LUS0MYA
JF-Expert Member
- Aug 4, 2011
- 862
- 1,097
Mheshimiwa waziri atambue kuwa mita ya umeme, waya, na nguzo ni mali ya Tanesco na ndiyo capital asset yake, ili TANESCO isambaze umeme lazima iwe na hivyo vitu vinginevyo hakuna usambazaji unaofanyika.
Kimsingi jukumu la mtumiaji umeme ni kulipa bili ya umeme anaoutumia. TANESCO wamezoea vibaya kwa kusaidiwa na mtumiaji umeme kujenga miundombinu yake ambayo siyo kazi ya mtumiaji umeme. Kama hawana fedha Wakakope benki waweke miundombinu ya kutosha kwa watu na warejeshe hiyo mikopo baada ya kuuza umeme.
Kutokana na TANESCO kusaidiwa hii gharama wamebuni mipango ya hovyo ya kutumia fedha kama ile ya kumchukua mkandarasi kutoka India kwa ajili ya kupima performance ya utendaji kazi. Ningeshauri pia mtumiaji anayelipa hela ya kufungiwa umeme arudishiwe hata kwa njia ya unit zenyewe za umeme.
Mfano kama nimelipia laki nne kuweka mita basi luku yangu ifungwe ikiwa tayari na unit za umeme za kiwango hicho cha fedha.