Mlenge
R I P
- Oct 31, 2006
- 2,125
- 2,291
Pongezi lukuki kwa juhudi za Serikali-Mtandao, mfano mzuri ukiwa Government electronic Payment Gateway (GePG), mfumo wa malipo ya kielektroniki kwa serikali.
GePG imeleta maboresho makubwa kwa upande wa kuilipa serikali, kwani sasa hivi unaweza kuilipa serikali ya Tanzania uwapo popote Tanzania. Sasa unaweza kuilipa serikali na taasisi zake kwa njia za kielektroniki kutokea kwenye simu, kupitia kwa mawakala na hata kwa mabenki.
Yafuatayo ni mapendekezo kuboresha zaidi huduma hizi.
1. Business Process
Baadhi ya huduma zinazotolewa na serikali taratibu zake (business process) hulazimisha mtu kwenda kupata huduma ofisini. Huduma nyingine kweli pana umuhimu wa kwenda ofisini, lakini nyingine hazina umuhimu wala ulazima.
Kwa mfano,
(a) Baada ya kufanya malipo kwa GePG, ofisi ya umma inakuambia ulete uthibitisho wa malipo. Hii haina mantiki kwa vile kwa mfumo wa kieletroniki wao wanatakiwa waweze kufikia sehemu ya kiutawala ( backend) ya GePG kujua nini kimelipiwa au bado. Afisi za serikali zingekatazwa kudai uthibitisho wa malipo kwa kitu chochote kilicholipiwa kielektroniki. Ofisi hizo ndio ziseme kitu hiki kimelipiwa au la. Wadai uthibitisho pale tu panapokuwa na sintofahamu ya mtu kuwa amelipia na wao wanasema hapajalipiwa.
(b) Kuendana na (a) hapo juu, kila ofisi inayopokea malipo kwa GePG, iweze kutoa risiti za kielektroniki (self-service) kwa kila malipo. Risiti hizo zitumwe kwa barua pepe au ziwepo kwenye app ya simu na website ya GePG. Mtu atakayetaka kupata nakala ngumu, ndie ajipatie usumbufu wa kwenda ofisini kuomba nakala ya risiti.
(c) Kila mwananchi au mlipaji mwingine aweze kuwa na uwezo wa kujitengenezea ankara za malipo, kulipa, na kuwa na uwezo wa kujionea historia ya malipo mbalimbali aliyofanya kwa serikali.
(d) Helpdesk ya GePG iwekewe sehemu ya kujiandikisha ili kuitumia. Kwa sasa http://helpdesk.gepg.go.tz/ haina huduma hiyo.
(e) Pesa za kigeni -- sina hakika iwapo GePG inaweza kuzipokea. Kwa sasa baadhi ya huduma ni za kwa ajili ya watu walioko nje ya Tanzania. GePG iwezeshe watu kuilipa serikali kwa njia yoyote inayowezeckana. Mf. Visa na Mastercard, Paypal, Skrill, n.k., na kwa pesa kadhaa za kigeni, na hata cryptocurrencies. Kufikia hili, GePG inaweza pia kushirikiana na payment gateway za binafsi zitakazokuwa zikiongea na GePG. Mfano wa gateway hizo ni Directpay Online (https://www.directpay.online/online-payments-tanzania/) , Lipa (http://lipa.co.tz/) na hata paypal (www.paypal.com).
Uwezekano mkubwa huduma hizo tayari zipo, ila tu awareness kwa public bado.
End of Feature Requests.