Gen. Mrisho Sarakikya aliwahi kuhusishwa na Uhaini?

Kichuguu,' The simple answer is no. Ukijua fungu ambalo Tanzania ilitumia katika ukombozi wa Afrika utazimia. Na kama harakati za ukombozi zingekuwa zinafanyika leo Tanzania tungekuwa bubu kama Kenya ilivyokuwa enzi hizo.
Tanzania si nchi masikini kama tunavyodhania. Hata Zambia kuna wakati walikuwa wanaishiwa hela wanakimbilia Dar.

Tuliskwanda mtaji?
 
After reading Kudi Shauri and realize that Captain Nkya (I presume ni Ibrahim Nkya) was one of the people who were "re-assigned" it makes me wonder if trully there was conspiracy or it was Mwalimu moving a bishop ahead ot time to send a message to any thoughts of overthrowing the government.

It is very possible there was something small and never serious but he had to confrot Sarakikya and gave him Uwaziri.

As far I know, Captain Ibrahim Nkya, became one of Mwalimu's aides(bodyguard, ADC or whatever) and travelled with Mwalimu even after Mwalimu's retirement.

Captain Mushi used to have a house around Ilboru area and worked for some company in Arusha and Major Ndosi, became a business man, a hunter and was married to Mary Kejo-Ndosi the attorney behind IPTL.

Nadhani captain Mushi alikuwa meneja wa kiwanda fulani cha mbao kule Arusha; ama Tembo Chipboards au TWICO.

Inawezekana kabisa jaribio lilikuwa dogo sana au lilikuwa katika hatua za mwanzo mwanzo sana na halikuwa credible; ndiyo maana mashushushu wa Nyerere wa wakati huo hawakuwa wamelitilia uzito wowote. Ila kama alivyosema Kudi Shauri hapo juu, Nyerere hakutaka kuchukua chances ndiyo maana akawa mkali kwa Sarakikya ingawa alijuwa wazi kuwa Sarakikya mwenyewe hakuwa amehusika. maofisa wengi waliotolewa jeshini wakati ule walipewa madaraka mengine tena mazuri zaidi ya yale waliyokuwa nayo jeshini. Kama kweli wangekuwa wana hatia Nyerere asingeshindwa kuwapeleka "kunakohusika ili wakasaidie upelelezi."
 
Mkuu ni kweli wale wanajeshi wenye asili ya kaskazini walioondolewa Jeshini wakati ule,wengi walipewa kazi serikalini na kwenye mashirika ya Umma.Captain Ibrahim Nkya alipelekwa ofisi ya Rais kama msaidizi wa Mwalimu,Alifanya kazi na Alhaj Mwinyi, Mkapa na baadaye alirudishwa Foreign kwa kazi maalumu.Kwa wale wenye kumbukumbu nzuri watamkumbuka Capt.Ibrahim wakati wa mazishi ya Mwalimu,kwani Nkya na Kikwete ndio walikuwa watu wa Protocal kwenye Msiba ule.Kwa hivi sasa Nkya ndio Mnunuzi wa Nyumba za Balozi zetu huko Ng'ambo,yupo Foreign lakini hakuna anayejua kwa dhati ana wadhifa gani hapo,aliletwa Foreign akitokea State House enzi za Mzee Mkapa baada ya kukataa appointment ya Ubalozi Msumbiji.

Captain Mushi aliwahi kuwa Meneja wa Tembo Chipboards na Mjumbe kwenye Board ya wakurugenzi wa Twico na hivi sasa anaishi Chang'ombe Maduka Mawili.

Lt. Ndosi alikwishafariki dunia ndio alikuwa mume wa Mama Maria Kejo,lakini walikwishatengana kabla ya kufariki.
 
vere interesting indeed.....
what i dont understand, huyu alikuwa kwenye kesi ya uhaini, lakini je, hajawahi kuwa bodyguard wa Nyerere?

''William Chacha, a former colonel in the TPDF, until recently military attaché in the Tanzanian embassy in Peking''
 
Nzoka,
The simple answer is no. Hakuwahi kuwa bodyguard wa Nyerere.
 
michango ni mizuri sana katika thread hii, naungana na rev.kishoka na wengine kumwomba mkuu mwanakijiji ahojiane na sarakikya kupata ukweli. jitahidi mapema kwa kuwa wazee wetu hawa saa zao kama mmoja wetu alivyoandika hapa zinakaribia magharibi

ingawa si kigezo sana, kwani hata viijana nao ndo mtindo mmoja
 
..kwa kweli Mwinyi hakukosea katika kumshughulikia Mrema.

Aliyemfukuza Mrema alikuwa ni the then Waziri Mkuu Msuya, ambaye alilaaaniwa sana kwenye kikao kilichofuatia cha CC na ni hoja hii ya kumfukuza Mrema ndio iliyopelekea kupitishwa kwa Mkapa,

Msuya alipokuwa anamfukuza Mrema, alidhani anajipalilia njia ya kuwa rais 1995, little he knew kuwa alikua anajinasa kwenye mtego ulkiowekwa tayari wa njia ya Mkapa kuwa the next president, na kwamba Mream was getting a bck up kutoka kwenye a strong hand,

Ni kwenye hicho kikao ndio Msuya akagundua the deal baada ya kushambuliwa sana, wakati yeye alidhani atasifiwa sana, and he cried very hard baada ya kikao.
 
Kwa hivi sasa Nkya ndio Mnunuzi wa Nyumba za Balozi zetu huko Ng'ambo,yupo Foreign lakini hakuna anayejua kwa dhati ana wadhifa gani hapo,aliletwa Foreign akitokea State House enzi za Mzee Mkapa baada ya kukataa appointment ya Ubalozi Msumbiji.

Yaaani haya mambo yapo mpaka leo bado ya mtu kuwepo serikalini na ikulu lakini hajulikani anafanya nini? Halafu baadye akitangulia kwenye haki tutaanza kuvutana mashati kuwa alikuwa hakuwa! damn!
 
FMES,Jasusi,Kichuguu,Mwawado,Kudi Shauri,Zanaki,Ether,....

..nimesikia sana kwamba Cleopa Msuya ni kati ya matajiri wakubwa Tanzania.

..ningependa kujua huyu Mzee by estimation ana worth how much.

..ni biashara gani anafanya? anamiliki assets zipi?
 
jokaKuu,
Na mimi hizo rumours nimezisikia siku nyingi. Pia nilisikia ule wakati wa kuhujumu uchumi Sokoine alikuwa amepanga kufanya msako nyumbani kwa Msuya na Msuya akampigia simu Mwalimu akisema kuwa kama waziri wa serikali hawezi kufanyiwa ukaguzi nyumbani kwake na Mwalimu akamsimamisha Sokoine. Kama nilivyosema hizo ni rumours tu sikuwepo nyumbani wakati huo labda wenye data zaidi hapa JF wanaweza kutuhabarisha.
 
Jasusi said:

Jasusi,

..Thank you, ingawa hujanipa jibu bado.

..hii habari ya Msuya na Sokoine tulishaisikia sana, na nadhani inaweza ikatupotezea muelekeo.

..i am reposting my questions:

..nimesikia sana kwamba Cleopa Msuya ni kati ya matajiri wakubwa Tanzania.

..ningependa kujua huyu Mzee by estimation ana worth how much.

..ni biashara gani anafanya? anamiliki assets zipi?
 
..nimesikia sana kwamba Cleopa Msuya ni kati ya matajiri wakubwa Tanzania.

1. Binafsi ninaamini kwamba Msuya, alikuwa na free access kwenye hazina yetu kwa excuse ya ruzuku kwa CCM,

2. Miaka yake yote in power, ali-steer hela nyingi na maendeleo mengi sana kwenda jimbo lake la Mwanga kwa mgongo wa taifa.

3. Kwamba ni tajiri mkubwa sana, sina uhakika sana kwa sababu yeye sio mtu wa kujionyesha wala huwa haongei sana, kwa hiyo you have to be mke au watoto wake kujua hilo, mtu yoyote mwingine nje ya hao akisema ni anakuwa sio mkweli,

- ila ninajua one thing, nacho ni kwamba he is very good kwenye kutumia mafao yake ya u-Waziri Mkuu, kuna marupu rupu mengi sana kwenye package ambayo wastaafu wengine hwua hawayafuatilii sana, lakini sio yeye,

-kwa mfano, magari mawili SUV kubadilishiwa mapya kila mwaka, ukarabati nyumba anamoishi mara moja kwa mwaka, yaani Dar na Dodoma na the rst of story.
 
FMES,Jasusi,Kichuguu,Mwawado,Kudi Shauri,Zanaki,Ether,....

..nimesikia sana kwamba Cleopa Msuya ni kati ya matajiri wakubwa Tanzania.

..ningependa kujua huyu Mzee by estimation ana worth how much.

..ni biashara gani anafanya? anamiliki assets zipi?

Kwa vile mimi pia uliniuliza, ngoja nitoe jibu langu.

Msuya ni waziri pekee aliyewahi kuendesha wizara nyeti tu katika kipindi chote alichokuwa mwanasiasa: ama Wizara ya Fedha, au Biashara na Viwanda au Waziri Mkuu. Nilipokuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kuna wakati room mate wangu alikuwa ndugu yake Msuya, na hiyo ni wakati wa Nyerere. Huyu mtu aliwahi kunidokeza kuwa Msuya alikuwa anaishi maisha ya aibu sana nyumbani kwake ingawa alikuwa anaisadidia sana wilaya yake kwa vile alikuwa ni maskini sana. Ila jambo lllokuwa wazi wakati ule ni kwamba kuna baadhi ya ndugu zake msuya walikuwa wananeemeka kwa haraka haraka sana kiasi kuwa walikuwa wanatisha. Vile vile kuna taarifa kuwa mojawapo ya viwanda vya Cocacola vilivyofunguliwa nchini kati ya mwaka 1985 na 1990 kilikuwa na mkono wake kwa vile Cocacola International ilitumia nguvu ya serikali ili kukamata soko la kwetu tena baada ya kuwa wamepigwa mwereka na Pepsi wakati huo. Matokeo yake, aliyekuwa Gavana wa benki kuu wakati huo alipata kipande chake cha Cocacola na aliyewa Waziri wa fedha nae akapata kipande chake cha Cocacola ili Cocacola irudi tena nchini. Aliyekuwa Waziri wa fedha wakati huo ni Msuya na aliyekuwa Gavana wa benki kuu ni Nyirabu.

Hata hivyo sijui kama kweli Msuya ni tajiri kiasi hicho ingawa sijawahi kufika kwake wala sijui account yake ya benki ina makaratasi kisai gani.
 
Kama kuna mawaziri "waliokula" vizuri ni Msuya.

Sina maana ya kusogeza hazina kwa kuhujumu au ufisadi, bali ni kwa kuleta maendeleo katika wilaya aliyotoka.

Inawezekana ni kupeleka miradi ya maendeleo kwa kutumia mgawanyo wa mapato au ni uhamasishaji, lakini wilaya ya Mwanga imekuwa ikipiga hatua za maendeleo yanayowiana kwa muda mrefu sasa.

Sasa ukija jirani zao Same ambako alikuwepo Chediel Mgonja na Daniel Yona, sijui ni maendeleo makubwa kiasi gani ya kuweza kuwiana au kushindana na jirani zao wa Mwanga!

Sijui kama ana utajiri wake binafsi wa kutisha zaidi ya alichokivuna kutokana na jasho lake!
 
Rev.Kishoka said:

Rev.Kishoka,

..Chediel Mgonja alikuwa mbunge wa Same[east + west] plus Mwanga, wakati ikiitwa wilaya ya Pare.

..Mgonja alikuwa mhamasishaji mzuri wa kazi za kujitolea kuchimba barabara za milimani.

..juhudi za wananchi zilimvutia sana Mwalimu mpaka kufikia kusifia kwa kutamka kwamba wananchi wa Same ni " Wachina wa Tanzania."
 
Kutokana na uwezo wake wa kuhamasisha, alikuwa pia mhamasishaji sana wa wanawake kwenda nao chumbani; mpaka wake za watu!
 
Kichuguu said:
Mgonja Kutokana na uwezo wake wa kuhamasisha, alikuwa pia mhamasishaji sana wa wanawake kwenda nao chumbani; mpaka wake za watu!

Kichuguu,

..hicho ulichokisema hapo juu was an open secret about Mgonja.

..labda inatokana na kupata madaraka makubwa akiwa kijana mdogo kabisa.

..Mgonja alikuwa ubalozi wa Tanganyika UN mwaka 1962. mwaka 1965 akaacha kazi[foreign service officer] na kwenda kugombea ubunge.

..moja kwa moja akateuliwa kuwa waziri. kama utakumbuka ndiye aliyetoa tamko la kuitambua Biafra mwaka 1967/68.

NB:

..nadhani Mgonja ni kati wa wa-Tanzania vijana kabisa kutumikia kama Cabinet Minister.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom