Gazeti la Mwananchi lamuangukia Waziri Membe

Sheba

JF-Expert Member
May 14, 2009
211
97
Kumradhi Waziri Membe

Monday, 23 July 2012

Katika gazeti hili la tarehe 12/01/2011 tulichapisha habari yenye kichwa. Membe: Polisi walikiuka Maadili (Mabalozi waibana Serikali, wahoji polisi kutumia risasi za moto).

Habari hiyo ambayo ilifuatia tukio la vifo vya watu watatu na majeruhi kadhaa vilivyotokea mjini Arusha wakati polisi walipokabiliana na waandamanaji wa Chadema, ilidai kwamba Waziri Membe alililaumu jeshi la polisi kwa kukiuka maadili, kuvuka mipaka yake na kusababisha mauaji hayo ambayo yalitia doa Tanzania.

Aidha habari hiyo iliendelea kudai kwamba mabalozi wa nchi mbalimbali walimbana wakitaka tamko la Serikali juu ya tukio hilo.

Baada ya uchunguzi wa kina, gazeti hili limebaini kuwa, Waziri Membe hakusema maneno hayo na wala hapakuwa na mvutano wala madai yeyote ya Mabalozi juu ya jambo hilo.

Kutokana na hayo, tunachukua fursa hii kumwomba radhi Waziri Membe, Jeshi la Polisi, Serikali, Mabalozi wote na Wananchi kwa ujumla.

Aidha tunapenda kumhakikishia Waziri Membe na wasomaji wote kwa ujumla kwamba habari hii iliandikwa kwa bahati mbaya na kwamba gazeti hili litaendelea kufanya kazi yake kwa kufuata misingi ya Taaluma ya uandishi wa habari, Maadili na sheria za nchi bila kumwonea mtu au kushinikizwa na mtu yoyote kwa maslahi binafsi.

Mhariri
 
Katika magazeti yote Tanzania, Mwananchi ndilo gazeti pekee ninaloliamini kwa habari za uhakika za papo kwa papo. Ilikuwaje wakakosea kwa miezi zaidi ya sita iliyopita?
 
Nyie si ndo pia mmeandika POLISI WANAUZA SMG KWA LAKI NNE? Natamani kujua hatma yake, kwani kwa silaha kubwa kama hiyo, mtu kuiiba na kuiuza laki nne, aidha hajui thamani ya bunduki hiyo, au amefanya hivyo kutekeleza matakwa fulani. Naisubiri kwa hamu
 
Katika kuonyesha uungwana gazeti la mwananchi leo limemtaka radhi Mh Membe kwa kuandika habari yenye kupotosha. Bravo Mwananchi!!. Sasa ni zamu ya magazeti uchwara kama Mtanzania kuiga mfano kwa kuomba radhi na kufuta kauli potofu na za uongo dhidi ya Membe kwa lengo la kumchafua. Mtalipuliwa!
 
hata mimi nimeshangaa!

Wanajua walikosea ndo mana wakaomba radhi.
Hawaogopi bali wanafuata sheria na kanuni za uandishi.
On the other side:: wawe makini la sivyo watapoteza heshima waliyojijengea, haki ya mtu haipotei hata siku moja
na kama kun madudu mengine kama hayo one day yatajulkana tu.
 
Kumradhi Waziri Membe

Monday, 23 July 2012

Katika gazeti hili la tarehe 12/01/2011 tulichapisha habari yenye kichwa. Membe: Polisi walikiuka Maadili (Mabalozi waibana Serikali, wahoji polisi kutumia risasi za moto).

Habari hiyo ambayo ilifuatia tukio la vifo vya watu watatu na majeruhi kadhaa vilivyotokea mjini Arusha wakati polisi walipokabiliana na waandamanaji wa Chadema, ilidai kwamba Waziri Membe alililaumu jeshi la polisi kwa kukiuka maadili, kuvuka mipaka yake na kusababisha mauaji hayo ambayo yalitia doa Tanzania.

Aidha habari hiyo iliendelea kudai kwamba mabalozi wa nchi mbalimbali walimbana wakitaka tamko la Serikali juu ya tukio hilo.

Baada ya uchunguzi wa kina, gazeti hili limebaini kuwa, Waziri Membe hakusema maneno hayo na wala hapakuwa na mvutano wala madai yeyote ya Mabalozi juu ya jambo hilo.

Kutokana na hayo, tunachukua fursa hii kumwomba radhi Waziri Membe, Jeshi la Polisi, Serikali, Mabalozi wote na Wananchi kwa ujumla.

Aidha tunapenda kumhakikishia Waziri Membe na wasomaji wote kwa ujumla kwamba habari hii iliandikwa kwa bahati mbaya na kwamba gazeti hili litaendelea kufanya kazi yake kwa kufuata misingi ya Taaluma ya uandishi wa habari, Maadili na sheria za nchi bila kumwonea mtu au kushinikizwa na mtu yoyote kwa maslahi binafsi.

Mhariri

Wametumwa hao, kujua kama membe hakuwasema polisi wala kutokuwepo kwa mvutano kati ya Serikali na Mabalozi inachukua miezi yote hiyo? hapa Gazeti limeuzwa kwa kambi ya Membe!!!!!
 
Inadhihirisha kabisa kwamba magazeti si ya kuaminiwa.Walitumiwa na Cdm au mwandishi ni mnazi wa cdm.Wangekuwa makini wangesema sababu halisi sio kukwepa kwa kusema kuwa ilikuwa bahati mbaya.Haiwezekani siku zote hizo zaidi ya mwaka na nusu ndo wanajitokeza kuomba msamaha
 
Haya magazeti nayo siku hizi si ya kuyaamini sana, maana habari zinazoandikwa nyingi zinatia mashaka.
 
waugwana kivipi wakati wameshikwa shati lazima wakiri kosa kwaajili ya kusafisha Membe,kumbe kunamakorokocho mengi tumepewa na gazeti hili na bila kufanya analysis wengi wetu tumechukulia kama reliable source.
 
Kumradhi Waziri Membe

Monday, 23 July 2012

Katika gazeti hili la tarehe 12/01/2011 tulichapisha habari yenye kichwa. Membe: Polisi walikiuka Maadili (Mabalozi waibana Serikali, wahoji polisi kutumia risasi za moto).

Mhariri

Mbona mmekawia sana kuomba radhi? Au mlikua mnashikilia uamuzi wenu mpaka mliposhindwa mahakamani? haukuna uungwana kama mmeshindwa mahakamani ndio mnaomba radhi. Mwaka na zaidi umepita nyie MWANANCHI ndio mnaomba radhi leo! Mwe!
 
eti habari hii iliandikwa kwa bahati mbaya kwani editor wao kazi yake ni nini? ndio maana mnapelekwaga mahakamani hivi hivi
 
Back
Top Bottom