Gharama za kuendesha Serikali ya Muungano

josam

JF-Expert Member
Nov 22, 2011
2,241
1,031
Ndg Wanajamvi,
Watetezi na waumini wa serikali 2 wanasema kuwa na serikali tatu kutaongeza gharama na Serikali ya Muungano haitakuwa na mapato hivyo Muungano kufa. Maswali ya kujiuliza;
1. Muungano wa serikali mbili uliopo sasa una gharama kiasi gani na nani anaugharimia?

2. Serikali ya Muungano inaendeshwa kwa mapato gani (taja vyanzo vikuu vya mapato 10)
3. Mapato yatokanayo na rasilimali za ndani yanatolewa na Nchi gani / zipi?
4. Je,Serikali ya Muungano inaendeshwa na Zanzibar na mikopo kutoka wafadhili kwani Tanganyika ambayo nayo ingechangia ilikufa?
5. Kwa vile huwezi kusema kuwa jambo lile ni ghari kuliko jingine bila kuwa na mlinganisho wa kimahesabu, je, watetezi wa serikali 2 wamefanya tathimini ya kuendesha serikali tatu na kuona kuwa ni ghari kuliko?
6. Kama jibu la swali la 5 hapo juu ni ndiyo, weka hapa mlinganisho wa gharama hizo kwa kuzingatia majawabu ya maswali no. 2, 3 na 4 hapo juu.

Binafsi sina majibu sahihi ya maswari hayo hapo juu zaidi ya kuhisi na sitaki kuendelea kuishi bila kuwa na majibu sahihi. Watetezi na waumini wa serikali 2 weka majibu hapa.

Note: Kinachotakiwa hapa ni ukweli utakao dhihilishwa kwa mahesabu yatakayokuwa yamejibu maswali tajwa hapo juu na lazima yawe majibu yaliyofanyiwa tafiti na yeyote atakaye yasoma aone kuna ukweli ndani yake. SIYO siasa.

Asante,
Josam
 
wao wanaotaka tatu wanasema kutakuwa na ya tanganyika na ya zanzibar na ya muungano,
sasa wanataka hii ya muungano iwe inachangiwa na tanganyika na zenji,
kuna mtu akasema watafikiria vyanzo vingine, sasa sijuk ni vyanzo vipi ambavyo havitatoka either bara au kisiwani,
labda watakopa imf, mfano wakikopa nje alafu nchi washirika wakagoma kulipa, hapo patanoga.
watakuja ikoloni tanganyika yao ambayo itakuwa present kama walivoiacha, hadi madeni yatimie
 
..serikali ya muungano inaweza kuchangiwa na nchi washirika.

..serikali hiyo ndiyo itakayokuwa na jukumu la ulinzi, sasa ukizingatia kwamba suala la ulinzi ni muhimu, then nchi washirika lazima zichangie. hivyo hivyo kwa huduma na masuala mengine ambayo serikali ya muungano itakuwa inashughulika nayo.

..nchi washirika zinapogoma kuchangia suala fulani, maana yake zimeamua zenyewe kushughulika na suala hilo. kwa mfano, Tanganyika ikiamua kukataa kuchangia suala la polisi, basi maana yake itakuwa imeamua kuwa na jeshi lake la polisi.

..uelewe kwamba hiyo serikali ya muungano itakuwa na watendaji toka nchi washirika. kwa msingi huo inapokwenda kukopa itakuwa imefanya hivyo kwa baraka za nchi washirika. pia ktk dunia ya leo siyo rahisi serikali ikope mahali halafu ikatae kulipa.

..hata hii serikali tuliyonayo sasa hivi inachangiwa na nchi washirika kwa kupitia kodi zinazokusanywa na TRA.

NB:

..usifikiri kwamba muungano wa serikali 2 hauwezi kuvunjika kutokana na mgogoro wa michango ya nchi washirika.

..leo hii Zanzibar inaweza kuamua kujitoa ktk BOT[benki kuu] kutokana na ufisadi[epa, import support,..] unaofanywa na upande wa Tanzania Bara.

..pia Zanzibar inaweza ikagoma TRA wasikusanye mapato Zanzibar kwasababu hawapati mgao stahiki kutokana na makusanyo hayo.

..serikali ya muungano itakuwa salama kama tu ita-DELIVER. hata tukiamua kuwa na serikali 1 as long as tumeungana nchi 2 basi kuna uwezekano wa muungano kuvunjika ikiwa upande mmoja utaona serikali ya muungano "haidelivi."

cc Mchambuzi, takashi, GHIBUU, Mzee Mwanakijiji, Mdondoaji
 
Last edited by a moderator:
Ni kanuni gani ya kuchangia itakayokubalika na kuonekana sawa; 50/50, 60/40, 80/20 kwa Tanganyika/Zanzibar?

..kwa hapo sina jibu.

..lakini at some point lazima nchi washirika zitafute formula ya kuchangia au kugawana kutegemea kama serikali ya shirikisho inachangiwa au inakusanya mapato na kuwagawia washirika.

cc Mchambuzi
 
Last edited by a moderator:
Jokakuu mkuu sikiliza and reason, usifate upepo.
Serikali tatu hazitafunction,
Ccm hawafai sawa, lkn serikali tatu si suluhisho
 
Tra mbona nasikia haifanyi kazi zanzibar,
Walishaikataa,
Tena wazenji wala hawataki serikali tatu wengi wao wanataka nchi yao
 
Serikali 3 haitafutwi kwasababu itakua nafuu kiuchumi, ila kwasababu ni matakwa ya wananchi wanzbr.
Nchi zote zimekua huru kwa lengo tu la kujitawala. Pengine kiuchumi ingefaa zaidi kubak na waingereza/waOman.
serikali 3 ilikua ni busara ya ku_harmonize kundi kubwa la wasiotaka muungano. Haikua suala la kubalance kati ya 2 na 3.
Uhuru una gharama

tragedy of the commons
 
Maswali hayajibiki???! Muungano wetu huu....mmh!
 
gharama hazitakuwa kubwa,chukua wizara zinazohusika na masuala ya muungano,zinafahamika,weka pembeni,chukua ambazo si za muungano,weka pembeni na umpe pinda azisimamie,kwa bajeti ileile mambo yanakwenda,hata leo tukiamua,wizara ya ulinzi,mambo ya nje,fedha,mambo ya ndani,very simple japo lukuvi na wasira hawaelewi
 
maswali meeengi......Ngoja na mie niulize
1. Kwa mfumo tulionao sasa wa Muungano nani analipia gharama za muungano?au hauna gharama?
2. Tanganyika inanufaika na huu muungano?(ukitengeneza balance sheet ya gharama za huu muungano na faida zake...inalipa?)
3. Kama tunapenda sana Muungano na hatutaki kuingia gharama 'kubwa' kwanini tusiwe na serikali MOJA tu?
 
Hatutaki kurudi utumwani lipumba anataka kurudi utumwani kwasababu tu asili yao utumwa wanyamwezi walikuwa watumwa enzi ya tanganyika
 
Sidhani kama wa-Tanzania tutakuwa wajinga kiasi gani kufikia hatua ya kufikiria vyanzo vingine vya mapato kwa ajili ya wanasiasa (Serikali tatu) badala ya kufikiria jinsi ya kutatua kero za huduma za kijamii zinazosababishwa na upungufu katika bajeti. Na sote tunafahamu kwamba bado bajeti yetu ya sasa bado ni tegemezi. Still watu wanakaa bungeni kuleta ujinga wa kuongeza mzigo kwa Watanzania. Hii haikubaliki hata kidogo! siku zote nakumbuka kauli ya Mh Ben Mkapa kwamba prof. Lipumba ni prof uchwara, na hii inaprove ukweli huo.
 
Umesoma na kuelewa ukubwa wa serikali ya Muungano inayopendekezwa kwenye rasimu ya 2 ya Katiba? Umeona itakuwa na mambo mangapi ya pamoja (mUungano) ya kushughulikia? Itakuwa na wizara ngapi? Itakuwa na Mawaziri na manaibu waziri wasiozidi 15! Hii serikali ya Muuungano tuliyonayo sasa ina baraza la mawaziri wangapi? Ipi kubwa kati ya hii tuliyonayo au inayopendekezwa?

Gharama unazozungumzia ni zipi? Mara ngapi wananchi tunalalamikia ukubwa wa serikali? Matumizi ya hovyo yasiyoendana na mahitaji yetu au vipaumbele vyetu? Serikali ina mashangingi mangapi nchi nzima ukianzia kwa Mkuu wa Police (W)? Bajeti ni wewe unavyoamua kutumia.

Mfano Serikali ya Tanganyika inaweza ikawa na baraza la mawaziri wasiozidi 15 hivyo baraza la mawaziri wa serikali ya Muungano (Tanzania) na serikali ya Tanganyika kuwa ndogo kuliko serikali moja ya Muungano tuliyo nayo kwa sasa!!!! Vipi nyie.... hamjitambui au una mnachokitetea, mnacho nufaika nachoooooo????????
 
..serikali ya muungano inaweza kuchangiwa na nchi washirika.

..serikali hiyo ndiyo itakayokuwa na jukumu la ulinzi, sasa ukizingatia kwamba suala la ulinzi ni muhimu, then nchi washirika lazima zichangie. hivyo hivyo kwa huduma na masuala mengine ambayo serikali ya muungano itakuwa inashughulika nayo.

..nchi washirika zinapogoma kuchangia suala fulani, maana yake zimeamua zenyewe kushughulika na suala hilo. kwa mfano, Tanganyika ikiamua kukataa kuchangia suala la polisi, basi maana yake itakuwa imeamua kuwa na jeshi lake la polisi.

..uelewe kwamba hiyo serikali ya muungano itakuwa na watendaji toka nchi washirika. kwa msingi huo inapokwenda kukopa itakuwa imefanya hivyo kwa baraka za nchi washirika. pia ktk dunia ya leo siyo rahisi serikali ikope mahali halafu ikatae kulipa.

..hata hii serikali tuliyonayo sasa hivi inachangiwa na nchi washirika kwa kupitia kodi zinazokusanywa na TRA.

NB:

..usifikiri kwamba muungano wa serikali 2 hauwezi kuvunjika kutokana na mgogoro wa michango ya nchi washirika.

..leo hii Zanzibar inaweza kuamua kujitoa ktk BOT[benki kuu] kutokana na ufisadi[epa, import support,..] unaofanywa na upande wa Tanzania Bara.

..pia Zanzibar inaweza ikagoma TRA wasikusanye mapato Zanzibar kwasababu hawapati mgao stahiki kutokana na makusanyo hayo.

..serikali ya muungano itakuwa salama kama tu ita-DELIVER. hata tukiamua kuwa na serikali 1 as long as tumeungana nchi 2 basi kuna uwezekano wa muungano kuvunjika ikiwa upande mmoja utaona serikali ya muungano "haidelivi."

cc Mchambuzi, takashi, GHIBUU, Mzee Mwanakijiji, Mdondoaji

Nadhani kama watu walikua wanafuatilia vizuri Bunge Maalum La Katiba , wasiwasi wa kuwa serikali ya Muungano itachangiwa vipi katika mfumo wa shirikisho ? Majibu mazuri tu, na yakuridhisha yametolewa na wana wa UKAWA.
 
Back
Top Bottom