NNasubiri wakianza kuichambua CHADEMA kama karanga waanze kuitwa hawa hawa kuwa si mashujaa
maana ushujaa kwa baadhi ya watu ni kusifia Chadema na viongozi wake na kuitusi serikali na waandamizi wake
ivi wewe unaumwa nin?ujioni kama una matatizo unafikiri humu nisehemu ya kutafuta mabwana
Naomba tafadhari mwenye Gazeti la Mwana halisi ambaye ana uwezo wa kuscan ukurasa wa kwanza na wa pili, hasa ile Document ya Rex Attorneys abandike hapa jamaa zetu wa mikoani wahabarike.Mbarikiwe!!!!!!!mkuu kuna habari gani mkuu, huku mikoani bado halijafika, nitupie headline
Magazeti mengine hawawezi maana wanafuata sera za Maboss. Wewe ulitegemea RAI litazimika kwenye ulingo wa harakati?? Tusiwalaumu maana wanaangalia mkate wa watoto. Waropoke waone kazi itakuwa basi. Kama wanakereketwa wajitoe wajoin media house zingine mbona nyingi siku hizi.Wapeni pole!!!!!!!!!Mtu anapofanya vizuri ni ungwana kumpongeza, Mwanahalisi wanastahili pongezi za dhati. Pamoja nao wapo Raia Mwema na Mwananchi bila kusahau the East Africa ambao ndio walioiweka vizuri article kuhusu Dowans na Rostam Azizi katika toleo lao la Jumatatu hii.
Hiyo habari ipo wazi kwenye hukumu ya ICC inayotutaka tumlipe huyo ponjoli hiyo 94bn/=, lakini magazeti mengine yamekazania personalities za kina Sitta, Mwakyembe vs Lowasa na Rostam badala ya kuzama kwenye hukumu kisha mtu aje na article iliyoenda shule kama hiyo ya East Afrika Jumatatu na Mwanahalisi leo. Raia Mwema ya leo bado sijaiona.
Article ya East Africa na Mwanahalisi katika matoleo yao ya wiki hii kuhusu Rostam na Dowans ni ujumbe tosha kwa magazeti mengine nchini, hususani Tanzania Daima ambalo hivi sasa limejibainisha kuwa kundi moja na kina habari leo, uhuru, mtanzania na raia. WAANDISHI WA HABARI BADILIKENI, jifunzeni kwa wenzenu Mwanahalisi, Raia Mwema, Mwananchi na East Africa
wamefanya kazi yao,pongezi ya nini.Watanzania tunapotea kwa kukosa maarifa kidogo,hiyo ndio kazi ya gazeti magazeti yanatakiwa yaige hapo sasa ukisema pongezi tena maana yake unaondoa uhalisia wa kazi za gazeti.HIYO NI KAZI YAO NA HAWAHITAJI PONGEZI YOYOTE
tuambie ukaribu uliopitiliza kati ya mfanyabiashara-FREEMA MBOWE na mhariri- KUBENEA una maslahi gani kwa jamii yetu.Ndugu zangu wana JF mtu akifanya kazi nzuri anastahili pongezi. Tena ikiwa kazi ya utaalam anapewa award. Hili gazeti la mwana halisi linafanya kazi nzuri kabisa,hata kama ni biashara, maana linafanya watu in certain quarters hawalali.
Hiyo inaitwa investigative journalism ya Bwn Kubenea and company.
Hivyo nawaomba wana JF Hawa vijana tuwatie moyo kwa kazi hii ya kujituma na risk. Kumbuka yeye na Ndg yangu Ndimara waliwahi kumwagiwa tindi kali!!!!!!! Huo sio utani maana yake ilikuwa nia ya wahujumu ni kuwapofusha macho ili wasione waache kuandika. Lakini wanazidi kufukua uozo zaidi na hawana woga wa kutaja mafisadi wahusika moja kwa moja.
Isiwe wanapigana vita ya peke yao kumbe tutafaidi Watanzania wote tukishinda, bila kujali dini kabila wala chama cha siasa. Tuwapongeze tafadhari tubuni mbinu ya kuwatia moyo!!!!!!!!!!!!!!!! (Soma; Mwana Halisi Na.227 Juma Tano Feb 2-8, 2011)
tuambie ukaribu uliopitiliza kati ya mfanyabiashara-FREEMA MBOWE na mhariri- KUBENEA una maslahi gani kwa jamii yetu.
ukinipa jibu la uhakika utaniondolea utata unanikabili.
jiulize huyu mtu ana ugomvi gani na KABWE ZITO..............