Dr Mathew Togolani Mndeme
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 201
- 808
- Thread starter
- #161
Togolani, upo sahihi kwa kiwango kikubwa, ila napingana na wewe kwakutokuwa muwazi sana kwa kuinyooshea serikali moja kwa moja na badala yake umegusa na mtu mmoja mmoja.
Sheria zinazowekwa na serikali na bunge letu ni kandamizi sana.
Na hii inatokana na tuliowaamini kuwa wameelimika na kuishi dunia ya kwanza kielimu au ya pili, tukawapa madaraka kutuongoza(kumbe hawajaelimika)
ndiyo waliotufikisha hapa.
Wamezoea kutambika tu na siyo kuiishi elimu waliyosoma.
Tafiti zako fanyia pia wakati ujao wa uchaguzi kama utakuwepo, utaona wanavyopishana kwa waganga wa kienyeji.
Watu kama hao utegemee wataleta sheria wenzeshi kwenye tafiti za kulisaidia taaifa?
Serikali ya uingereza imetoa billions kufadhiri tafiti siyo mtu Brother.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ndugu nguruka wa kig0ma, sijailamu serikali moja kwa moja kwa kuwa hiyo haikua msingi wa hoja yangu. Hoja yangu ni kuonesha msingi wa tatizo. Siku zote naamini serikali na vyombo vingine tulivyo navyo ni reflection yetu sisi. Wanaoongoza wanatoka kwenye jamii hivyo wanayofanya, kusema, kusimamia, na kuweka kama vipaumbele kwa sehemu kubwa ni yale yaliyoko kwenye jamii. Hivyo kama tunataka kujadili tatizo kisayansi, lazima tupanue macho kutazama angles zote za tatizo badala ya kuirushia mawe serikali pekee.
Ukitaka kuelewa msingi wa hoja yangu jiulize kama shida ni serikali pekee, kwa nini wabunge nao walikubaliana na hoja za serikali? Wangetakiwa kuikataa sheria kama sio nzuri. Pili, jiulize kwa nini wabunge hawahawa wanaopitisha sheria hizihizi unazoona zina shida, wanaendelea kuchaghuliwa na wananchi kila mara?
JIBU: tatizo sio wabunge wala serikali. Wao ni matokeo tu. Tatizo ni mfumo mzima unaozalisha walio kwenye hizo nafasi tukianza na mimi na wewe. Hivyo kama tunataka mabadiliko ya kweli na endelevu, tuanzie chini na sio juu.
MM