Habari za afya ya Dr. Harrison Mwakyembe


Ndugu yangu, muamini Mungu lakini funga na funguo milango ya gari lako, usije ukaenda bongo kichwa kichwa!

Naanza kuogopa sasa bongo tukiendelea na mafisadi Bongo inaweza kuogopesha kuliko hata South africa. Hapa inaonekana Bongo Mtu anakumaliza huku anacheka.
 
Mkuu tema mate chini bro, hivi umesikia yaliyomjiri Ditopile? I mean unapoona viongozi wote wakubwa wa taifa hawataki kualikwa kwenye dinner isiyokuwa na buffet, yaani ya kila atakayehudhuria aonekane anachota mwenyewe chakula chake mbele ya hadhara,

Halafu watangulie watu wengi kabla kiongozi hajaingia kwenye line naye kuchota tena pale pale walipochota wananchi wengine, mkuu ujue kuna jambo, sisemi ndiyo yaliyomkuta Mwakyembe, lakini wallahi hapa kuna kuna maneno! Haya ndio masharti mapya ambayo viongozi wote wa juu hudai ili wahudhurie tafrija yoyote ya chakula siku hizi!

Ndugu yangu, muamini Mungu lakini funga na funguo milango ya gari lako, usije ukaenda bongo kichwa kichwa!

kwi! kwi! kwi! Haa!! hee!!
 
Mwakyembe kaumwa kama wanavyoumwa watu wengine atapona/atakufa kama wengine hakuna cha Chenge wala nini...
 
Uwoga niliousema ni kwamba kuna watu wanaamini Mafisadi wana nguvu sana, wanaogopa mafisadi mno. Mafisadi hawana kitu wala hawawezi kumwua Dr.

This is the worse thing a human being can do...
...kwamba kuna watu wanaamini Mafisadi wana nguvu sana, wanaogopa mafisadi mno...

Huu ujinga wa kutokujua kiundani maana ya woga kutaimaliza jamii.

Mbwa akipiga mkwara wa nguvu mbele ya kundi la watu. Yule atakayezalisha na kusambaza woga mkubwa kuliko wenzake..ndiye atamvuta mbwa na mbwa atamdhuru muhusika. Woga ni sumaku ya kibaologia..

Bila woga toka kwa victim mbwa hawi mbwa... Hana uwezo binafsi wa kujikamilisha kuwa mla nyama za watu!

Hii ni kweli kwa wanyama wote wala nyama. Chui anaweza kutengenezwa ..kuwa kipaka tu!

Negative emotion ndio KIWEZESHAJI. Hiyo ndio siri iliyokuwa imefichika.

Bila woga mbwa hawi na sifa zake zote.

Nini maana yake.

Mafisadi ni MBWA TU!

Kwani hawajui hii siri. Kwani si tunawafuga kwa woga wetu. Kama simba wanvyofugwa kwa "woga wa Swala" pale serengeti!

ONDOA WOGA MBELE YA FISADI....na ana-paralyse with actionless movement...They become xtrimely cowered. They simply die.

Ndio maana Mafisadi..
Mafisadi hawana kitu wala hawawezi kumwua Dr.
..na wanajua hivyo.

They have no power on their own..except what we give them..but their secret has been set open....Watalia machozi mazito ya kifo kichungu.

Na wajue kuwa tunamalizia kujipanga..tutajimwaga mtaani tutaiweka hii siri hadharani kwa kila mtanzania..yaani {UKAME WA WOGA NDIO SILAHA..WALA SI KUWA SILAHA NI MABOMU} kuwa sio muda wa mtanzania yeyote kupigwa mkwara na mbwa ..kwani Mbwa unaweza kumuua kwa kumtizama machoni kwa ujasiri na kumuacha apige kelele zake na kwa makusudi hakuna kumzalishia woga....akiendela kubweka wewe husogei..mpaka afe....au aweke mkia katikati ya muguu na kurudi kule alikotoka. Huo ndio ujumbe sahihi wa kitaalam kwa mafisadi.

Mafisadi ni "mbwa watu" to terminate them is even easier..ujingawao they wont beliave what Im say here is technical na hapo ndipo watakufa kwa kihoro cha shock siku wakiona ..Mtanzania wa kweli akijitokeza...Hana woga na hisia hasi nyingine za chuki,hasira,wasiwasi ..nk kama ilivyo kwenye nembo ya mwenge wa uhuru ..uliopepea kileleni kilimanjaro...na kuwa kwenye nembo ya serekali. Ni nembo ya kweli ya Mtanzania asiye ujua WOGA.

UTANZANIA SIO KUPIGWA MKWARA NA MBWA_FISADI!!

This is coming to pass very soon...! Huu ni ujumbe kwenye nembo ya serekali ya Tanzania. I am just elaborating. Na wafuateni wataalam wote wa mambo hayathey will give you the beuty of tha symbol..Wataka Watnzania warudie JADI YAO.

Woga sio UTU

Wasiwasi sio UTU

Mashaka sio UTU

Negative emotions sio UTU.

Lakini UTANZANIA NI UTU

Kumbwaga Fisadi is our forgoten Nature! We just have to re_activate it. And soon this is manifesting!

Ole wenu nyie mafisadi mnaoanza kujipanga kwa makundi uchwara huko mliko.

Thechnology is far..far than yur stupidity... 'will nock you down very easly.. AND I mean it...WOGA NITOE WAPI sina!!!!MIMI Mtanzania Woga nitoe wapi?
We will bring you down kwa movement kma ile iliyopandisha mwenge wa wa uhuru kilimanajaro but this time we will use IT. The symbols, the songs , the spirit will be the same...but differenttechnology... Tunaapa..hatuna uwoga..kwani hiyo ndio asili yetu. Na FISADI atachanganyikiwa.

Ujinga wenu you r just like a dog..Bila woga hamli...You freez still.

kwanini simba na nguvu zote ..amshitue swala ndio amle?

Swala angekuwa na Busara angembania tu simba ..asiogope..wasishituke..simba angeaibika. No Lunch..No Dinner...No Breakfast! They simply perish. Na hiyo ndio the only way to fix FISADI au Hata FISI.

Lakini swala hawana Utanzania. But we are..full of it! Vibaya zaidi we know how to activate it for the mass support! Si alama na nyimbo zipo? wazifute kama wanajeuri.Waanze kuvuja minara ya mwenge wa uhuru iliyotapakaa nchi nzima. Wangofoe alama za mwenge kwenye uniform za kila mwanjeshi wa nchi hii, wabadili nembo ya serekali ya Taifa...No They cant, that means they have already lost..Ujumbe ndio huo! Huo ndio utanzania..Ni kuuufufua tu!

UTANZANIA NI UTU!! Na kwnye UTU hakuana woga, wala hisia hasi zozote.

Mungu Ibariki tz.
 
Na kwa taarifa yao baada ya kusikia uzushi wao ameamua akatize dozi ya kupumzika kwa kulamba ulabu na sasa anamalizia ya tatu
 
Haya jamani hayawi hayawi yamekua ndio maana naipenda jf,hatimaye spika amekiri........................mafisadi mwaka huu mbaya kwenu
Mbunge 'amwekea' uchawi Mwakyembe

*Kamera bungeni zamnasa 'akimwangia' kitini
*Spika, Naibu na wajumbe wa kamati nao wamo
*Mwakyembe azushiwa kifo, arejea Dar kuchunguzwa


Na Mwandishi Wetu, Dodoma

SIKU moja baada ya Mbunge wa Kyela, Dkt. Harrison Mwakyembe, kuugua ghafla bungeni sasa imethibitika kwamba suala hilo lina uhusiano wa moja kwa moja na watuhumiwa wa ufisadi na tayari vyombo vya usalama vimeanza kulifanyia kazi.

Kuhusishwa moja kwa moja kwa watuhumiwa hao wa ufisadi na kuugua kwa Dkt. Mwakyembe, unatokana na mmoja wao kunaswa na kamera za chombo kimoja cha habari (jina tunalo) zilizoko bungeni.

Inadaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alinaswa na kamera hizo akifuatana na Ofisa wa Bunge na kuweka vitu vinavyoaminika kuwa ni dawa za kienyeji katika kiti cha Mbunge huyo cha Spika wa Bunge Bw. Samwel Sitta, Naibu wake Bibi Anne Makinda, aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Kuchunguza tuhuma za Richmond Bibi Stela Manyanya, Mbunge wa Same Bibi Anne Kilango na wabunge wengine.

"Unajua hatukuamini macho yetu, tulishangaa sana kumwona Mheshimiwa huyo akiwa na mmoja wa maofisa wa Bunge wakiingia na kuweka vitu fulani kwenye kiti cha Dkt. Mwakyembe, Spika, Stela Manyanya, Naibu Spika, Anne Kilango-Malecela na baadaye kwenye viti vya baadhi ya wabunge.

"Wakati huo kamera ya chombo husika ilikuwa 'on' kwa majaribio, kamera za Bunge zilikuwa zimezimwa, kwa kuwa muda ulikuwa bado kidogo, hawa ni wajanja sana, waliingia muda mfupi tu baada ya watu wa usalama kumaliza kukagua ukumbi," kilisema chanzo chetu ndani ya Ofisi ya Bunge.

Kilisema kitendo hicho kilimpa hofu kubwa pamoja na mwenzake waliyekuwa naye, hivyo kuamua kutoa taarifa hiyo kwa Spika.

Akizungumza na Majira jana, Bw. Sitta alikiri kutokea kwa tukio hilo na kueleza kwamba amesikitishwa na kitendo hicho, ambacho hakutarajia katika maisha yake kama kinaweza kufanywa na mtu mwenye akili na kiongozi aliyechaguliwa na wananchi.

"Kwa kweli taarifa hizo zipo na zimezagaa hapa mjini, mimi mwenyewe nimesikitishwa sana na tayari vyombo vya usalama vimeanza kufanya uchunguzi juu ya suala hili. Hatuwezi kuacha hivihivi katika mazingira kama haya...ni matukio ya kijingajinga tu hivi, ila hatuwezi kuyaacha hivihivi," alisema Bw. Sitta.

Alisema hatua zitakapochukuliwa dhidi ya watuhumiwa hao itajulikana baada ya uchunguzi wa kiusalama kukamilika na kwamba tayari Ofisa wa Bunge ameshahojiwa juu ya tukio hilo.

Kwa kawaida maofisa wa usalama hupita mapema ndani ya ukumbi wa Bunge kukagua kila eneo wakiwa na vitendea kazi kadhaa za kubaini kitu chochote kabla ya saa 2 asubuhi.

Dkt. Mwakyembe alirejea mjini Dar es Salaam jana kwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa afya yake. Hata hivyo jana ulizushwa uvumi kuwa Mbunge huyo amepoteza maisha, ambapo chumba cha habari cha gazeti hili kilipokea simu kadhaa zikiulizia hali hiyo.

Haya kada mpinzani unalolote hapa?
 
JF is the first.. others will follow.. ni vizuri kutupa JF benefit of the doubt jamani.. we in too deep!
 
JF is the first.. others will follow.. ni vizuri kutupa JF benefit of the doubt jamani.. we in too deep!

Unajua majuzi nilikuwa naongea na mkulu mmoja ambaye ni wa ndani kabisa huku Ikulu, alikuwa hajui kuwa mimi ni member hapa, akaniambia "...hawa vijana wa Jambo Forums hawa unajua ni hatari sana hawa huwa wanakuwa na very serious information za serikali hivi wanazipataje ....", nikamwamba mzee yaaani hata sielewi,

sasa mkulu akaniuwa na sentesi yake ya pili akasema "....hivi ni kwa nini hawatumii majina yao kamili ya ukweli it will make sense sana....maana hii mambo ya Mzee wa Kijiji, .......sijui Kana ka-nsungu, mwingine eti ni Field Marshall" nikamwambia cynically kuwa mzee wako watu kama Mnyika, Freeman, Zitto, na Kitila ambao wanatumia majina yao ya kweli, mkulu akashitukia ".....vipi na wewe umo huko nini unaonekana kuelewa sana....." nikamwambia hapana mzee mimi kama wewe tu huwa sometimes nachungulia chngulia tu huko,

My point ni kwamba nimesema mara nyingi san kuwa tumefikia mahali sasa inatisha, unajua baada ya ile kasheshe ya kufungiwa hapa JF, Mkulu wangu Mtanzania, aliwahi kusema kuwa "....sasa taifa wametupa too much of responsibility I hope tutaweza kui-full fill..." ninasema kuwa we are almost there kama sio tayari!

JF mbele alyways, one step ahead!
 
Siku hizi hoja zote nzito zinaanzia hapa JF kisha magazeti yanafuata....hapa kuna vunjwa wanapembua news na wana update news kila second....
 
Unajua majuzi nilikuwa naongea na mkulu mmoja "...hawa vijana wa Jambo Forums hawa unajua ni hatari sana hawa huwa wanakuwa na very serious information za serikali hivi wanazipataje ....", nikamwamba mzee yaaani hata sielewi...

Nilisha sema ..hawa vibosile/mafisadi kuna program wamezibeba akilini..lakini sio_activated...

kinachotakiwa ni password tu! Tuki_activate..wamekwisha....Huoni kama huyo ...kukiri kwa moyo na mdomo wake kuwa ....ni hatari sana ..hawa vijana ....Ni dalili nzuri..TUNAWAFIKIA. Kinachotakiwa Ni idadi iongezeke.

Inatakiwa kuwazonga na kuwa Prssure...sensible na viable...wata_Click tu!

hakuna kutumia silaha za kizamani. Maandamano na marungu yamepitwa na wakati.

Nafikiri sikueleweka.
 
Nilipata nafasi nyembamba sana ya kuongea na Mheshimiwa Mwakyembe personally kwenye simu baada ya mtu niliyekuwa nimempigia kuipokea akiwa kwa Mwakyembe alikokuwa amekwenda kumjulia hali. Dr Mwakyembe anaelekea ana matatizo ya kawaida yatokanayo na kufanya kazi zinazotumia nishati nyingi ya mwili bila kupata mapumziko ya kutosha; yeye mwenyewe hana wasiwasi kabisa na afya yake na wala hahusishi tatizo lake la sasa na uchawi wowote ule au ufisadi. Vile vile hana historia ya medical conditions zozote zile za kutisha zinazohitaji uangalizi wa karibu kutoka kwa madakitari, kwa hiyo anachohitaji ni mapumziko tu. Kitu ambacho sikuelewa mara moja ni kwa nini apate uchovu wa aina hiyo; huenda amekuwa anafikiria jambo fulani kwa nguvu sana tangu apate celebrity status kutokana na vita dhidi ya mafisadi.
 
Na hiyo kamera ya ukumbini mwa bunge kumnasa afisa mmoja aliyeweka midawa ya kichawi ktk kiti chake bungeni kulikoni?
 
Augustoons said:
Haya jamani hayawi hayawi yamekua ndio maana naipenda jf,hatimaye spika amekiri........................mafisadi mwaka huu mbaya kwenu
Mbunge 'amwekea' uchawi Mwakyembe
Kamera bungeni zamnasa 'akimwangia' kitini
*Spika, Naibu na wajumbe wa kamati nao wamo
*Mwakyembe azushiwa kifo, arejea Dar kuchunguzwa

“Unajua hatukuamini macho yetu, tulishangaa sana kumwona Mheshimiwa huyo akiwa na mmoja wa maofisa wa Bunge wakiingia na kuweka vitu fulani kwenye kiti cha Dkt. Mwakyembe, Spika, Stela Manyanya, Naibu Spika, Anne Kilango-Malecela na baadaye kwenye viti vya baadhi ya wabunge.

Kilisema kitendo hicho kilimpa hofu kubwa pamoja na mwenzake waliyekuwa naye, hivyo kuamua kutoa taarifa hiyo kwa Spika.

“Kwa kweli taarifa hizo zipo na zimezagaa hapa mjini, mimi mwenyewe nimesikitishwa sana na tayari vyombo vya usalama vimeanza kufanya uchunguzi juu ya suala hili. Hatuwezi kuacha hivihivi katika mazingira kama haya...ni matukio ya kijingajinga tu hivi, ila hatuwezi kuyaacha hivihivi,” alisema Bw. Sitta.
QUOTE]

Hii ni aibu kwa taifa kama la Tanzania.

Take this event and extrapolate it...NA: Unapata kiini cha kwanini Albino wanauliwa, kwanini kijana kama yule aliyeshikwa muhimbili anakula kichwa cha mtu anakuwepo, unapata kwanini watu wanachunwa ngozi, unakuta kwanini kuna biashara ya vioungo vya vya binaadamu. VINAANZIA BUNGENI BILA MSWAADA KUPITISWHA RASMI. Au umepitishwa kichawi..who knows?

Kama viongozi wetu ndio wanafanya hivi, tena ndani ya nyumba ya bunge, Kwanini wananchi wasifuate nyayo? Tena kwa kishindo?

Tunataka baada ya uchunguzi kufanyaika ...Huyo Mbunge Ajiuzulu mara moja. Ni mfano mbaya kwa Taifa, haijawahi kutokea. Ni kweli tupu kuwa huyo mbunge anachochea ushirikina...anaunga mkono kwa vitendo...mauaji ya vikongwe na fukuto kubwa la ushirikina linalolikumba Taifa kwa sasa.

JF lazima tushike banko na jambo hili...Mpaka tuone mwisho wake. Nchi haiwezi Kuongozwa kwa PRIMITIVE FORCES like this. Na sisi tukijivunia kuwa wananchi wake. This has to stop.

Bunge si mahali pakufanya na kuonyesha mifano mibovu kama hiyo.

BUT:

Kwa upande mwingine ni habari njema kwetu.

Tunapata mwanga na habari za kutosha kwa watu tunaopambana nao.

THEY ARE SIMPLY VERY PRIMITIVE CREATURES. Hizi sio enzi zao kabisa.

Kama silaha yao kubwa ya kuendeleza UFISADI ni kutumia Dark Forces they are done.

Somehow JF tunalazimishwa na hawa mafisadi waamini uchawi..kuanza kujadili mambo ya kutupotezea muda. But we have to..kwa maana ya kuelimishana na kuonyesha kwamba..Physics ya negative emotions its the antidote of such rabish. Simply usiupe woga, wasiwasi, mashaka and any other negative emotions... UCHAWI au tetesi kama hizo... And it will never work.

Dr Mwakyembe natumaini unapitia huku mara kwa mara vinginevyo msamaria mwema amplekee ujumbe huu muhimu. And If it works..Dr uje mwnyewe hapa na kutoashukrani kwa JF. Na kutupa moyo wa kuendela kulipelekataifa kunakotakiwa!

Wachawi and all primitive Dictators they know exactly how to use our negative emotions to empower themselves.

Muogope Mbwa ..na atakumaliza...

Muogope Dikteta au fisadi na atakufanya kitoweo...atakulipisha umeme juu, mafuta juu, kodi juu etc ...but kimya huna cha kufanya.

Na

Mugope mchawi na atakuendesha kwa ungo..kuelekea kusiko julikana.

The choise is yours!
 
Back
Top Bottom