama kimetelekeza wafuasi wako mahabusu baada ya kuwaandamanisha bila kibali,
si Dj wala nani anayeenda kuwaona huko gerezani.

Hapa unategemea wakitoka wataendelea kuipenda Chadema??
 
Udikteta wa mbowe utaingamiza chadema.

Sasa hivi chama kimetelekeza wafuasi wako mahabusu baada ya kuwaandamanisha bila kibali,
si Dj wala nani anaoenda kuwaona huko gerenizani.

Hapa unategemea wakitoka wataendelea kuipenda Chadema??
A kettle calling the pot black!!
 
WAKATI vuguvugu la madiwani kujiuzulu nyadhifa zao likiendelea kuchukua sura mpya siku hadi siku, imebainika kwamba tangu Januari mwaka juzi hadi sasa, kata 89 ziliondokewa na madiwani wake kwa sababu mbalimbali, ikiwamo vifo, kutenguliwa mahakamani na kujiuzulu.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa katika idadi hiyo, madiwani 60 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamejiuzulu nyadhifa zao na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Madiwani hao walijiuzulu na kufuata uanachama wa CCM kwa hoja kwamba wanaunga mkono utendaji kazi wa Rais Dk. John Magufuli.

Mbali na idadi hiyo, madiwani watano wa Chadema na mmoja wa CCM walitenguliwa na mahakama katika nyadhifa zao.

Katika orodha hiyo, pia kata 23 zilibaki wazi baada ya madiwani waliokuwa wakiziongoza kufariki dunia.

Ndani ya orodha ya madiwani 23 waliofariki dunia, 19 walikuwa wa CCM, wawili Chadema, mmoja ACT-Wazalendo na mmoja CUF.

Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Tume ya Uchaguzi (NEC), Clarence Nanyaro, ameliambia gazeti hili kwamba hadi Februari 17, mwaka huu, kata 82 zilishafanya uchaguzi kuziba nafasi zilizoachwa wazi.

Chanzo: Mtanzania
Watatoka lakini hawatashinda, Chadema itakuwepo tu.
 
Duuuh, Ahsante Tundu Lisu, maana Boniface alisema, wengine ni takataka Ila Lisu ndio jembe
 
Je hao sitini wametucost shillingi ngapi? Na hizo hela zimetoka wapi? Na kazi ya kutayarisha chaguzi mpya zimetucost fedha ngapi? Zimetoka wapi na kwamanufaa tu ya kumsifu mfalme?
Jamani ccm mtuhurumie mnatuumiza na kodi kwa matumizi yenu holela!!!
 
faida ya madiwani 60 kuhamia ccm ni ipi? wakati waziri mpango amekiri hali ya uchumi ni tete!
 
WAKATI vuguvugu la madiwani kujiuzulu nyadhifa zao likiendelea kuchukua sura mpya siku hadi siku, imebainika kwamba tangu Januari mwaka juzi hadi sasa, kata 89 ziliondokewa na madiwani wake kwa sababu mbalimbali, ikiwamo vifo, kutenguliwa mahakamani na kujiuzulu.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa katika idadi hiyo, madiwani 60 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamejiuzulu nyadhifa zao na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Madiwani hao walijiuzulu na kufuata uanachama wa CCM kwa hoja kwamba wanaunga mkono utendaji kazi wa Rais Dk. John Magufuli.

Mbali na idadi hiyo, madiwani watano wa Chadema na mmoja wa CCM walitenguliwa na mahakama katika nyadhifa zao.

Katika orodha hiyo, pia kata 23 zilibaki wazi baada ya madiwani waliokuwa wakiziongoza kufariki dunia.

Ndani ya orodha ya madiwani 23 waliofariki dunia, 19 walikuwa wa CCM, wawili Chadema, mmoja ACT-Wazalendo na mmoja CUF.

Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Tume ya Uchaguzi (NEC), Clarence Nanyaro, ameliambia gazeti hili kwamba hadi Februari 17, mwaka huu, kata 82 zilishafanya uchaguzi kuziba nafasi zilizoachwa wazi.

Chanzo: Mtanzania
Isee mada Kama hizi siku hapa jamvini hayafai utawafanya wenzio wapasuke mioyo. Halafu nadhani kati ya kata hizo 82 zilizofanya uchaguzi ccm wana kata 80 waliyobaki wana kata 2 halafu wanasema upinzani unakuwa
 
WAKATI vuguvugu la madiwani kujiuzulu nyadhifa zao likiendelea kuchukua sura mpya siku hadi siku, imebainika kwamba tangu Januari mwaka juzi hadi sasa, kata 89 ziliondokewa na madiwani wake kwa sababu mbalimbali, ikiwamo vifo, kutenguliwa mahakamani na kujiuzulu.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa katika idadi hiyo, madiwani 60 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamejiuzulu nyadhifa zao na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Madiwani hao walijiuzulu na kufuata uanachama wa CCM kwa hoja kwamba wanaunga mkono utendaji kazi wa Rais Dk. John Magufuli.

Mbali na idadi hiyo, madiwani watano wa Chadema na mmoja wa CCM walitenguliwa na mahakama katika nyadhifa zao.

Katika orodha hiyo, pia kata 23 zilibaki wazi baada ya madiwani waliokuwa wakiziongoza kufariki dunia.

Ndani ya orodha ya madiwani 23 waliofariki dunia, 19 walikuwa wa CCM, wawili Chadema, mmoja ACT-Wazalendo na mmoja CUF.

Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Tume ya Uchaguzi (NEC), Clarence Nanyaro, ameliambia gazeti hili kwamba hadi Februari 17, mwaka huu, kata 82 zilishafanya uchaguzi kuziba nafasi zilizoachwa wazi.

Chanzo: Mtanzania

Mimi nilidhani mpaka sasa vimejengwa viwanda vingapi kumbe madiwani

Hapo TZ kuna tatizo kubwa sana
 
Gharama za chaguzi za marudio gharama ya chini kabisa tuseme millioni 150 x 60 = bilioni 9 hasara kisa upuuzi mtupuuu
 
Viwanda zaidi ya laki 2 vimejengwa. Wananchi wana furaha kuliko wale wa Scandinavia. Mishahara imeongezeka mara dufu kuliko awamu zooote. Ajira zimemwagwa. Haki za binadamu zinazingatiwa mnoo. Vyombo vya habari vina uhuru wa kukosoa. Hakuna kikosi maalumu cha watu "wasiojulikana". Miji ni misafi mnoo especially jiji la mtoto mpendwa. Kidumu chama cha wenyewe!!!
Wonders will never end!!!
 
Nasikia wanatekwa, wanalatiwa na kurekodiwa, then wanalazimishwa kuwa kama hutajiuzulu tunaisambaza... sijui kama ni kweli... ameandika Mtatiro
 
Back
Top Bottom