Godbless Mushi adaiwa kujaribu kumbaka mtoto wake wa miaka mitano

Nyuki Mdogo

JF-Expert Member
Oct 31, 2021
4,138
10,539
Jeshi la polisi mkoani Mwanza limemkamata na linaendelea kumhoji Godless Mushi (39) mfanyabiashara wa kuza vifaa vya magari kwa tuhuma za kujaribu kumbaka mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka mitano

Taarifa ya jeshi la polisi kwa vyombo vya Habari inasema mnamo Aprili 2/2023 saa nne usiku katika mtaa wa Shibula wilayani llemela mwanaume huyo alitaka kumfanyia mtoto wake kitendo cha udhalilishaji wa kingono wakati akiwa amelala chumbani kwenye kitanda cha wazazi wake wakati mama yake mazazi akiwa anaendelea na shughuli zake za nyumbani


Aidha jeshi hilo kupitia dawati la jinsia na Watoto limesema uchunguzi kuhusiana na tukio hilo unaendelea kwa kuwahoi mashahidi na kumfanyia binti huyo chunguzi wa kitaalamu, na kwamba wanashirikiana na ofisi ya Ustawi wa jamii Mkoa wa Mwanza na upelelezi utakapo kamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani

Chanzo: East Africa TV
 
Hakuna hata mwenye uhakika wa habari, haya wana jf njooni tupige ramli
 
Unaweza kukuta Mama amemuundia zengwe Baba ili kumpoteza..
Mazingira kama hayo yalitokea Moshi au Arusha tukabishana humu ila ukweli ni masharti ya waganga maana yule wa mwanzo ni mfanyabiashara kama huyo wote wachaga na alikuwa na mabinti wakubwa tu ..kwa nn afaute kitoto
 
Soma hii kwa makini,mada yetu hii inasema adaiwa kumbaka mtoto wake na tamko la polisi linasema ajaribu kumbaka mtoto wake!,tendo la kubaka halijafanyika!
 
Back
Top Bottom