Gesi Asilia Iliyoshindiliwa (CNG) Ndiyo Mwarobaini wa Bei ya Mafuta Tanzania

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,333
8,251
images.jpeg-126.jpg

Tanza ikadiriwa kuwa na mita trilioni 230 za ujazo za gesi asilia, ingawa zilizothibitishwa mpaka sasa ni futi trilioni 57.5, hivyo kuiweka kwenye ramani ya dunia ikishika nafasi ya 82.

Gesi hiyo tayari imeanza kuzalishwa katika visiwa vya Songosongo wilayani Kilwa, mkoani Lindi na eneo la Msimbati mkoani Mtwara, ikitumika kuzalisha umeme na kuendesha mitambo ya baadhi ya viwanda nchini.

Pamoja na wingi wa hazina ya gesi hii muhimu, kwa kiasi kikubwa Tanzania bado inategemea mafuta kuendesha mitambo ya viwanda vyake pamoja na magari ya mizigo na abiria na pia baadhi ya majenereta ya kuzalisha umeme unaosambazwa na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

Uhalisia wa hali ukiwa hivyo, Shirika la Petroli Tanzania (TPDC) kwa upande wake lina mkakati wa kuanzisha vituo vya kujaza gesi kwenye magari yaliyoongezewa mfumo unaotumia gesi.

Bei ya mafuta imeathiriwa sana na vita vya Russia na Ukraine vinavyoendelea. Mafuta yalipanda bei na jinsi yalivyopanda, bidhaa nazo zilipanda bei na nauli zilipanda. Thamani ya vitu vingi ilionekana kupanda bei kwa sababu mafuta yalipanda.

Hivyo gesi hiyo ndiyo suluhisho la tatizo la mafuta nchini. Kwa wastani kg 1 ya CNG inakufikisha km 15 wakati lita 1 ya petroli inakufikisha km 10. Lakini pia unaokoa 33.5% ya gharama unapotumia CNG hata kama bei ya CNG ni sawa na ya petroli.

Screenshot_20221013_082537.jpg

Julai 2020, TPDC, ilisema Sh28 bilioni zilitengwa kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya kujaza gesi kwenye magari. Vituo vya CNG vinatarajiwa kujengwa katika kituo cha mabasi yaendayo haraka kilichopo Ubungo, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na pembezoni mwa Barabara ya Sam Nujoma na vituo vidogo vya kupokelea na kusambaza gesi asilia vingejengwa Soko la Samaki Feri, Hospitali ya Taifa Muhimbili na katika kiwanda cha dawa cha Kampuni ya Kairuki Pharmaceutical kilichopo Zegeleni mjini Kibaha.

Hivyo kutokana na hilo, uelewa wa umma juu ya matumizi ya gesi asilia unapaswa kuongezwa ili kuikomboa nchi kutokana na matatizo ya kupanda kwa bei ya mafuta duniani.

Na hilo ndilo ninalolifanya sasa kuhakikisha Tanzania inaelewa umuhimu wa kutumia gesi asilia iliyoshindiliwa kama nishati kwenye magari kwa kuendelea kuandika makala kwenye mitandao ya kijamii.

Hivyo kubadilisha magari ya Tanzania ili yatumie vyanzo mbalimbali vya nishati imekuwa ikiongezeka kila siku. Watanzania wengi zaidi wabadilishe magari yao yatumie gesi asilia ili wanufaike na maliasili nono zinazopatikana katika taifa letu.

Screenshot_20221013_082611.jpg
Screenshot_20221013_082711.jpg
Screenshot_20221013_082643.jpg

Ngoja nikupe mifano ya hesabu inayoeleza faida za kutumia mfumo wa gesi kwenye gari yako na jinsi unavyo okoa fedha nyingi:

1. Ukijaza gesi ya Tsh. 17,000 unaweza kusafiri kilomita zaidi ya 200.
Tsh. 17000 = Km. 200
? = Km. 1
Km. 1 = Tsh. 17000/200 = Tsh. 85

Kikawaida ukijaza lita moja ya petroli unaweza kusafiri kilomita 10 hadi 12. Chukulia lita moja ya petroli ni Tsh. 2886
Tsh. 2886 = Km. 12
? = Km. 1
Km 1 = Tsh. 2886/12 = Tsh. 240.5

Sasa ukitumia gesi kwenye gari yako kwa kila kilometa 1 unaokoa Tsh. ngapi?

Unaokoa = Tsh. 240.5 - Tsh. 85 = Tsh 155.5

Kumbe kwa kila Km. 1 unaokoa Tsh. 155.5

Gharama za kuiongezea mfumo wa gesi gari yako ni Tsh. 1,800,000. Tunazibadili hizi kwenda kwenye Km.

Km 1 = Tsh. 85
? = Tsh 1800,000
Tsh 1800, 000 = Km. 21176.5

Unataka tujue katika Km. hizo tunaokoa Tsh. ngapi?

Km. 1 = unaokoa Tsh. 155.5
Km. 21176.5 = ?

Unaokoa = Tsh. 21176.5 × 155.5 = Tsh. 3,292,941

Sasa unaweza kuona ukiongeza mfumo wa gesi unatumia Tsh. 1,800,000 ambazo zinakuwezesha kutembea Km. 21176.5 kama ukizitumia kununulia gesi. Sasa ukitembea Km. 21176.5 hizo kwa kutumia gesi utaokoa Tsh 3,292,941. Kumbe gharama uliyotumia kubadilisha gari yako itumie gesi itarudi ukisha tembea Km. 21176.5 na faida juu.

2. Kuongeza mfumo wa kutumia gesi kwenye gari inayotumia mafuta inagharimu Tsh. 1,800,000. Gharama hii ni kwa gari zenye cc 400-2000. Na kutakua na ongezeko la Tsh. 80,000 endapo kama spark plugs hazitaruhusu mfumo huo.

3. Ukisafiri kwa kutumia Tsh. 100,000 za mafuta ukitumia gesi utatumia Tsh. 40,000 tu. Umeokoa Tsh. 60,000.

4. Ukiweka mafuta ya Tsh. 45,000, kwa mwezi utatumia Tsh. 1,350,000. Kwa miezi miwili ni Tsh. 2,700,000.
Gesi unaweka ya Tsh. 17,000 na unatumia siku 2 mpaka 3. Inamaana unaongeza gesi kila baada ya siku 2 or 3.
Kama kila baada ya siku 2 unaongeza gesi mara 15 kwa mwezi (Tsh. 17,000 × 15 = Tsh. 255,000). Kwa miezi mwili hii ni Tsh. 510,000.
Gharama za kuongeza mfumo wa gesi ni 1, 800,000 + gesi ya miezi miwili ni Tsh. 510,000 jumla ni Tsh. 2,300,000.

Hivyo ukichukua gharama za mafuta kwa miezi miwili Tsh. 2,700,000 ukatoa gharama ya kufunga mfumo wa gesi na matumizi ya miezi mwili ya Tsh. 2,300,000 unabakia na Tsh. 400,000.

Kwa hiyo kwa mfano huu faida unaanza kuiona baada ya miezi miwili. Kuanzia mwezi wa tatu badala ya kutumia Tsh.1,300,000 kwa mafuta anatumia Tsh.255,000.

Hivyo unaweza kuona jinsi unavyo okoa fedha nyingi ukiongezea mfumo wa gesi kwenye gari yako inayotumia mafuta.

Kwa ushauri zaidi na ukitaka kuibadilisha gari yako itumie mfumo wa gesi piga namba hii +255747744895/+255687746471


Kama unahitaji msaada wa kuandika na kuhariri documents zako mbalimbali, tunayo habari njema kwako!

Bright and Genius Editors wapo hapa kukusaidia.
Tunatoa huduma za uandishi na uhariri wa documents za aina zote.

Wasiliana nasi kwa njia yoyote upendayo:

Piga/WhatsApp : +255687746471/+255612607426
WeChat ID: bandg_editors
Barua pepe: bandg.editors@gmail.com/submit@bgeditors.com/contact@bgeditors.com

Pia, unaweza kutembelea tovuti yetu www.bgeditors.com, Bright & Genius Editors kujifunza zaidi kuhusu huduma zetu na kufanya maombi yako moja kwa moja kutoka kwenye tovuti yetu.
 
Kwanini bei ya gesi ilinganishwe na bei ya petroli wakati gesi hii inazalishwa hapa nchini, kusafirishwa kwa bomba (letu), au tayari Serikali imeshaingiza matozo ya REA, TBS, Railway Levy n.k, kwenye mfumo wa bei ya gesi??
Gesi asilia inauzwa kwa bei ndogo kuliko petrol kwasababu inazalishwa hapahapa nchini. Hiki ndicho nachokijua.
 
Elimu inatolewa kwa njia nyingi ila inahitaji gharama na Serikali haitaki kuingia gharama hizo au ni wavivu wa kufikiri hatua chache mbele.

Advertising ndio mpango mzima na bila kuitangaza biashara au kitu chochote kwenye magazeti, TV na hata Radio hapo tunadsnganyana tu
 
Dunia nzima sijawai ona gari ya gas ila naona gari ya umeme na
Mafundi wa bongo wanaobadilisha gari ya mafuta kitumia mfumo wa gas wengi ni matapeli na wanaharibu na kupunguza uwezo wa gari.
 
Back
Top Bottom