DOKEZO Giza limetawala Kituo cha Daladala Mbezi Mwisho, abiria wanategemea mwanga wa taa za gari

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Taa za Kituo cha Daladala cha Mbezi Luis maarufu kwa jina la Mbezi Mwisho haziwaki na hali ya Giza imetawala eneo hilo na hivyo kuhatarisha Usalama wa mali na abiria wenyewe.

Mpishano wa magari unaendelea huku purukushani za watu nazo zikiendelea hivyohivyo.

Kwa ninavyowaona vijana ambao tunawajua kuwa sio watu salama, nao hawachezi mbali Kila Daladala inapofika ila hawaingii, najua utakuwa umeshaelewa namaanisha kina nani.

Hii pia sio mara ya kwanza kwa taa za Kituo hiki kutowaka nyakati za usiku, hii inavyoonekana uongozi wa kitoo hili au wa Wilaya umeshindwa kuwajibika ipasavyo.

Ajabu sehemu nyingine zonazozunguka Kituo hicho umeme upo kama kawaida.

Hatua zichukuliwe
IMG_20230710_191509_251.jpg

IMG_20230710_191233_326.jpg

IMG_20230710_185927_928.jpg
 
Back
Top Bottom