Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

Wapelekeni Serikali hii mahakamani, na wakishindwa kesi walipe ghara kali sana. Watakoma kutumia madaraka vibaya.
 
Kuna watu wamezaliwa wana chuki ya asili,wanakuwa na tabia ya husuda,wivu na gubu mioyoni mwao,huwa hawapendi kuona watu wakiishi kwa kupendana na kushikamana.hii haikubaliki.mwanahalisi halikubaliki kwa watu wenye akili timamu,e


Kikwete bwana ana gubu na inda kama amiri jeshi mkuu ametoa amri ya mauaji, ya Dr Ulimboka maofisa wake uchwara waliokosa akili hata ya kuua,mchezo umemefeli watu wanatafiti na kujua ukweli wanatuhabarisha wananchi yeye anafungia gazeti mwambie ajiulize kama kuna dickteta yeyot hapa duniani alibaki salama ataishia kuchomekwa majiti kama Gaddafi rafiki yake kipenzi
 
mkuu naona nzi wanakufuata mdomoni kapige mswaki na huko nyuma pia kuna harufu mbaya inatoka,kajichambe

umekosa hoja unaleta viroja,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, gambaz bhana sijui mna matatizo gani,,,,,,,,,,, pole sana kwa kumteka na kumtesa Dr. ULIMBOKA
 
amna chanzo kingine cha information zaidi ya media,all tanzanians depend on media in geting information.serikali angalieni pande zote
 
serikali inajijengea mazingira magumu kwa wananchi,ikielezwa ukweli inasema magazeti yanachochea vurugu wakati wao wenyewe ndio wanaoleta hizo vurugu
 
unajua mara nyingine jaribu kufiri kabla hujaa andika.
Yeye anasema maovu ambayo ulikuwa huyafahamu sasa hapo pia yeye sio mzuri?


Ndugu mimi nipo pamoja nawe katika mawazo yangu. Kuna mtu alitapika PUMBA ZAKE HAPA ndio maana nikamjibu hivyo.

Ndio maana nikasema:"Anajifanya anajua sana upelelezi sasa si angelienda kuomba kazi Usalama wa Taifa tujue moja kuwa ni mpelelezi.

Kisha upelelezi wake siku zote ni kuivua nguo hadi ya ndani Serikali ya CCM tu, kwanini asipelelezi Majambazi????



Tupo Pamoja



MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
Kubenea ayamwage mavituz yake JF au na HILI watalifungia? Au kama vipi atinge mahakamani....huenda akakutana na jaji muungwana anayezijua sheria na kuzisimamia.
 
Kitendo cha kulifungia gazeti la MwanaHALISI ni cha kusikitisha na kinastahili kulaaniwa na wanademokrasia wote walitakiao mema taifa hili. Lakini wakati huo huo sharti pia tulaani Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976. Kwa maana, bila ya sheria hii, pengine leo hii tusingelikuwa na hali hii.
Kuanzia leo Julai 30, 2012; Gazeti la MwanaHalisi limefungiwa na serikali kwakuwa linadaiwa kuandika habari za uchochezi.

CHANZO: TBC1



Wajameni serikali hii inataka kutufunga mdomo tuendelee kuwa gizani tusijue madudu yao.

Pole sana KUBENEA tupo na wewe habari zako za kiuchunguzi zinatusaidia sana na ndizo zinazotufungua macho tujue nchi yetu inavyoliwa.
 
Kwa kweli nakubaliana na mnyika kwa 101% kuwa serikali yetu ni dhaifu. Mwanahalisi lilitoa taarifa ya alioyemteka dr. ulimboka likiwa na data kamili. Mimi nafikiri kama serikali yetu ingekuwa makini ingekanusha taarifa hii kwa data ambazo zingewaconvice wananchi kuwa alichoandika mwanahalisi si kweli then ndio serikali ingechukua hatua ya kulifungia gazeti. Lakini kwa sasa inaonekana serikali imeshindwa kabisa kila sehemu kumetoboaka sasa linajaribu kuziba matobo yanayovujisha ambayo ndio kulifungia gazeti la mwanahalisi.
 
Akitukanwa Lowassa sawa,wakiguswa wao wanakimbilia kufungia gazeti,kweli mkuki kwa nguruwe!
 
JK awaepuke washauri hawa. Membe pamoja na Sitta. Nakumbuka kabla gazeti la Mwanahalisi halijawa maarufu liliandika habari kuhusu orodha ya Mafisadi. Mhe. Lowasa akiwa ni waziri Mkuu wa wakati huo alimshauri Rais walifungie gazeti hilo, lakini kwa kuzingatia ushauri aliopewa na Waziri wa Mambo ya nje ikaonekana kwamba huu ni wakati wa uhuru wa vyombo vya Habari hatupaswi kunyanyasa vyombo hivyo. Yeye kwa kudanganywa na demokrasia ya uwongo na kweli ya Marekani akakubaliana na wazo hilo. Aidha pia kwa kiasi kikubwa JK alimsikiliza Sitta kuhusu kusomwa kwa taarifa ya Kamati teule ya Richmond ambayo ilipelekea kujiudhuru kwa Mhe. Lowasa.

Makosa haya mawili aliyoyafanya kwenye Utawala wake yatamgarimu sana yeye mwenyewe, familia yake, Chama Chake, Serikali yake na Watanzania wote. Kwani upinzani anaoupata kutoka CDM misingi yake ni kwa yeye kutoa uhuru uliopitiliza kwa kwa vyombo vya Habari na wanasiasa. Kumsiliza Sitta kumesababisha Chama kumeguka na Serikali kutokuwa na muelekeo kutokana na watendaji wengi wa serikali kuwa Pro. Lowasa. Hivyo kwa kulifungia Mwanahalisi kwa Sasa amechelewa sana kwani baada ya gazeti hilo kupata umaarufu kupitia habari hizo magazeti mengi yameiga na wananchi wengi wameshaona yanayosemwa na Mwanahalisi ndio kweli. "Mzarau mwiba humchoma"

Ushauri; ni Serikali ya JK itizame ilipojikwa na sipo inapoenda kuangukia
 
Safi sana gazeti la udaku na majungu na kufitinisha watu hata hivyo serikali imechelewa mno kulifungia.

Nasikia Magamba wanakushika makalio. Ile habari ya Rama Ighonda ndio imesababisha kufungiwa lakini ukweli utabaki kuwa pale pale.
 
Mpumbavu kabisa wewe, yaani kuuwa watu wewe na baba yako ndo mnaona raha eeh. Subirini siku yenu yaja. Hii haina ubishi, utaanza wewe kabla ya mwaka huu kuisha, kisha baba yako kabla ya 2014. Na wengine ambao ni wanafamilia watafuata mfululizo hadi kufikia 2017 kizazi kitakuwa kimekwisha. Najua mwanahalisi iliwakamata pabaya, kama imeandika habari za uchochezi kwa nini lisifunguliwe mashtaka ya jinai mahakamani. danganyaneni wenyewe make ndiyo principal ya familia iliyojaa watu wenye utahira, ujinga lakini zaidi upumbavu make hapo hata kushtuka kwa mwanga wa jua ni kazi.
 
Mwanahalisi waende mahakamani. Ninauhakika Serikali itashindwa kesi, na siri nyingi zitafichuliwa.
 
Kuukimbia ukweli ni kazi sana ndugu zangu tusubiri tu uwezi kuuzuia ukwli hata kidogo. siku zote ukweli utabaki kuwa ukweli na hapa amuwezikutudanganya nyinyi ndio mliomteka na kumdhuru Dr. Ulimboka ili linajidhihirisha dhairi kuwa nyie serikali mliusika. kama ni mchochezi na mnajua anachochea kupotea kwa amani ya nchi yetu kwanini msimkamate na kumfungulia mashitaka?
 
Nimesikitishwa sana na hatua ya serikali kulifungia gazeti la Mwanahalisi kwa kusema ukweli. Tumefikia hatua kwamba wasema uwongo wanaheshimiwa na wakweli wanadidimizwa
 
Hahahaha serikali imekalia kuti kavu,mara waseme chizi sijui kaenda kuungama kwa gwajima sijui blablablaaaa wajipange vizuri
 
Back
Top Bottom