Hadi sasa EX wangu ndo namba moja yangu

Yofav

JF-Expert Member
Mar 12, 2021
3,961
6,891
Habari wakuu,

Ni mwaka na ushee sasa toka niachane na huyu dada, Huyu dada tulianza mahusiano ya kawaida nikiwa bado sina uwezo wa kujitegemea hadi nikawa nao.

Yeye alinitangulia kiumri na kimaisha pia, Kwani alinizidi miaka minne na pia wakati tunaanza mahusiano mimi nilikuwa bado tegemezi ila yeye alikuwa tayari ana maisha yake (amepanga na anajimudu). Nakiri kwamba nilikuwa mdogo kwenye kila kitu kumzidi ila akili Mungu kanijaalia za kuishi mwanamke... Mzaa mzaa yule dada akaelewa mikato yangu akanipa tunda nikamega akanogewa tukaanza mahusiano rasmi.

Ni kweli nilikuwa na hamasa ya kutoka kuwa tegemezi na kuanza kujitegemea ila baada ya kuanza mahusiano na huyu dada ilifanya kuongeza nia na speed zaidi kuhusu kufanya hivyo na kweli haba na haba miezi saba baadae nilifanikiwa kuanza kujitegemea kwenye room yangu (nakiri pia licha ya ukubwa wa akili yangu na nia ila bado yule mdada alichangia hatua ile kuwa nyepesi mno).

Baada ya miezi saba tena ya kujitegemea na room yangu na mapenzi yetu yalizidi kupamba moto kwani alikuwa wakati mwingine anakuja kulala kwangu wakati mwingine naenda kwake... Ikafika mahali tukaona kama tunapoteza pesa nyingi why tusiamue kuishi pamoja tu.

Wazo hilo lilitoka kwangu (Mtoto akaafiki✅) Dah! though ilikuwa hatua ngumu kwangu for the first time kuishi na mwanamke chumba kimoja na ukizingatia umri wangu ila niliona no way kwa kuwa lengo ni kutengeneza maisha basi haipo shida, Kijana nikiwa na miaka 19 mwaka 2019 tu nikaanza mahusino serious kama mke na mume na yule dada.

Tumeishi kwa miaka 2 na miezi 10 ndo tukaja kuachana mwaka 2021 mwishoni, Kipindi chote tunaishi na huyu dada sikuwahi kumvunja moyo wake kwani nilikuwa muaminifu 100% na si kwamba sikutamani au kutamaniwa na girls wengine huko la hasha tena mwanzoni huyu dada alikosaga amani na mimi sana maana kimuonekano ni ile kana kwamba lazima tu nina madem wengi ila baadae alikuja kurelax na kuniamini baada ya kuona kwamba baada ya yeye sina muda na wengine (nadhani kosa langu lilianzia hapo) , nilitambua umuhimu wake na thamani yake kwangu na sikutaka kum-disappoint, Mara zote malumbano na ugomvi ulisababishwa na yeye mwenyewe kutokuwa muaminifu na kuonesha hali ya dharau kwangu ila nilijitahidi kuishi nae nikimvumilia na kumsamehe kwani alipotambua makosa aliomba radhi nami nilijua udogo wa makosa yake yale yasingekuwa na nguvu ya kutosha kung'oa kisiki chenye mizizi yake kwenye moyo wangu. Nilimpenda sana yule dada.

Hadi pale nilipokuja kufuma ujumbe wake na mtu alietoka kufanya nae mapenzi usiku wa kuamkia siku niliyoifuma message ile nikasema "sasa basi".

Yule dada kwangu ni mwanamke bora kwa kuwa alijua wajibu wake kwa mume, Alinifulia nguo zangu vizuri, Alinipasia na kunipelekea maji bafuni ilipobidi, Alinipikia chakula kizuri mno, Aliuguza nilipoumwa, Alinijua vyema wakati sipo sawa na alinipa sikio kutaka kujua kilichonisibu, Alijua kucheka na majirani vizuri, Alijua kuniheshimisha, n.k Kiufupi ile ilikuwa full package moja safi sana ya Mke na ndiyo maana niliweza kuvumilia mapungufu mengine yote yake kasoro tu uasherati na nilimuonya pia... Alikuja kuniachia kidonda chenye maumivu makali bila hata ya huruma yule dada, Nikamchukia na nikalia mbele yake kumuuliza why aniumiza yeye kila siku ila yeye mwenyewe aknijibu kwamba kwa kosa hilo hata yeye anaona kabisa hastahili kusamehewa, Na ubaya alijua kabisa kwamba aliekuwa amelala nae siku ile ni mtu ambae walikuwa ndo wameanza mahusiano punde na wasingeliweza kuachana, Basi nikaona sio kesi niachane nae na sio riziki.

Sipo hapa kuelezea mazuri yangu kwake maana siyajui anayajua yeye ila kikubwa sikuwahi kumvunja moyo wake, Nilimfanya ajione anapendwa kwa outing za hapa na pale mambo yalipokaa fresh swali nililomuuliza ni "Bby leo unataka kula kitu gani sema upesi kitu chochote kile" na nilijaribu kuwa mwalimu wake mzuri kumfunza mambo asiyoyajua kuhusu maisha na sisi wanaume pia ili kumuepusha na vishawishi ila mwisho alifuata akili za rafiki zake.

Kwanini nasema kwamba bado ni the best kwangu, Ni kwa sababu toka niachane nae sijawahi kuwa na mahusiano mengine hadi sasa, Mimi ni mwamba ambae kimuonekano nipo fresh mno na Dm zinajaa kwelikweli ila kila nikifikiria kuhusu kunapata mwanamke kama yule dah! Naona sio kazi ndogo wakuu wadada wanajigonga ni wazuri mno na wengine wamemzidi kila kitu kimuonekano ila sasa issue ipo kwenye vigezo alivyokuwa navyo yule na mengi nilimfunza mimi akaa kwenye mstari kabisa na akanijua mimi ni Mwanaume wa aina gani na akaweza kuishi na mimi. Dah! yule dada hakuwa na vizinga asee, Alikuwa anajishughulisha hivyo aliijua pesa na nidhamu ya matumizi, hakuwa na makuu yule dada ndo maana akipobadilika tu ilikuwa rahisi mimi kumjua na tukaachana.

Salam zangu kwake. Bado namkumbuka sana ila masikitiko ni kwamba mimi naweza kumpata nikimtaka ila mimi ni kama samaki sirudigi nyuma na analijua hil, Najua pia ananikumbuka sana pia ila anajua na kuelewa misimamo yangu.

Namshukurugi tu kwa kuwa nami kipindi kile chote.
 
Hayo maisha mliyoishi niliwah kuyaishi na demu mmoja ingawaje nilikuwa nmemzid umri kama miaka 6

Mwanzo hakuniambia kuwa yeye ni mchepuko wa mtu,nilihamia kwake nikawa marioo demu akawa ananijari kinoma,chai tu napikiwa ile ya kishua yenye mazaga zaga kibao kumbe nikawa natumia hela za mwanaume mwenzangu,alifanya hvyo ili kumkomoa huyo bwana ake maana alikuwa ana mademu kibao na jamaa alikuwa hapendi kujificha mambo yake alikuwa anafanya wazi wazi na mke wake alikuwa hata hamfatiliii,huyo mwanamke nae alikuwa analiwa nje na wana wengine

Tatzo la huyu demu wangu alikuwa na visafari vya ghafula ghafla na alikuwa hazuiliki akitaka kuondoka lazima aondoke hapo nilianza kupata wasiwasi ila kwa vile mwanzo nilikuwa namuamin sikushituka baadae nilkuja kugundua kumbe alikuwa anaenda kwa bwana ake kugegendwa na kupewa hela ya matumiz
 
Bado ukijana, muda upo na utakuponya, maisha yataendelea na mtu utakaye endana naye. Uwe na subira. Ugumu wa mahusiano ni hamuwezi kuendana kwa asilimia 100. Ila uamuzi uliochukua ni sahihi, hata biblia inasema sababu zote zinavumilika, ila uasherati, ni halali kuvunjisha ndoa.
 
Me sijawahi kuwa marioo mkuu.
 
Bado ukijana, muda upo na utakuponya, maisha yataendelea na mtu utakaye endana naye. Uwe na subira. Ugumu wa mahusiano ni hamuwezi kuendana kwa asilimia 100. Ila uamuzi uliochukua ni sahihi, hata biblia inasema sababu zote zinavumilika, ila uasherati, ni halali kuvunjisha ndoa.
Nakubali mkuu✊
 
Habari wakuu,

Ni mwaka na ushee sasa toka niachane na huyu dada, Huyu dada tulianza mahusiano ya kawaida nikiwa bado sina uwezo wa kujitegemea hadi nikawa nao.

Yeye alinitangulia kiumri na kimaisha pia, Kwani alinizidi miaka minne na pia wakati tunaanza mahusiano mimi nilikuwa bado tegemezi ila yeye alikuwa tayari ana maisha yake (amepanga na anajimudu). Nakiri kwamba nilikuwa mdogo kwenye kila kitu kumzidi ila akili Mungu kanijaalia za kuishi mwanamke... Mzaa mzaa yule dada akaelewa mikato yangu akanipa tunda nikamega akanogewa tukaanza mahusiano rasmi.

Ni kweli nilikuwa na hamasa ya kutoka kuwa tegemezi na kuanza kujitegemea ila baada ya kuanza mahusiano na huyu dada ilifanya kuongeza nia na speed zaidi kuhusu kufanya hivyo na kweli haba na haba miezi saba baadae nilifanikiwa kuanza kujitegemea kwenye room yangu (nakiri pia licha ya ukubwa wa akili yangu na nia ila bado yule mdada alichangia hatua ile kuwa nyepesi mno).

Baada ya miezi saba tena ya kujitegemea na room yangu na mapenzi yetu yalizidi kupamba moto kwani alikuwa wakati mwingine anakuja kulala kwangu wakati mwingine naenda kwake... Ikafika mahali tukaona kama tunapoteza pesa nyingi why tusiamue kuishi pamoja tu.

Wazo hilo lilitoka kwangu (Mtoto akaafiki) Dah! though ilikuwa hatua ngumu kwangu for the first time kuishi na mwanamke chumba kimoja na ukizingatia umri wangu ila niliona no way kwa kuwa lengo ni kutengeneza maisha basi haipo shida, Kijana nikiwa na miaka 19 mwaka 2019 tu nikaanza mahusino serious kama mke na mume na yule dada.

Tumeishi kwa miaka 2 na miezi 10 ndo tukaja kuachana mwaka 2021 mwishoni, Kipindi chote tunaishi na huyu dada sikuwahi kumvunja moyo wake kwani nilikuwa muaminifu 100% na si kwamba sikutamani au kutamaniwa na girls wengine huko la hasha tena mwanzoni huyu dada alikosaga amani na mimi sana maana kimuonekano ni ile kana kwamba lazima tu nina madem wengi ila baadae alikuja kurelax na kuniamini baada ya kuona kwamba baada ya yeye sina muda na wengine (nadhani kosa langu lilianzia hapo) , nilitambua umuhimu wake na thamani yake kwangu na sikutaka kum-disappoint, Mara zote malumbano na ugomvi ulisababishwa na yeye mwenyewe kutokuwa muaminifu na kuonesha hali ya dharau kwangu ila nilijitahidi kuishi nae nikimvumilia na kumsamehe kwani alipotambua makosa aliomba radhi nami nilijua udogo wa makosa yake yale yasingekuwa na nguvu ya kutosha kung'oa kisiki chenye mizizi yake kwenye moyo wangu. Nilimpenda sana yule dada.

Hadi pale nilipokuja kufuma ujumbe wake na mtu alietoka kufanya nae mapenzi usiku wa kuamkia siku niliyoifuma message ile nikasema "sasa basi".

Yule dada kwangu ni mwanamke bora kwa kuwa alijua wajibu wake kwa mume, Alinifulia nguo zangu vizuri, Alinipasia na kunipelekea maji bafuni ilipobidi, Alinipikia chakula kizuri mno, Aliuguza nilipoumwa, Alinijua vyema wakati sipo sawa na alinipa sikio kutaka kujua kilichonisibu, Alijua kucheka na majirani vizuri, Alijua kuniheshimisha, n.k Kiufupi ile ilikuwa full package moja safi sana ya Mke na ndiyo maana niliweza kuvumilia mapungufu mengine yote yake kasoro tu uasherati na nilimuonya pia... Alikuja kuniachia kidonda chenye maumivu makali bila hata ya huruma yule dada, Nikamchukia na nikalia mbele yake kumuuliza why aniumiza yeye kila siku ila yeye mwenyewe aknijibu kwamba kwa kosa hilo hata yeye anaona kabisa hastahili kusamehewa, Na ubaya alijua kabisa kwamba aliekuwa amelala nae siku ile ni mtu ambae walikuwa ndo wameanza mahusiano punde na wasingeliweza kuachana, Basi nikaona sio kesi niachane nae na sio riziki.

Sipo hapa kuelezea mazuri yangu kwake maana siyajui anayajua yeye ila kikubwa sikuwahi kumvunja moyo wake, Nilimfanya ajione anapendwa kwa outing za hapa na pale mambo yalipokaa fresh swali nililomuuliza ni "Bby leo unataka kula kitu gani sema upesi kitu chochote kile" na nilijaribu kuwa mwalimu wake mzuri kumfunza mambo asiyoyajua kuhusu maisha na sisi wanaume pia ili kumuepusha na vishawishi ila mwisho alifuata akili za rafiki zake.

Kwanini nasema kwamba bado ni the best kwangu, Ni kwa sababu toka niachane nae sijawahi kuwa na mahusiano mengine hadi sasa, Mimi ni mwamba ambae kimuonekano nipo fresh mno na Dm zinajaa kwelikweli ila kila nikifikiria kuhusu kunapata mwanamke kama yule dah! Naona sio kazi ndogo wakuu wadada wanajigonga ni wazuri mno na wengine wamemzidi kila kitu kimuonekano ila sasa issue ipo kwenye vigezo alivyokuwa navyo yule na mengi nilimfunza mimi akaa kwenye mstari kabisa na akanijua mimi ni Mwanaume wa aina gani na akaweza kuishi na mimi. Dah! yule dada hakuwa na vizinga asee, Alikuwa anajishughulisha hivyo aliijua pesa na nidhamu ya matumizi, hakuwa na makuu yule dada ndo maana akipobadilika tu ilikuwa rahisi mimi kumjua na tukaachana.

Salam zangu kwake. Bado namkumbuka sana ila masikitiko ni kwamba mimi naweza kumpata nikimtaka ila mimi ni kama samaki sirudigi nyuma na analijua hil, Najua pia ananikumbuka sana pia ila anajua na kuelewa misimamo yangu.

Namshukurugi tu kwa kuwa nami kipindi kile chote.
ulikosea kumuacha ulitakiwa kumsamehe

Sent from my CPH2371 using JamiiForums mobile app
 
Nenda kamuoe, wanawake Huwa hatujiamini Kwa wanaume tunaowazidi umri, Huwa tunaona tunapoteza muda.....huyo alikuwa anatafuta security na ikibidi ndoa. Kama unampenda nenda kajitambulishe umuoe....
kingine kuwa mwanaume kamili, sio unamuogopa kisa kakuzidi umri, siku Moja Moja unafoka mwanaume, na akikukalia vizuri unamzabua vibao....sio dada Yako huyo🤣

Kama hapo unasimulia kabisa eti umefumania msg halafu unalia wewe, Khhhaaaaa.....alitakiwa Alie yeye Kwa kichapo ulichomshushia, Kwa hili nashauri uwaombe radhi wanaume wenzako mara Moja.....sijapentaaaaa
 
Mkuu wewe ni mdhaifu , nasema wewe ni mdhaifu kwasababu bado unamuwazia sana huyo mwanamke

Na unamuweka kwenye sifa bora yaani mtu kakusaliti hadi kufanya mapenz na njemba nyengine ndo unamuweka namba moja??

Huyo hakukupenda kabisa , girl akikupenda ningumu sna kukicheat kiasi hicho

Anyway alikuona wewe dhaifu sana

Na kwa namna hio yakumsifia sifia hutakaa umsahau

Tafuta sabbu moja mbaya sna kwake yakumdharau na kumtoa kabisa moyoni

Life goes on brother

Nilishapia hayo yote uliopitia ila now nimesahau kabisa about that bitch
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom