Green Guard wa CCM wamjeruhi dereva wa mbunge wa CHADEMA

MZK

JF-Expert Member
Sep 13, 2012
223
303
Habari za kusikitisha sana kutokea katika Nchi ya Kidemokrasia. Dereva wa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga kupitia CHADEMA Salome Makamba, amejeruhiwa na Vijana wa CCM maarufu kama Green Guard. Dereva huyo amejruhiwa vibaya sana sehemu mbali mbali za mwili wake na amelazwa katika Hospitali ya Halmashauri ya Kahama.

Matukio kama haya yamefanyika wakati wa Uchaguzi wa Udiwani Kata ya Segese, kinachosikitisha pia Timu ya kampeni ya CCM inasemekana alikuwapo pia Waziri wa Mambo ya Ndani hivyo wananchi walitegemea uchaguzi utakuwa wa amani kwani Waziri mwenye dhamana ya ulinzi inasemekana alikuwapo huko wakati wa kampeni

Picha ya Dereva aliyejeruhiwa

IMG_20170124_081103.JPG
 
mkuu hao jamaa hata kama wangeamua kumuuwa na kuchoma gari yake moto bado wangetetewa tu,usifikiri matendo hayo ya ukatili wanayafanya kwa kupenda bali ni mashinikizo kutoka juu

nenda leo burundi kuna kikundi kinaitwa "imborenakhule" hawa wahuni wapo chini ya serikali ya burundi wanauwa watakavyo acha kabisa

hii ndio afrika mkuu
 
Chadema nao wamekuwa mdebwedo kupita kiasi. Mbona mishale ya sumu inauzwa kila mahali? Mtalia lia Vijana mpaka lini? Hivi kapigwa dereva kaumizwa halafu Vijana wa green guard wawili waka rip kwa mishale mnadhani yatatokea hayo tena?
Sasa hivi manung'uniko yenu ya kila siku yamekuwa wimbo wa burudani kwa Ccm na vibaraka wao.
Kama hamuwezi kuchukua hatau za kuondoa unyonge basi mlilie hukohuko mahospitalini mkitibu majeraha au mkizikana, maana hata manyang'au ikinachofuata watakuueni wazidi kufurahi na hakuna hatua watachukuliwa zaidi ya kupongezwa.
Jee mnakubali kuendelea kuwa mdebwedo?
 
Chadema nao wamekuwa mdebwedo kupita kiasi. Mbona mishale ya sumu inauzwa kila mahali? Mtalia lia Vijana mpaka lini? Hivi kapigwa dereva kaumizwa halafu Vijana wa green guard wawili waka rip kwa mishale mnadhani yatatokea hayo tena?
Sasa hivi manung'uniko yenu ya kila siku yamekuwa wimbo wa burudani kwa Ccm na vibaraka wao.
Kama hamuwezi kuchukua hatau za kuondoa unyonge basi mlilie hukohuko mahospitalini mkitibu majeraha au mkizikana, maana hata manyang'au ikinachofuata watakuueni wazidi kufurahi na hakuna hatua watachukuliwa zaidi ya kupongezwa.
Jee mnakubali kuendelea kuwa mdebwedo?

Nikweli kabisa,,,wamekuwa laini sana
 
Nikweli kabisa,,,wamekuwa laini sana
Na sijui wanadhani kulalamika kutasaidia nini? Hata kule Zenji nako ambako kulikuwa ngangari sasa hivi wanalia eti zombie wanatupiga! Watu wamepatwa na nini?
Ulimwengu wa sasa ni tofauti, hakuna kulialia na jino kwa jino. Ona kule Israel kulivyo tulia sasa. Zamani ukitega bomu likaua watu wao watatu wao wanatuma ndege za vita inachakaza kitongoji na mnachimba makaburi mia mpaka wameacha ujinga.
 
huu ni uzushi, uongo na uchochezi uliopituka mipaka. acheni kutafuta promo zisizo na maana
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kuhutubia pale UDSM Nkrumah Hall, akasema, ' unatakiwa kuifanya haki yako kama mali yako yenye thamani kuliko chochote, mtu akikunyang'anya, ni lazima udhihirishe kuwa ni mali yako na hutakubali iporwe. Na akikimbia nayo halafu akaenda nayo kwake akajifungia ndani ya nyumba yake, wewe uliyeibiwa una mawili, moja ni kuvunja mlango auirejeshe mali yako lakini unapovunja, hujui humo ndani utamkuta amejiandaje. Uamuzi wa pili ni kuamua kuondoka, na kuipoteza mali yako'.

Habari za viongozi au wapenzi wa vyama vya upinzani kupigwa au kutekwa na greenguards tumezisikia mara nyingi. Cha kujiuliza ni je, wataendelea kulalamika mpaka lini? Ina maana hao wapenzi wa CCM/greenguards wana akili na uwezo kuwazidi wapinzani wote? Tangu waanze kulalamika wamepata nini? Kama hawajapata chochote, kuna umuhimu gani kuendelea kulalamika wakati unajua hakuna hatua zitakazochukuliwa dhidi ya unaowalalamikia?

Vyama vya upinzani vinatakiwa kutafakari, na kuona mbinu na mipango gani utavisaidia ili wasiendelee kuwa walalamikaji wa kupigwa na greenguards au kuibiwa kura. Unaibiwa leo, na kesho na keshokutwa, upo tu!!
 
Back
Top Bottom