Godbless Lema kurejea nchini hivi karibuni

2025DG

JF-Expert Member
Jan 30, 2023
508
1,426
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini, Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama na aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Jonathan Lema, atarejea nchini March 01, 2023, siku ya Jumatano, saa sita kamili mchana kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

“Lema, aliondoka nchini na kuelekea Kenya tarehe 8 November 2020 ambako alikaa kwa mwezi mmoia na kisha tarehe 8 December 2020 alielekea nchini Canada ambako alipata hifadhi ya kisiasa kutokana na kuwepo kwa tishio la kuuawa yeye na Familia yake”

“Atakaporejea nchini, Lema atapokelewa uwanja wa ndege (KIA) na Viongozi wa Chama, Wananchama na Wananchi watakaojitokeza kumpokea na kisha atakwenda moja kwa moja kwenye mkutano wa hadhara utakao fanyika Arusha Mjini”

“Lema, baada ya kurejea atakuwa na vikao ya kazi ya kuongoza kikao cha Kamati ya Utendaji ya Kanda na Baraza la Uongozi la Kanda ya Kaskazini na kisha ziara za mikutano ya hadhara na vikao vya ndani kwenye Mikoa yote ya kanda ya Kaskazini (Tanga, Kllimanjaro, Arusha a Manyara), pia atashiriki kwenye mkutano Mkuu wa Jimbo la Arusha Mjini na atakuwa na ratiba ya ziara kwenye Kata mbalimbali za Jimbo la Arusha Mjini”
 
Hakika lazima tuuseme ukweli panapostahili kusema.

Ameruhusu siasa za vyama pinzani kuendelea pasipo kupigwa virungu wala kutupwa lupango.

Ameruhusu mchakato wa katiba mpya uendelee.

Tundu Lissu amerejea nyumbani kutoka alikokimbilia kuiokoa roho yake.

Anarudi Lema kutoka alikokimbilia kuinusuru roho yake kutoka kwa wauwaji.

Atarudi mh Wenje amabaye alikuwa anasakwa kama kipusa kisa siasa.

Kumbuka hao wote na mambo yote niliyo yataja yalikatazwa na Jiwe yasifanyike akiwa hai maana yeye hakuhitaji kupingwa wala kuhojiwa.

Nini tunataka angalau kumpongeza mama Samia?

Tuwache roho mbaya jamani kama taifa tunaelekea angalau panapotia moyo.

Screenshot_20230216-163437_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom