Ghasia: Msibweteke kikombe cha babu

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174
Ghasia: Msibweteke kikombe cha babu Send to a friend Sunday, 29 May 2011 22:15

Elizabeth Ernest
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Hawa Ghasia, amewataka wahitimu wa Chuo cha Utumishi wa Umma kutobweteka na tiba ya magonjwa sugu inayotolewa na Mchungaji mstaafu Ambilikile Mwaisapila wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na badala yake wajikinge na mambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU).

Ghasia alitoa kauli hiyo juzi jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wahitimu hao na kuwataka kuepukana na majanga ya maradhi ili walitumikie taifa kwa kutumia taaluma waliyoipata. “Najua kuna kikombe cha babu, lakini kikombe hicho siyo kinga ya janga la ukimwi. Nimalizie kwa kuwaasa kuwa waangalifu na afya zenu ili kuepukana na majanga ya maradhi yanayowakumba Watanzania,” alisema.

Alisema masharti ya babu ni magumu kwani kikombe hicho kinatolewa mara moja tu na kufafanua kwamba wahitimu hao wanapaswa kuwa waangalifu wa afya zao ili kulinda ujuzi walioupata.

“Kikombe cha babu kinatolewa mara moja tu, na siyo kinga kwa hiyo kama hautakuwa mwangalifu kwa kulinda afya yako ukitegemea kikombe, basi tutaendelea kupoteza rasilimali watu ambayo imepatikana kwa gharama kubwa, wazazi wenu wamewekeza katika elimu,” alisema. Pia Ghasia aliutaka uongozi wa chuo hicho kujikita kwenye tafiti za kuboresha huduma katika jamii.

“Nawashauri waajiri wote wa umma Tanzania wakitumie chuo hiki kwa ufanisi wa kazi zenu, wenyewe mmekuwa mashahidi kwamba chuo hiki kinakua siku hadi siku,’’alisema. Akisoma risala yake kwa Waziri Ghasia mkuu wa chuo hicho, Said Nassor alisema mwaka jana chuo hicho kilianza kukarabati kituo cha mafunzo ya watumishi wa umma.

Alisema chuo hicho kinaendelea kupanua wigo wa kutoa mafunzo kutoka ngazi ya cheti mpaka Stashahada.“Chuo kiko mbioni kutafuta uwezo kwa kujenga tawi lake katika Wilaya ya Rufiji, mkoani Pwani kwani tayari tuna hekari 200 ambazo kwa sasa tuko katika mchakato wa kutafuta hati mikili,’’alisema.


 
Back
Top Bottom