Gharama za mazishi ya Kanumba - huu ni upumbavu

HAKUNA

Senior Member
Mar 12, 2012
133
66
Jamii yetu imekuwa ikivutwa na hisia zaidi kuliko kuangalia uhalisia wa jambo. Tumekuwa tukitumia pesa nyingi sana kwa kuchangia shughuli za harusi, mazishi, happybirthday part, kumtoa mtoto arobaini, kumcheza mtoto ngoma, ubatizo, kipaimara, maulid na mengineyo.

Kubwa zaidi ni mazishi ya KANUMBA eti watu wamechanga milioni 70; Nimejaribu kufuatilia gharama za mazishi katika nchi za wenzetu, yanakaribia dola $9000, imezidi sana haizidi dola $15,000. Hata hivyo gharama hizi kwa nchi za wenzetu inabidi ujiandae mwenyewe wakati wa uhai wako, kwa hiyo katika financial plan zako inabidi uweke na gharama za mazishi siku ukifa. Hapa bongo tunachangishana millioni 70 ndani ya wiki 1, halafu tunadai sisi ni maskini, hii ni laana tunajitafutia.

Kama kuchangiana ndio utamaduni wetu, kwa nini hatuna utamaduni wa kuchangiana katika mambo ya msingi...............??????, ELIMU, HUDUMA ZA AFYA, BIASHARA n.k
 
Cha kushangaza zaidi kuna msanii mwenzao anaitwa Sajuki anaitaji milioni 25 kwenda India kutibiwa hakuna hata msanii anayejigusa wanasubiri akifa wachangie milioni 30 za mazishi na mashairi mengi ya tulimpenda zaidi, Huu ndio unaitwa usanii kila kitu kuigiza
 
nina imani kuna mambo ya msingi mengi ya kujadili,huyu kanumba muacheni adeal na ya huko aliko huku 2kingojea na cc ciku ye2.
 
Cha kushangaza zaidi kuna msanii mwenzao anaitwa Sajuki anaitaji milioni 25 kwenda India kutibiwa hakuna hata msanii anayejigusa wanasubiri akifa wachangie milioni 30 za mazishi na mashairi mengi ya tulimpenda zaidi, Huu ndio unaitwa usanii kila kitu kuigiza

hilo la sajuki hata mi limenigusa! wakina jb sasa hivi wapo kimya, wakisikia tu mwenzao kimenuka watakavyowahi kwenda na kuwa vimbelembele wa kutoa number za m-pesa ili michango itumwe! wakati huu ndio wakati wa kuchangia, wangetangaza sasa ili apate MATIBABU!
 
Hata mm nawashangaa hawa wasanii sijui km wana akili au vipi?..kama hawajala hela watoe mchanganuo kwa kila item km maturubai, jeneza etc
 
kwa nini kwenye hoja zenu zoooooote huwa hamuwaoni wazee wetu wanaoteseka kwenye makambi tuliowaweka eti kwa kuwaiga wazungu? kwa nini watu wasichangie kwa hawa wazee kwani serikali tayari imeshaonyesha haiwezi.
 
Jamii yetu imekuwa ikivutwa na hisia zaidi kuliko kuangalia uhalisia wa jambo. Tumekuwa tukitumia pesa nyingi sana kwa kuchangia shughuli za harusi, mazishi, happybirthday part, kumtoa mtoto arobaini, kumcheza mtoto ngoma, ubatizo, kipaimara, maulid na mengineyo.

Kubwa zaidi ni mazishi ya KANUMBA eti watu wamechanga milioni 70; Nimejaribu kufuatilia gharama za mazishi katika nchi za wenzetu, yanakaribia dola $9000, imezidi sana haizidi dola $15,000. Hata hivyo gharama hizi kwa nchi za wenzetu inabidi ujiandae mwenyewe wakati wa uhai wako, kwa hiyo katika financial plan zako inabidi uweke na gharama za mazishi siku ukifa. Hapa bongo tunachangishana millioni 70 ndani ya wiki 1, halafu tunadai sisi ni maskini, hii ni laana tunajitafutia.

Kama kuchangiana ndio utamaduni wetu, kwa nini hatuna utamaduni wa kuchangiana katika mambo ya msingi...............??????, ELIMU, HUDUMA ZA AFYA, BIASHARA n.k

Nadhani wamekuza au "kupika" taarifa! Milioni 70 kwa kipi hasa? Kusafirisha mwili wa marehemu kutoka Marekani hadi Dar huku mwili ukiwa kwenye casket nzuri utalipa kama $ 15,000....sasa kwa Kanumba wanataka kusema nini kilikuwa kikubwa mno? Jeneza la Milioni 2? Au kulipia kwaya, MC, usafiri na chakula pale nyumbani? Piga ua gharama ile hifiki 20m....sema heabu zimechakachuliwa ili michango yote ionekane ilitumika, wajanja hapo wamepata magari nk...
Bongo zaidi ya uijuavyo
 
Back
Top Bottom