JAMHURI
JF-Expert Member
- Dec 15, 2010
- 449
- 60
Wanachama wa CCM Wilayani Kiteto mkoani Manyara wamejikuta katika malumbano na mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka baada ya Mbunge huyo machachari kuwaambia "Kiteto hakuna mwanaume"
Kauli hiyo alitokana na kile kilichodaiwa kuhofiwa kubadilishwa matokeo ya Ubunge na kufanya wanachama hao kufika kwa wingi katika ofisi hizo kushinikiza matokeo yasibadilishwe.
Kauli hiyo iliwaudhi wanaCCM hao na kujikuta wakirusha mawe na kuvunja gari lake kioo cha nyuma kisha kusababisha kuchafuka kwa hali ya amani ofisini jambo lililolazimu polisi kutumia mabomu ya machozi na risasi za moto kuwatawanya wafuasi hao.
Pia wanachama hao walienda kufanya fujo nyumbani kwa mbunge huyo na kuvunja taa za nje pamoja na kumpiga mlinzi jambo ambali lilidaiwa ni kosa.
Wajumbe hao wa CCM mkoa walifika kwa ajili ya kuhakiki matokeo ya Ubunge ambapo Benedict Ole Nangoro alilalamika kuhusu kuhujumiwa katika uchaguzi huo uliompa nafasi Emmanuel Papian.

Gari la Ole Sendeka lavunjwa vioo,Ole Nangoro anusurika kichapo
Nyumba yake yavamiwa na wanachama, wavunja taa na kumpiga mlinzi
JESHI la Polisi wilayani Kiteto mkoani Manyara limetumia mabomu ya machozi na silaha za moto kuokoa aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Kiteto Benedict Ole Nangoro na Christopher Ole Sendeka pamoja na kamati ya siasa ya Mkoa wa Manyara waliofika kuhakiki matokeo ya Ubunge.
Awali wajumbe hao walizuiwa kwa mawe na magogo barabarani kata ya Engusero wasifike makao makuu ya wilaya ya Kiteto wakitokea Dodoma, hali iliyolazimu Jeshi la Polisi kuwaokoa kwa kuwapa ulinzi kwa kuwafikisha Kibaya kwaajili ya kuhakiki matokeo hayo
Baada ya kamati ya siasa ya mkoa kufika katika ofisi za CCM Wilaya ya Kiteto majira ya mchana walianza kuhakiki matokeo ya Ubunge ambayo yalidaiwa kulalamikiwa na aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Kiteto Benedict Ole Nangoro aliyeambatana na wajumbe hao kutaka yahakikiwe.
Baada ya kusikia kuna kamati ya siasa mkoa wa Manyara imefika wanachama tulilazimika kufika ofisi za CCM kutaka kujua hatma ya ujio wao, kwani tumeshuhudia maeneo mengi matokeo ya uchaguzi yanabadilishwa baada ya kutangazwa washindialisema mwananchi Rajabu Jagon
Hali ilivyokuwa muda mchache uliopita.