Gazeti la Mwanahalisi nimekumiss utarudi lini?

mmaroroi

JF-Expert Member
May 8, 2008
2,960
544
Ni muda mrefu sana Gazeti la Mwanahalisi halionekani, wanaJF naomba mnijulishe sakata la Gazeti hili limeishia wapi na tutarajie nini kuhusu hatima yake. Tumeona kuibuka magazeti ya wiki kama hilo yanayoshambulia kinyume na Mwanahalisi kwa maana ya kushambulia uanaharakati badala ya kuiunga mkono. Je inawezekana wenye Magazeti hayo ndio wameshinikiza Mwanahalisi lifungiwe ili magazeti yao yakue? Naombeni ufafanuzi kuhusu hili.
 
Hatuna namna ya kufanya kushikiza Gazeti hili lifunguliwe? Kweli kizuri halidumu. Mods tafadhali muiache mada hii ili ipate wachangiaji wa kutosha.
 
Ukweli tangu mwanahalisi liondolewe mtaani, hamu ya kusoma magazeti imeniishia kabisa
 
kwa kusema kweli mi namshauri Kubenea aanzishe gazeti lingine lenye safu ya wachapakazi walewale aache kuisubiri serikali sikivu ya mkuu wa kaya kulifungulia gazeti. mbona sheraton-royal palm-moving peak inawezekana, iweje Kube ashndwe Mwana halisi-mwana halisia-bwana halisi..........
 
Kufungia mwanahalisi ni harakati ya magamba kudidimiza ukweli na uwazi. This is Neo Dictatorship
 
Back
Top Bottom