Said Cosmetics
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 2,001
- 1,586
Kwanini hamjamkatia bimaKuna kipindi pia aliumwaaa.... tukafikia hatua tukasema bora tu arudishe number maana sasa inakuwa changamoto kwetu. Akaja akapona. Shida ikawa pale pale. Hakuna afadhali akiwa mzima shida akiugua shida. Ni msumbufu sana.
Sasa this time anaumwa tena. mwezi wa 3 huu amelala tumehamisha hosp zote. Tunagharamia ukimwangalia age yake nayo imeenda sana. 90 plus. Anataka aendelee kuishi kufanya nini hapa duniani? Sasa tunatumia pesa ambazo zingesaidia wajukuu wake kumtibu mgonjwa mbaye kwa kweli ameshakula chumvi ya kutosha hapa duniani. Mwisho wa siku tunamuona tu kama chuma ulete. Maana kila pesa zetu zinaenda kwenye matibabu yake. Meno yake yameshatoka, anaishi kwa shida. Anaanikwa tu juani kama mjusi ila bado anataka aendelee kuishi. Unajiuliza aishi kufanya nini hapa duniani? Mbona alishamaliza kila kitu?
Sasa inafikia kipindi tunasema bora tu akapumzike nasi tupumzike kidogo maana atatufilisi kwa kweli. Mimi nimeshauza gari moja, nimechukua mkopo, nimekuwa sasa nina madeni ile mbaya. Kwa mabro wengine nao.. ishakuwa shida. Maana tulishampeleka mpaka India kipindi fulani. Wakatwambia kwa huu umri asifanyiwe hayo matibabu maana kinga zake nazo zimekosa nguvu. So alilazwa tu akipewa madawa miezi mitatu. Gharama kubwa ilikuja kwetu. Akarudi amekuwa tia maji tia maji kama gari la mkaa trip moja shamba nyingine gereji.
Ila bado mbishi sana, bado anataka atibiwe na kupelekwa hosp za gharama, sasa mzee si atatuacha watoto wake tumefilisika halafu ndo afe? Hapo tutakuwa tumefanya nini? Nahitaji ushauri wenu kwa kweli hili jambo limenifika hatua nimechoka sana. Sipendi unafiki... hii hali ni ngumu sana maana sasa hata ukiona simu toka kwa ndugu unashindwa kupokea maana huchelewi kuambiwa sasa tuchangie kila mtu atoe 700,000 kuna vipimo na matibabu flani tena yanatakiwa.