Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,564
- 7,973
Katika magazeti yote Tanzania, Mwananchi ndilo gazeti pekee ninaloliamini kwa habari za uhakika za papo kwa papo. Ilikuwaje wakakosea kwa miezi zaidi ya sita iliyopita?
Mkuu Kichuguu hii habari iliandikwa 12 January 2011, hadi hii leo wanapokuja kuikanusha ni zaidi ya mwaka mmoja na miezi sita. Hata mimi ninapata wasiwasi kwamba gazeti la mwananchi linaelekea ku compromise na waziri membe ama serikali.
Kumradhi Waziri Membe
Monday, 23 July 2012
Katika gazeti hili la tarehe 12/01/2011 tulichapisha habari yenye kichwa. Membe: Polisi walikiuka Maadili (Mabalozi waibana Serikali, wahoji polisi kutumia risasi za moto).
Au ni katika harakati za waziri membe kujiweka sawa katika kinyang'anyiro cha ukazi wa magogoni! Kwani ni juzi juzi tu amelipuka kwamba kuna watu hatari 11 ambao ni maadui wake na pia ni maadui wa serikali hii dhaifu. Kwahiyo anatafuta kila namna ya kufyeka vichaka vyote vinavyomzunguka ili kujisafishia njia.
Last edited by a moderator: