Gazeti la Tanzania daima

everybody

JF-Expert Member
Oct 30, 2010
337
103
Habari ya Pasaka wana JF?

Kwa muda mrefu sasa hili gazeti la Tanzania daima halipo online na ukifungua website yake inasema under mantainance. Ningependa kujua nikweli kuna matatizo kwenye huo mtandao wao au ndo katika zile harakati za kuyaondoa magazeti yanafichua mambo?
 
Kuna jukwaa lake! Lakini kwa mwongozo kidogo waeza wasiliana na uongozi wa gazeti husika kwa maelezo zaidi
 
Ka gazeti ka chadema hako

Nimeshangazwa sana kusoma kwenye gazeti la Tanzania Daima article yenye kichwa cha habari "Polisi wajitathmini uvamizi wa kumbi". hivi sikuhizi Tanzania Daima mnatafuta kiki hadi sehemu ambayo haihitaji kiki?
Nilitegemea mtawapongeza sana polisi kwa kujali wananchi kuingilia kati ili wananchi wanaotaka kupumzika baada ya saa sita usiku waweze kupata faragha hiyo. Nyinyi bila haya wala soni mnaanza kutetea wapiga bendi ambao wanaleta kero kubwa sana katika mitaa yetu? Hivi sasa mmeishiwa mada sasa mnatafuta habari za kuokoteza? Je umefikiria hata kidogo zatu wangapi wanaadhirika na makelele ya bendi hizo ambazo bila kuingilia kati polisi zangekuwa wanakesha usiku kucha? Hebu Tanzania Daima badilisheni mtizamo wenu sio kila kitu kiwe cha kiuanaharakati wakati mwingine muwe mnafikiria tu cha kuandika na hizo kalamu zenu. Nadhani mwandishi hajawahi kukaa maeneo yetu ya uswazi. Hatua wanazochukua Askari winawafurahisha wananchi walio wengi ambao ni wengi kuliko hao wenye ukumbi. Muda wa kufunga ukumbi siku za kawaida ni saa nne usiku na wikiendi ni saa ssita. sasa wao wanaendelea kukosesha wananchi usingizi mpaka saa saba na kuendelea halafu Mhariri wa Tanzania Daima anathubutu kutetea wenye ukumbi? Shame on you!
 
Back
Top Bottom