Habar zenu wakuu

Said Cosmetics

JF-Expert Member
Sep 4, 2017
2,001
1,586
MADA YA LEO SEHEM 10 AMBAZO PESA ZIMEJIFICHA

10 hours ago


ninawafundisha somo hili ili usije ukasema mimi sijui wapi pakutafutia pesa unapokuwa unatafuta pesa lazima ujiulize unapozitafuta pesa zipo kama unapozitafuta hakuna utaishia kuchoka tu sasa leo tuangalie zilipojificha pesa halafu baada ya mada hii kila Mtu aanze kuzisaka kwa Nguvu.

1.PESA ZIMEJIFICHA KWA WATU

kama unataka leo nataka nikwambie kitu kwamba fedha ziko kwa watu sasa watu hawawezi kukupa tu pesa eti kwasababu wanakujua hapana wanataka ufanye kitu. Jiulize hao watu wanaokuzinguka wanamahitaji gani ambayo wewe unaweza kuwatimizia wakakupatia pesa chochote ambacho unaona kwamba unaweza kuasaidia watu wasaidie watakupa fedha. Kwa mfano unaweza ukawa unaweza kufundisha ufugaji bora tafuta wenye mahitaji watakulipa tu

2.PESA ZIMEJIFICHA KWENYE MATATIZO

Siku zote kama unataka kufanikiwa tafuta matatizo sehem kwenye matatizo ya watu ukiyatafutia suluhu utapata fedha. Ukitatua matatizo madogo madogo utapata fedha kidogo matatizo makubwa fedha Kubwa

Kaa chini jiulize hapo kwenye jamii yako wanamatatizo gani hapo kazini kwako wanakula wapi tatua tatizo upate pesa

3.PESA ZIMEJIFICHA KWENYE KIPAJI ULICHONACHO

DIAMOND, PLATNUM, HARUNA NYONZIMA, ALI KIBA, MBWANA SAMATA, MC PILIPILI.KANUMBA hebu jiulize yakitajwa majina hayo unapata picha gani na likitajwa jina lako unapata picha gani. Kama ukiweza kukitumia kipaji chako ulichokacho unaweza kuwa milionea kwa muda mfupi tatizo watu wengi hawajui jinsi ya kutambua vipaji vyao kama mkilitaka somo hili mtaniambia tukubaliane. Ninachotaka kukwambia nikuwa kipaji chako ndio maisha yako. Ukikuza kipaji chako unatoka kimaisha

4.PESA IMEJIFICHA KWENYE MAONO

Hii ni sehem ya nne ambayo fedha imejificha, unamaono gani hapa dunaini, ili uweze kupata fedha pia lazima uwe na maono labda ya kuanzisha kiwanda, yakuanzisha taasisi yakusaidia watu, wewe jiulize unamaono gani ambayo baadae yatakupatia pesa?

5.PESA ZIMEJIFICHA KWENYE FURSA

matatizo yoote unayiyaona Ni fursa chamsingi niwewe kukomaa Na kuyageuza kuwa fursa


6.PESA ZIMEJIFICHA KWENYE BIDHAA AU HUDMA

anzisha Biashara ya kuuza bidhaa au anzisha Huduma utapata fedha tu. Jiangalie unakitu gani ndani yajo uanze kumitoa kwa wengine

7.PESA ZIMEJIFICHA KWENYE MAWAZO

Unaweza kuwa huna pesa Lakini Kama unawazo linaweza kukuzalishia Pesa nyingi jiulize unamawazo gani ambayo yatakukelea pesaaaa

8.FEDHA IMEJIFICHA KWENYE KAZI

kama uanataka kufanikiwa fanya kazi kwa bidiii Mungu atakulipa tu Kama nimfanyakazi fanya kwa juhudi zote

9.PESA IMEJIFICHA KWENYE KUWEKEZA

WEKEZA KWENYE ARDHI MAANA INAPANDA BEI WEKEZA SEHEM MBALIMBALI ITAKAYOKUPIA FAIDA

10.SEHEM YA KUMI PESA IMEJIFICHA KWA MUNGU

Kama uanataka kufanikiwa kuwa mtoaji wa sadaka

[https://lh3]
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom