Labani og
JF-Expert Member
- Sep 15, 2020
- 15,774
- 24,209
Simon Patrick (Mwanasheria wa klabu ya Yanga SC)
Hongereni sana @taifastars_ , binafsi siwadai, matokeo haya ndio kipimo chetu cha uwekezaji wetu kwenye soka.
Kwa maslahi mapana ya Taifa, nipende kushauri yafuatayo;
1. Tuziunganishe TFF & ZFF na tuwe na ligi moja bora yenye timu kutoka bara na Zanzibar.
2. Serikali itoe ruzuku kwa timu za vijana kama inavyofanya kwa vyama vya siasa.
3. Serikali ifute kodi na michango isiyo na tija kwa timu za mpira mfano NSSF, WCF, SDL, etc haina tija kwa wachezaji bali huongeza mzigo kwa vilabu, ianzishe kodi maalam ya zuio (WHT) kwa ajili ya wachezaji.
4. Hela zetu za FIFA za maendeleo ya mpira wa miguu zielekezwe kwenye kurekebisha miundombinu ya viwanja hasahasa sehemu ya kuchezea (pitch) ili ligi iwe na ubora zaidi.
5. TFF ianzishe mashindano ya vijana ya kitaifa nje na vilabu na yafanyike kila mwaka sambamba na kurudisha mashindano ya mashuleni.
6. Serikali ianzishe scholarship maalum kwa wanafunzi wote wenye vipaji na kuwataftia akademi nje.
7. Kwakuwa AFCON ya 2027 tunaandaa wenyewe hivo hatutakua na presha ya kufudhu, tuandae timu ya taifa kuanzia leo.
Je ni ushauri Gani unaona ni konk??
#daimambelenyumamwiko
Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app