Gwajima Lisha kondoo NENO: Je ni wapi ktk Bibilia Mungu amehalalisha VISASI kwa Mtu kutuhumiwa?

naona unalazimisha kulink vifungu na watu mashuhuri kwenye bibilia ili kujustfy KISASI. sasa vyeti ndio vitamsafisha.
Ushauri mtumishi wa Mungu haruhusiwi kutuhumiwa popote pale hata kama ni kwa lengo la kuuisaidia polisi.
Umesahau ni watumishi wa Mungu hawahawa walifuel chuki rwanda genocide.
Umewahi kujiuliza mtumishi Athanase Seromba wa rwanda kwa nini hadi kesho anatumikia kifungo cha maisha kwenye gereza la Akpro-Missérété benin.
VISASI viko sambamba na CHUKI, Kwa watu wenye ushawishi wanatakiwa kuwa makini na kauli zao au kupindisha maandiko for personal gains and protections.
Mkuu hapa hoja ni VISASI, Leo analipa kisasi kwa huyu, Hatujui kesho ataamka kulipa kisasi kwa nani, na nini itakuwa madhara ya muda mrefu na mfupi wa VISASI vyake.
Hilo fundisho la kisasi Halikuwa sawa hata kidogo, Na kama hoja ni vyeti, alisema kuna room ya kwenda mahakamani angefuata taratibu za nchi sio kutumia kanisa.
hapo ni kupigana na adui ndugu, unapigana kiroho na kimwili. tofautisha na adui aliyekupiga halafu ametulia haendelei kukupasue, na adui ambaye amekupiga pakauma na bado anakukimbiza anataka akumalize kabisa na hana hata shida ya kuomba msamaha ili muyamalize. hapo unachofanya ni kukimbia, kujihami na kushambulia.
 
Kwanza niseme, siungi mkono cheti feki au mambo yoyote bandia maana ni kinyume na taratibu za nchi yetu tulizokubaliana ikithibitika pasipo shaka hatua kali zichukuliwe...

Ni maswali ninayojiuliza kila nikiangalia hotuba ya mtumishi Gwajima jana.
Kama Kigezo ni KUTUHUMIWA, Watumishi wa Mungu kuanzia Mwanzo hadi Ufunuo wanatuhumiwa. Yesu alituhumiwa kuwa Mlevi,ana Mapepo, Mzushi, Muongo....

Mtumishi anafundisha kisasi ni cha Mungu sio aliyetendwa baya, anaenda mbali kwa kutoa kisa cha NABOTH na Ahabu ambapo naboth alinyang'anywa shamba lakini kisasi akalipa Mungu kupitia mtu mwingine sio MTENDEWA BAYA. Hakuna popote alipotoa Mstari unaoonyesha Mungu kuhamasisha Mtendewa mabaya kulipa kisasi badala yake yesu anasema WAOMBEENI WANAOWAUDHI.

1/ Je! Mtumishi anapopindisha maandiko ili Kuhalalisha kulipa kisasi kwa kutuhumiwa (SIo Kuhukumiwa), hatuoni hapa anapaswa kurekebishwa ?

2/ Je mtu huyu akifanikiwa kuwa na Waumini zaidi ya Millioni, na akapandikiza mbegu hii ya kisasi kwamba ukipigwa moja(Tuhuma) wewe piga Visasi 10+, taifa litaishia wapi?

3/ Anatufundisha nini watanzania kwa kuhamasiha Visasi pale Tunapotuhumiwa(Tuhuma inaweza kuwa kweli au si kweli) na vyombo halali kisheria?

4/ Kama mamlaka (Zimewekwa na Mungu) zina haki ya kutuhumu yeyote, Kwa nini mtumishi usitumie jukwaa la kanisa kuwafundisha waumini ukweli huo?

5/ Je ikiwa wachungaji wote na mashehe wote wakahamasisha Visasi waumini wao kwa misingi ya kutuhumiwa huku wao wakiahidi kulipa mara 10+, Hii nchi nani atakayeishi?

Ushauri:
Badili mwenendo wa hotuba zako, Maneno yenye Sura za kisiasa Ita Press Conference kama unataka kutoa ushauri au ufafanuzi wa jambo lenye sura ya kisiasa, au kuisaidia serikali katika mapambano juu ya vyeti au vitu vyovyote visivyohalali:

Yesu kuonyesha umakini alimuuliza Petro mara tatu kama anampenda, Baada ya kuthibitisha akampa agizo LISHA KONDOO WANGU. KONDOO ALISHWI VISASI AU PERSONAL CONFLICTS BALI NENO Mtumishi. Pia wale ni wanafamilia wa Mungu, Mungu ndio baba yao wewe ni Muangalizi tu usijibinafsishie.

GWAJIMA LISHA KONDOO WA BWANA
Nyie ndio mnaosababisha Bashite anaendelea kulipuliwa na Gwajima
 
mwenye namba ya Gwajima anitumie tafadhali, nataka nimkumbushe kuwa Bashite amesharudi nchini hivyo aendeleze mashambulizi. asisahau pia kuamuru yale mapepo yamfuate pale ilala boma.
 
hahahaa unaniita brother! Umejuaje kama mi me au ke..!! Well, tatiza lako mkuu umeacha main point ya VYETI unatuletea "kisasi" hiyo kisasi unayoona wewe ni mtazamo wako tu na biaseness towards daudi. Kama unataka umsaidie mwambie aache maneno aweke vyeti, baasi. Hii bla bla nyingine ni kupoteza muda na kuzidi kumuharibia daudi.
ukimsikiliza critically na analytically mzizi wa yote ni kulipa kile alichofanyiwa(kuingizwa kwenye listi ya watuhumiwa wa biashara hiyo haramu na wengine wana taarifa muhimu zinazoweza kuwasaidia polisi kuwatia nguvuni vinara wa biashara hiyo. ) cheti ni kama kasia ya kumfikisha anapokwenda. Ndio maana cheti anatumia kama silaha.
ndio maana nimetoa maoni
1:Kama anania nzuri kuhusu cheti aite confenference au aende mahakamani kama alivyoeleza jana
2:Atumie kanisa kama sehemu ya Kuhubiri NENO sio platform ya mambo ya SIASA, Au Visasi kwa mujibu wa kauli yake.
3:Asihusianishe tuhuma na kuombwa kusaidia polisi kama anataarifa yoyote sio lazima yeye maana anawatu zaidi ya 70,000
 
naona unalazimisha kulink vifungu na watu mashuhuri kwenye bibilia ili kujustfy KISASI. sasa vyeti ndio vitamsafisha.
Ushauri mtumishi wa Mungu haruhusiwi kutuhumiwa popote pale hata kama ni kwa lengo la kuuisaidia polisi.
Umesahau ni watumishi wa Mungu hawahawa walifuel chuki rwanda genocide.
Umewahi kujiuliza mtumishi Athanase Seromba wa rwanda kwa nini hadi kesho anatumikia kifungo cha maisha kwenye gereza la Akpro-Missérété benin.
VISASI viko sambamba na CHUKI, Kwa watu wenye ushawishi wanatakiwa kuwa makini na kauli zao au kupindisha maandiko for personal gains and protections.
Mkuu hapa hoja ni VISASI, Leo analipa kisasi kwa huyu, Hatujui kesho ataamka kulipa kisasi kwa nani, na nini itakuwa madhara ya muda mrefu na mfupi wa VISASI vyake.
Hilo fundisho la kisasi Halikuwa sawa hata kidogo, Na kama hoja ni vyeti, alisema kuna room ya kwenda mahakamani angefuata taratibu za nchi sio kutumia kanisa.
Mbona sijaona ukimpinga Aliyekuwa anatuhumu watu hovyo kwenye TV?
Hukuona kama ni visasi?

Kwa sasa kindoo wanahitaji kula vyeti vya Bashite tu..
 
Gwajima ukiona anawaka ujue umemchokoza pia huwa anakutahadhalisha kabla hajakufumua
Au kwa kuwa ni kiongozi wa dini mkimfanyia ujinga awavumilie wakati hamvumiliki
 
Mbona sijaona ukimpinga Aliyekuwa anatuhumu watu hovyo kwenye TV?
Hukuona kama ni visasi?

Kwa sasa kindoo wanahitaji kula vyeti vya Bashite tu..
Mchungaji anategemewa kuonyesha high degree of morality Bila kujali uovu wa muumini au raia mwingine.
 
Hiyo ni imani, kama waumini wake wanamwamini basi wewe haikuhusu, tuliza boli, na kwa sasa ndo kanisa lake linajaa balaa, anachofanya ni sawa, na wala hujalazimishwa kufuatilia, mind your own business!
 
Nawaonea huruma hao wafuasi wake. Mchungaji mwenye roho za kulipiza kisasi namna hii sijui atasubutu vipi kunifundisha somo la msamaha, upendo na tunda la roho .

Ni roho gani inayomuongoza huyu baba? Kamwe haiwezekani akaongozwa na roho Mtakatifu na akafanya hayo anayoyafanya.
 
Mchungaji anategemewa kuonyesha high degree of morality Bila kujali uovu wa muumini au raia mwingine.
kazi ya wachungaji ni pamoja na kukemea uovu kwa nguvu zote.wizi wa vyeti ni uovu (dhambi ) kama dhambi nyingine na kila mpenzi wa MUNGU lazima aikemee na kuipinga kwa nguvu zote. safi sana mch.Gwajima,endelea kuwasaidia waovu waache maovu.
 
Unasemaje kuhusu kupindisha maandiko kuverify kisasi. Wewe unaona anasaidia jamii lakn yeye anasema analipa kisasi. Tuchukue lipi mkuu
 
yote ni sawa.kwa sasa suala muhimu uovu wa huyo mjamaa ukomeshwe.
 
Ningekuona wa maana kama ungeli mwambia Daudi Albert B. yule aliyesoma shule ya msingi Koromije, afanye bidii kuonesha vyeti vyake haraka kwani watu wanamvisia, akitia mguu tu, wanaanza kuulizia vyeti.
Muosha, huoshwa. Aliwavimbia wafanya kazi wenzake kweli kweli kuwa bila cheti ajira imeota mbawa. Hakuna uovu kama huo; Kumdai mwenzio usichokuwa nacho. Daudi ili kuonesha kuwahurumia watu angekuwa wa kwanza kupinga kuonesha vyeti. Lakini, yeye ndo wa kwanza kabisa kujigamba kumtimua yeyote atakaye gairi kuonesha cheti chake. Utadhani yeye mwenyewe anacho.
Tumuombe rais atuulize hadharani; Nimtumbue nisimtumbue Daudi wenyu?? Jibu tushaandaa tiyari; Mutumbuyeeeeeeee.
 
Huna akili kabisa, Tanzania unahitaji watu kama Gwajima angalau hata 10 tuu, utoto utoto unoendelea hapa nchini ungeisha, kwahiyo kiss yeye ni mchungaji ndio Hana haki yakuongea ukweli ambao watu wengine wameshindwa kuongea kwa uoga wao, tumepata mtu jasiri na mwenye akili timamu badala ya kujivunia wewe unaongea kama mnafiki, Gwajima katokea mbinguni wewe yule sio kama wale wala usimfananishe na wale. Swala la Bashite bado kabisa hadi tuone hatima yakudanganya umma nakuwarubuni maraisi wawili waamu mbili kuwa yeye ni Paulo wakati yeye ni daudi, hili swala sio jepesi kama akili zako zinavyokutuma. Kabla hujampuuza mtu jitasmini kwanza akili zako zinakutosha mwenyewe au zinakutosha pamoja na jamii?

Back
Top Bottom