Gari yangu ya kwanza nimenunua, Nissan Dualis

Habari wana JF,

Kwa mara ya kwanza kwenye maisha yangu nimenunua na kumiliki gari yangu ya kwanza nissan dualis, kusema ukweli sijui vitu vingu kuhusu magari nafahamu vitu vichache sana.

Naombeni msaada jinsi ya kuitunza hii gari angalau idumu napokea maoni na ushauri jamani, gari nimeipokea juzi tu
Dualis Nyingi ni za Gearbox za CVT
Hizi gear box ni nzuri sana kama utafatisha mashart yake
Ni mbaya sana kama utachukulia poa
Weka oil sahihi hua inaandikwa katika dipstik
Ukichanganya madesa tu unaua gear box fasta
 
Jambo la kwanza kwenye oil ya gear box. Fanya ubahiri wote ila sio hilo eneo. Usije ukaweka brand ya oil nje ya ile ya Nissan au ipo moja ya mobil ila sidhani kama inapatikana sana hapa Bongo. Ukiweka nje ya hiyo utakuja hapa kulia lia kuwa gari hizi ni mbovu kumbe ni wewe unashida.

Oil ya engine pia tumia yenyewe ya Nissan zinajulikana maana zipo za gear box na za engine. Asije akatokea fundi akakuchanganyia hiyo taarifa na kusema oil ni oil unaweza mix HAPANA. Kataaa. Tumia hizo oil za Nissan tuuu.

Gear box ya hiyo gari ni CVT so haitumii gear box oil (hydraulic) nyingine nje ya recommended ambayo ni zake na brand ya mobil. Utakutana na CVT oil (hydraulic) za brand zingine na mafundi wanaweza kushawishi kutia tu kwa sababu yoyote kataaaaaaaaa weka only ya Nissan.

Kingine, zingatia kutunza movements zako. Ni bora upite njia ndefu ya lami ukaingia gharama isiyozidi elfu 5 au 10 ya mafuta kuliko kufosi kupita njia fupi yenye mashimo makubwa na rough ambayo itaweza kukuchakazia gari yako na kuja kununua spare isivyo lazima. Ukiheshimu unapoipitisha ina uimara wa kutokukusumbua spare hata kwa miaka 2 bila shida yoyote.

Mengine nitakushauri kulingana na wachangiaji wanavyochangia. Karibu kwenye familia ya Nissan Dualis. For anything unaweza uliza tu bila shaka.
Umenikumbusha kitu hapo kwenye oil kuwa inatumia CVT sio hizi za kwetu Hydraulic
Ila kupita rafu rod usimuogopeshe gari hiyo inapita vizuri bila shida yoyote ili mradi tu isiwe mashimo makubwa; aende tu mdogo mdogo; Unataka asipeleke gari Kijijini desemba hii wakati IST inaenda?
 
Dualis Nyingi ni za Gearbox za CVT
Hizi gear box ni nzuri sana kama utafatisha mashart yake
Ni mbaya sana kama utachukulia poa
Weka oil sahihi hua inaandikwa katika dipstik
Ukichanganya madesa tu unaua gear box fasta
Kuna Dualis imetengenezwa na gear box isiyo ya CVT?
 
Umenikumbusha kitu hapo kwenye oil kuwa inatumia CVT sio hizi za kwetu Hydraulic
Ila kupita rafu rod usimuogopeshe gari hiyo inapita vizuri bila shida yoyote ili mradi tu isiwe mashimo makubwa; aende tu mdogo mdogo; Unataka asipeleke gari Kijijini desemba hii wakati IST inaenda?
Gari zote hizi zenye shock absorber hazijatengenezewa mazingira ya off-road kuna zile kama Land cruiser mkonga, land Rover 109,etc ndizo maeneo yake.

Hizi hazitaki sana fujo ndio hautaona unahangaika na mafundi.
 
Kuna jamaa zangu kama wawili wana hii gari, mmoja anasema kainunua 2020 lakini hadi June 2022 keshabadili gear box mara tatu mwingine nae keshabadili mara moja wanasema shida kubwa ya hizi gari ni kwenye gear box je wenye uzoefu hii ni kweli maana baada ya maelezo Yao nimejikuta naogopa kutekeleza ndoto yangu ya kumiliki hii gari
 
Watakuwa wanaweka vilainishi vya traditional automatic transmission badala ya vilainishi vya continuous variable transmission (CVT). Ukifanya hilo kosa, dk 0 tu unaua gearbox.
 
A

Asante mkuu, kwa hiyo unanishauri nisiogope kuichukua Iko poa?
 
Gari zote hizi zenye shock absorber hazijatengenezewa mazingira ya off-road kuna zile kama Land cruiser mkonga, land Rover 109,etc ndizo maeneo yake.

Hizi hazitaki sana fujo ndio hautaona unahangaika na mafundi.
Turudi kwenye Uhalisia; ni watanzania wangapi wenye hizo Mkonga, Landrover nk?
Mbona magari ya kawaida yamejaa vijijini na yapiga mzigo bila shida
 
Kuna jamaa zangu kama wawili wana hii gari, mmoja anasema kainunua 2020 lakini hadi June 2022 keshabadili gear box mara tatu mwingine nae keshabadili mara moja wanasema shida kubwa ya hizi gari ni kwenye gear box je wenye uzoefu hii ni kweli maana baada ya maelezo Yao nimejikuta naogopa kutekeleza ndoto yangu ya kumiliki hii gari
Hizo ni story za uongo. Amenunua gari kutoka kwa mtumiaji wa Tanzania au aliagiza used ya Japan?!
 
Turudi kwenye Uhalisia; ni watanzania wangapi wenye hizo Mkonga, Landrover nk?
Mbona magari ya kawaida yamejaa vijijini na yapiga mzigo bila shida
Haibadilishi ukweli kuwa hiyo gari imetengenezwa kwaajiri ya mazingira ya mjini. Huko kwenye makorogo na barabara za vumbi ni kulazimisha.
 
Kuna jamaa zangu kama wawili wana hii gari, mmoja anasema kainunua 2020 lakini hadi June 2022 keshabadili gear box mara tatu mwingine nae keshabadili mara moja wanasema shida kubwa ya hizi gari ni kwenye gear box je wenye uzoefu hii ni kweli maana baada ya maelezo Yao nimejikuta naogopa kutekeleza ndoto yangu ya kumiliki hii gari
Wanaoharibu haya magari ni mafundi wababaishaji na wajuaji
 
Habari wana JF,

Kwa mara ya kwanza kwenye maisha yangu nimenunua na kumiliki gari yangu ya kwanza nissan dualis, kusema ukweli sijui vitu vingu kuhusu magari nafahamu vitu vichache sana.

Naombeni msaada jinsi ya kuitunza hii gari angalau idumu napokea maoni na ushauri jamani, gari nimeipokea juzi tu
Hakikisha unafaya exitingisha
 
Back
Top Bottom