Hadhari: Kuna maji feki ya kunywa kwenye mzunguko!

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,621
2,567
Ndugu wanaJF, kwenye kipindi cha Usiku wa Habari kinachorushwa na TBC1 kuanzia saa 5 usiku, kuna mfanyabishara mmoja Kariakoo (leo Julai 4) alikuwa akidai amenunua maji feki (yanayo fanana na yale ya kiwandani na yanatumia nembo ya Maji ya Uhai) na wateja waliyoyatumia walilalamika kuwa siyo salama (walianza kuumwa matumbo baada ya kuyatumia) na walipofuatilia waligundua kuwa ni maji yaliyochakachuliwa na matapeli ya mjini.Jamani haya matapeli yatatumaliza kwa sababu ya kuabudu mali na kutaka utajiri wa harakaharaka! Kuna matapeli nayouza dawa feki na vyakula feki (ikiwa ni pamoja na mayai feki, maziwa feki, mafuta ya kupikia feki). Kuna tuhuma pia kuwa matapeli mengine yanawawapa kuku wa kienyeji na wa kigeni madawa wanayotumia watu wanaoishi na virusi vya ukimwi ili wanenepe au madawa mengine ambayo hayastahili kuwapa kuku au mifugo tunayotumia kama kitoweo.Huku kupenda hela kupita kiasi kumetoka wapi?
 
Mbona kila kitu ni feki, hata wanasiasa na serikali ni feku tu? Msijali, kunyweni tu!
 
Vyakula Fake,
Maji Fake,
Ajira Fake,
Mishahara Fake,
Matumizi Fake,
Nchi Fake,
Rais Fake,
Wabunge Fake,
Serikali Fake,
Raia Fake,
UWT Fake,
Utendaji Fake,
Polisi Fake,

Hata hapa napost hii comment kwa kutumia ID fake!!!!
 
Vyakula Fake,
Maji Fake,
Ajira Fake,
Mishahara Fake,
Matumizi Fake,
Nchi Fake,
Rais Fake,
Wabunge Fake,
Serikali Fake,
Raia Fake,
UWT Fake,
Utendaji Fake,
Polisi Fake,

Hata hapa napost hii comment kwa kutumia ID fake!!!!

Hapo nyekundu umeniacha hoi.
Kila neno lisilo maana watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu yake siku ya hukumu.
 
Tofauti yake ni nini?

Mfanyabishara mwathirika na maji haya feki kwa vile amenunua mengi ni kwamba hao matapeli wana'seal' maji yao karibu sawa na yale genuine ila ukiyachunguza kwa chini utakuta ni kama wanatumia utaalamu fulani kujaza kwenye plastic containers, ambazo ama wame'recycle' au wamezichakachua ili zifanane na zile genuine.
 
Back
Top Bottom