Gundu la Addis Ababa 1989

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,264
GUNDU LA ADDIS ABABA

Nina bahati mbaya na Ethiopia.
Hili la sanamu halinishangazi

Mara ya kwanza kufika Addis Ababa ilikuwa mwaka wa 1989 mwezi December kuelekea Christmas.

Mwaliko wangu ulikuwa unatokea Nairobi nimetumiwa telex nikachukue tiketi Ethiopian Airways (EA).

Mkosi ulianza siku moja kabla ya safari.
Watu wa Tanga wanaita "gundu."

Tanzania imeshusha thamani ya shilingi.

EA wakanipigia simu kunifahamisha kuwa tiketi yangu inahitaji kuongezwa fedha vinginevyo sitasafiri.

Nikapiga simu Nairobi kuwapa taarifa waongeze fedha kwenye tiketi yangu.
Fedha zenyewe dola ya Mmarekani.

Hii huipata popote ila Benki Kuu na mlolongo wake mrefu sana.
Nairobi ofisi imefungwa kwa ajili ya Christmas.

Safari ikaingia hatihati.
Baba yangu ana travel agency - Sykes Travel.

Nikenda kumweleza tatizo lililonifika.

Palepale akamwamuru Meneja wa Sykes Travel Agent afuatane na mimi hadi AE Mtaa wa Ohio na ahakikishe kuwa naandikiwa tiketi nyingine na yeye atalipa.

Dada yangu Mariam Tewa Allah amrehemu alikuwa akifanya kazi EA dakika tatu hazikufika tiketi ninayo mkononi.

Nilipanda EA kuelekea Khartoum na kulikuwa na transit ya muda mrefu Addis Ababa kutwa nzima hadi siku ya pili mchana ndiyo tunaruka kwenda Khartoum.

Abiria wa daraja la kwanza walishushwa na basi la EA Hilton na si abiria wa kawaida tukapelekwa kulala Wabe Shebele Hotel.

Hii Wabe Shebele ilikuwa hoteli kubwa ya sifa katika wakati wake lakini Mengistu alipompindua Haile Selassie mambo yakaanza kuharibika.

Wabe Shebele ikaporomoka kama ilivyoporomoka nchi nzima.

Kijana wa Kariakoo Hussein Shebe na bendi maarufu The Ashantis walikuwa wakipiga muziki wao hapo Wabe Shebele.

Billy Bandawe alikuwa kiongozi Yanga katika 1980s na mchezaji pia katika miaka ya 1960s alinihadithia kuwa Yanga ilikwenda kucheza na St. Michael ya Ethiopia na timu ilifikia hapo.

Katika wachezaji wa Yanga alikuwa Awadh Gesani.
Awadh Gesani na Hussein Shebe ni ndugu.

Katika moja ya show zake hapo wachezaji wa Yanga walikwenda kumsikiliza Hussein Shebe na Ashantis.

Hussein alipomuona Awadh na wachezaji wengine wameingia hapo ukumbini huku akiimba alishuka kwenye jukwaa akampandisha Awadh na kumtambulisha kwanza kwa Kiingereza kisha akamtambulisha kwa Kiswahili na kuongea maneno mengi ingawa akijua Waethiopia hawajui Kiswahili.

Nilikula chakula cha jioni hapo na nikaliona jukwaa ambalo Hussein Shebe na Ashantis wakipiga muziki wao.

Wabe Shebele imechoka ni kivuli cha hoteli iliyokuwa maarufu.

Nimeletewa Coca-Cola kwenye chupa iliyosagika na kupoteza haiba yake kuwa hii ni chupa ya kinywaji maarufu dunia nzima.

Mkosi ulinikuta barabarani vijana wadogo wa mtaani kama watano hivi walinifuata wakiniomba fedha.

Wakati naingiza mkono mfuko wa nyuma wa suruali mmojawao akachomoa kalamu yangu mfuko wa shati.

Kalamu hii ni Cross ina lifetime guarantee.
Ikiharibika unawarudishia wanakuletea nyingine bure.

Kijana kabla hajanyanyua mguu nikawa nimemdaka.
Safari hii nilikuwa nakwenda ofisi za OAU nikapaone.

Huwezi kuamini.
Ilikuwa mchana wa jua kali.

Nimefika OAU gate ziko wazi.

Naangalia askari.
Hakuna.

Nimepigwa na butwaa.
Nikaona kibanda cha askari pembeni.

Nakakisogelea.
Nikachungulia ndani.

Askari wawili wako ndani wamekaa kwenye viti wamelala fofofo.

Sasa hili la sanamu la Mwalimu Nyerere AU limenikumbusha hawa askari walalavi na mengine.

Nimefika Addis mara tatu na kila safari ina gundu lake la kuhadithia.
1709137460945.png

University of Khartoum​
 
Syll...
Soma makala hayo hapo chini:

SIGARA "CLIPPER" ALIYOKUWA AKIVUTA MWALIMU NYERERE
Picha hiyo hapo chini imepigwa mwaka wa 1955 Magomeni Mapipa Mtaa wa Jaribu kwenye Tawi la TANU alilofungua Ali Msham nyumbani kwake.

Ali Msham ni huyo upande wa kulia aliyekuwa katika ya vijana wawili wamepiga lubega za kaniki mmoja ana shoka begani.

Hawa walikuwa Bantu Group wahamasishaji umma na walinzi wa viongozi wa TANU.

Waliokaa kulia ni Zuberi Mtemvu, Julius Nyerere na John Rupia.
Ukimwangalia Nyerere utaona ameshika paketi ya sigara na ana sigara mkononi.

Mwalimu katika ujana wake akivuta sigara na sigara yake ilikuwa "Clipper," sigara maarufu enzi hizo. Paketi yake ni hiyo hapo juu.

Mwalimu aliacha kuvuta mwaka wa 1962 baada ya kifo cha rafiki yake kipenzi Hamza Mwapachu kufariki kwa maradhi ya moyo yaliyosababishwa na uvutaji sigara.
1709147298365.png

1709147344369.png

Aisee.
Na sio tu nimeona hiyo paketi na sigara, nimeona pia hao Wazee JR na ZM walivyo fanana na wanawe. Balozi (R.I.P) na Mbunge.

...kumbe vinasaba vinatembea mbali sana.

Namuona Mzee Zuberi alivyofanana na mbunge wetu! Sura-kope lol
 
Hii picha ni katika picha 11 nilizopewa na watoto wa Ali Msham kama ushahidi wa mchango wa baba yao katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Search "Ali Msham."
 
Back
Top Bottom