Jamaa_Mbishi
JF-Expert Member
- Jun 15, 2013
- 9,155
- 6,060
Ujinga ni kitu kimoja kibaya sana....Nakumbuka jinsi Dudus alivyokuwwa anatumia watu wake kuua watu ili amiliki biashara ya unga peke huku akisaidia hao mambumbumbu/misukule mahitaji yao. Ikumbukwe, Dudus alikuwa anasomesha watoto wa hawa misukule yake, alilipa kodi za nyumba kwa baadhi ya misukule yake ambao walikuwa hawana uwezo wowote (unemployed na illiterate), kuwapa food rations, na vinginevyo kama alivyosem mleta mada. Ile misukule ya Dudus haikujali kuwa Lord wao anaua watu kujinufaisha yeye lakini walikuwa radhi kumtetea, kisa wanasaidiwa na jangili. Tuje sasa kwa hawa Gwajima na Manji....hawa jamaa ni watuhumiwa tu japo kuna taarifa chini ya zuria kuwa Gwajima kwa muda mrefu anashughulisha na hii biashara ya uuzaji unga, I can confirm kuwa ni habari ya ukweli kwa sababu aliyesema alikuwa kwenye ule mtandao na alikuwa na wadhifa fulani. Waumi wake wengi walimtoroka baada ya kupata taarifa zake including my own brother. Kama nilivyosema kwenye ufunguzi kuwa ni ujinga, haiwezekani mtu mwenye akili timamu kumsindikiza Gwajima au Manji mahakamani ikiwa anaangamiza jamii. Hata kama anakulipia pango la nyumba au kukuchapia mkeo (kama Flora Mbasha) kusingizia anampa fadhila za kiroho, huu ni ujinga na misukule wa namna hii pia ni janga la taifa kwani wanafuga maradhi ndani ya jamii.