Going thru Divorce

Nakupa offa uje tuone hii picha kwangu off course na Belinda akiwepo maana huwezi jua....labda utaondokana na wazo eti wakina mama wanalea vizuri kuliko kina baba....

Masa

...talking about mifano ya movies, hata Kramer vs Kramer, au The Champ ni baadhi tu ya mifano japo kuna wengine watasema aaargghh, si maigizo tu1 Wanasahau zote zilikuwa based on true story, kama ile Not without my daughter!

...Back to reality, kuna watu ambao kuzungumzia mas'ala ya talaka na kuachana wao wanaona kama taboo! utawasikia oooh, msizungumzie hilo...vibaya, uchuro. Ni sawa na wale wasiotaka kuandika will kwa kukiogopa kifo, japo wanajua ipo siku roho itaacha mwili!

Kuna manyanyaso makubwa wawili wanapoachana;

1. Mume anashikilia mali

2. Mke anashikilia watoto

kwanini?
 
una manyanyaso makubwa wawili wanapoachana;

1. Mume anashikilia mali

2. Mke anashikilia watoto

Mbu unavituko sana nilikuwa sijaona signature yako looohh haya mpwa!

Mzee kama ni mali nitamwachia kila kitu, ila watoto wangu aniachie...maana njemba nyingine ianze kubandua mama yao watoto watajisikia vibaya.....I will rather fight again to achieve mali zingine....
 
Kihivi na sababu hii: Nimeona watu wengi wakienda cancelling mambo ya mahusiano na kama wakitaka kuachana kwa talaka wafanyaje tena kama wana kids na kuwashirikisha. I mean ni ngumu ila inaweza kuwa rahisi na mkabaki friends baada ya kutua mzigo kwenye maisha yenu.

Kufikishana kwenye vyombo vya sheria inatokana na wengine kutalikiana kwa kushirikisha sheria huku mojawapo ya kitu muhimu ni malezi ya watoto(incase wanao)..Ina mana wenyewe binafsi wanandoa wameshindwa kukubali kuwa lea watoto ninatoa support nk kwahiyo wanabishana na kila mmoja akivuta watoto upande wake..

Back to you: Wewe unaonaje?Watoto wakae na nani, mama au baba?Maana kuhusu kuoa/olewa tena kati ya hao wanandoa watakaoachana inaweza itokee au isitokee japokuwa lazima relationships watakuwa nazo na watu wengine watakaokutana nao maishani mwao tena.

...BJ nadhani unamaanisha Counselling, au? ...kwa maana hiyo, kutokana na mila na desturi zetu wabantu inatuwia ngumu kupata suluhisho za namna hiyo kutokana na mapungufu ya kisheria au?

Tukirudi kwenye maaadili na tamaduni za kikwetu. Panapotokea mifarakano, mara nyingi pataitishwa kikao cha familia kujaribu kuwasaidia makubaliano mtavyoachana. Mara nyingi hii humpelekea mzazi aliye na uwezo kupewa jukumu la kulea watoto wakubwa, na yule/wale wadogo kuendelea kulelewa na mama, au sio jamani?

Tatizo langu linakuja, hata kama mama anaamini mumewe ana uwezo wa kulea watoto wote, bado yeye atang'ang'ania kuwachukua wanawe, na kama hiyo haitoshi...ugomvi kila mara kutaka mafungu na mafungu yaliyopitiliza ya hela za matumizi toka kwa mtalaka wake.

Hamuoni hapo mama anatumia mtoto/watoto kama fimbo ya kumchapia mumewe?

Mume nawe, kwa kumwambia mkeo aondoke na kila alichokuja nacho, huoni unamnyima mkeo haki ya kudai kila mlichochuma naye?
 
Mbu
Asante kwa kunisahihisha,kweli nilimaanisha counselling.
Suala la wanawake kung'ang'ania watoto ni kutokana na mawazo kwamba mume mtaliki ataoa au kuwa na mwanamke mwengine hivyo na kuwaza watoto wake watateseka kwa mama wa kufikia. Of which is not true,siyo kila mzazi mlezi anawafanyia hivyo watoto wa mwandani wake. Ni kasumba fulani iko akilini hivyo kuibadili kwa wengine ni ngumu na shughuli kubwa sana.
Mambo ya talaka ni magumu sana na mazito na ukisikia watu wametalikiana ujue kuna kitu/vitu vimewafanya waachie walipofikia.Tatizo kubwa ni jinsi ya kuachana na maisha ya hao watu baada ya talaka tena kama wana watoto. Kuambiwa ondoka na ulicho nacho bila kujali muda na mali mlizochuma wote inauma ndo mana urafiki hauwezi kuisha na kuona talaka ni kama sehemu ya maisha.
 
Mbu unavituko sana nilikuwa sijaona signature yako looohh haya mpwa!

...ha ha ha, kulala na njaa ndani ya chandarua wakati kwa chandarua hicho waweza vulia samaki ni sawa na msemo, uchumi mnao lakini mnaukalia!

Mzee kama ni mali nitamwachia kila kitu, ila watoto wangu aniachie...maana njemba nyingine ianze kubandua mama yao watoto watajisikia vibaya.....I will rather fight again to achieve mali zingine....

...kwahiyo mpwa upo radhi njemba nyingine zitanue ndani ya 'Prado' yako na ile 'mansion' uliosota kuijenga miaka nenda rudi pale 'Rock City?'...upo tayari kusota 'uswazi' na wanao kwenye chumba cha kupanga na kila kukicha kukimbizana na dala dala?

mambo ya pride magumu bana, yataka moyo aisee... :D
 
...kwahiyo mpwa upo radhi njemba nyingine zitanue ndani ya 'Prado' yako na ile 'mansion' uliosota kuijenga miaka nenda rudi pale 'Rock City?'...upo tayari kusota 'uswazi' na wanao kwenye chumba cha kupanga na kila kukicha kukimbizana na dala dala? mambo ya pride magumu bana, yataka moyo aisee... :D

Mazee kwa kweli niko tayari, nitanunua hata Kibajaj 4WD na kupanga nyumba kule Kapili point baada ya muda nitakuwa kwenye mstali najua kwa kuwa nitakuwa mzima nitamtimulia vumbi na X5 mpya.....nikiwa na amani na raha zangu...
 
...Tatizo kubwa ni jinsi ya kuachana na maisha ya hao watu baada ya talaka tena kama wana watoto. Kuambiwa ondoka na ulicho nacho bila kujali muda na mali mlizochuma wote inauma ndo mana urafiki hauwezi kuisha na kuona talaka ni kama sehemu ya maisha.

that's what am talking about!

Ukishaliweka akilini suala la kuoana kwa heri, na kuachana kwa heri nadhani haitokuwa ngumu kuzingatia haki za kila mhusika kwenye ndoa yenu.

Ile shari ya kukomoana ndio inayoletesha mama kuingia mitini na watoto, mume naye kung'ang'ania mali! Haipendezi mmeachana halafu mazungumzo baina yenu yanafanyika via watoto, solicitors, au ustawi wa jamii :)
 
Mazee kwa kweli niko tayari, nitanunua hata Kibajaj 4WD na kupanga nyumba kule Kapili point baada ya muda nitakuwa kwenye mstari najua kwa kuwa nitakuwa mzima nitamtimulia vumbi na X5 mpya.....nikiwa na amani na raha zangu...

Ndo maana sikuachii nakwambia, kwako nitabanana tu mpaka kieleweke maana najua mwisho wa siku lazima niachie kasri na mikoko. Nimekosa nini sasa mpaka nikimbilie kwengine muda huu..ha ha ha
 
Ndo maana sikuachii nakwambia, kwako nitabanana tu mpaka kieleweke maana najua mwisho wa siku lazima niachie kasri na mikoko. Nimekosa nini sasa mpaka nikimbilie kwengine muda huu..ha ha ha

Thats sweet of you.....hapa tunawapa hisia zetu na ushauri nasaha! sisi is for life hata tukifa kaburi moja!
 
Masa naona muda si mrefu Mbu atakuwa kwetu tunasema 'mtwanzi' wako kwa mdogo ake Bellies tafadhali muheshimu lasivyo atakupa maralia mwaka mzima.
 
Ndo maana sikuachii nakwambia, kwako nitabanana tu mpaka kieleweke maana najua mwisho wa siku lazima niachie kasri na mikoko. Nimekosa nini sasa mpaka nikimbilie kwengine muda huu..ha ha ha

wewe BJ wewee, :D shauri yako,...kuna wengine wataku challenge hiyo sentensi niliyoitia wekundu. Kasri na mikoko vitu vya mpito hivyo, penzi likichuja je?

Anyway,...kwanini mume na mke wakishaachana, utawaona (wengi wao) bado wanaendelea kukomoana?
 
Masa naona muda si mrefu Mbu atakuwa kwetu tunasema 'mtwanzi' wako kwa mdogo ake Bellies tafadhali muheshimu lasivyo atakupa maralia mwaka mzima.

Nimekusoma mazee, anakaribishwa ila asilete ushabiki wa mpira home!
 
Nimekusoma mazee, anakaribishwa ila asilete ushabiki wa mpira home!

....ha ha haaa :D sawa, nikifika mlangoni navua jezi, tukiangalia mpira kwenye Tv hakuna kushangilia goli wala ku smile! kaaaaaazi kweli kweli.
 
....ha ha haaa :D sawa, nikifika mlangoni navua jezi, tukiangalia mpira kwenye Tv hakuna kushangilia goli wala ku smile! kaaaaaazi kweli kweli.

Kuna siku nilienda ukweni (kwa kina Belinda off course) siku hiyo Chelsea walikuwa wanacheza na Everton, na Liverpool walikuwa wanacheza na Aston Villa....channel tofauti zilikuwa zinaonyesha mipira hiyo. Kumbe mdingi alikuwa ni mshabiki wa Liverpool wakaweka ile channel. Mzee wa ze blues nikaomba remote...si nikabadili channel...bila kujua mzee aliboreka half time bellies akanambia kwa sms mazee umeboa warudishie ile ya awali....niliaga ghafla.....kuwahi pub kumalizia second half
 
that's what am talking about!

Ukishaliweka akilini suala la kuoana kwa heri, na kuachana kwa heri nadhani haitokuwa ngumu kuzingatia haki za kila mhusika kwenye ndoa yenu.

Ile shari ya kukomoana ndio inayoletesha mama kuingia mitini na watoto, mume naye kung'ang'ania mali! Haipendezi mmeachana halafu mazungumzo baina yenu yanafanyika via watoto, solicitors, au ustawi wa jamii :)

Umeongea ukweli,kila kitu ni heri kuoana au kutalikiana kwahiyo maisha yaendelee vizuri.
Ndoa kama ndoa ni makubaliano kati ya watu wawili na wanaokaa pamoja katika maisha yao hivyo kuachana ikiwa kati yao wawili pia inapendeza. Hivyo vikao vinaweza kuitishwa hata kila mwezi lakini kama hao wanandoa wawili hawawezi kukaa tena pamoja au kurekebisha mapungufu na matatizo katika ndoa yao ni kazi bure. Na mwisho wa siku hao hao ndo wana maamuzi juu ya ndoa yao huku wakiwafikiria watoto wao katika ndoa yao ila siyo kutumia kigezo cha watoto kukaa pamoja wakati wamefika point ni heri wapeane nafasi.
Altenatively kuseparate kama watahitajiana warudiane au talaka kabisa.
Ndoa ni good experience though ukiacha talaka na matatizo mengine, next time tuongelee upande mzuri wa ndoa na raha zake pia jinsi ya kuboresha mahusiano ya wanandoa.
 
wewe BJ wewee, :D shauri yako,...kuna wengine wataku challenge hiyo sentensi niliyoitia wekundu. Kasri na mikoko vitu vya mpito hivyo, penzi likichuja je?

Anyway,...kwanini mume na mke wakishaachana, utawaona (wengi wao) bado wanaendelea kukomoana?

Nope,wasinichallenge ni utani tu jamani. Siwezi kumfanyia hivi hata tone.
Pia muda mwingine wanaume wanawaachia wanawake nyumba na kila kitu akijua labda na watoto kwahiyo akae vizuri na kule watoto wao kwa kuwa wamekorofishana.
Siwezi kuita ulimbukeni ila mapenzi yanachangia. Umempenda mtu hupendi ateseke hata kama hatakuwa na wewe tena. Kukomoana ni kama vile kumwonyesha mwenzio kuwa bila wewe naweza au wewe umesusa wenzio wala ila yana mwisho na inabidi upande mmoja udharau kukomolewa hatimaye mkomoaji atajiona mbona hafuatiliwi na kuacha mwenyewe.
 
... next time tuongelee upande mzuri wa ndoa na raha zake pia jinsi ya kuboresha mahusiano ya wanandoa.

...ndio, lakini kuelezeana 'machungu ya kaburini' (I mean kuachana) kunasaidia wale wenye roho dhaifu kurudi kwenye msitari na kuondoa tofauti katika ndoa zao.

... Kukomoana ni kama vile kumwonyesha mwenzio kuwa bila wewe naweza au wewe umesusa wenzio wala ila yana mwisho na inabidi upande mmoja udharau kukomolewa hatimaye mkomoaji atajiona mbona hafuatiliwi na kuacha mwenyewe.

...te he hee :D
 
Ndiyo maana wazee wetu walisema ndoa ni msalaba, unabidi uubebe mpaka mwisho wa safari yako duniani, Mungu anakataa kuachana.

Ugonvi wa wanandoa kwa kweli maumivu ni kwa watoto. hii inabaki maishani. Ngumu zaidi pale wazazi waliotengana wamezeeka na wanahitaji msaada toka kwa watoto. Hapo ndipo watoto wana-pay zaidi price ya wazazi kuachana. Huwezi ukatuma pesa kwa baba halafu kwa mama, ni gharama mara mbili. Wangelikuwa pamoja natuma once au hata kama ni huduma najua naipeleka nyumbani ambako wote wanaishi.

Tusizizungumzie kuachana, tujaribu kuangalia jinsi gani tutadumisha wazazi waishi pamoja, walee watoto na mwisho wale matunda ya watoto wao. I hate hii idea ya kuachana.

Mungu uzibariki hizi ndoa, nanyi mnaoolewa kwa kutoa nuksi, pleease, msifuate mkumbo halafu mnasababisha kuachana. You have only one chance to select your love.

Nawatakia upendano wenye mafanikio usio na fitina wala majaribu.
 
The situation is you have to be in to understand is soo confusing depend on the divorse base.The bottom line is wakinadada wanakuwa na emmotion zaidi when you come to divorse.Is very important wakati devorse inapotokea kupata ushauri wenye hekima otherwise watoto wasio na hatia ndio watakuwa waathirika wakuu.Emmotion za akinadada zinazidi hasa kwa wale house wives considering the cost of life after divorse.Is up to us men to make this transition process as smooth as possible.KAMA NDOA HAIWORK WANDUGU GET DIVORSE DON'T WAIT.Wengi tunasingizia watoto but watoto sio sababu ya kuwa pamoja kama hamna furaha ndani ya nyumba.Children will be fine.IF ANYONE GOES THROUGH DIVORSE YOU CAN CONTACT ME FOR MORE TRANSITION HELPFULL INFORMATION.

SAHIBA.
 
Back
Top Bottom