Gari la Kampuni ya Pepsi Arusha lakamatwa kwa kukwepa kodi

Waziri2025

Senior Member
Sep 2, 2019
148
379
HALMASHAURI ya wilaya ya Longido Mkoa wa Arusha ,inalishikilia gari la Mauzo la kampuni ya Vinywaji baridi ya Pepsi (SBC)ya jijini Arusha baada ya kampuni hiyo kukwepa kodi kwa kipindi cha miaka 7.

Akiongea mhasibu wa halmashauri hiyo,Magige Chacha alisema kuwa gari hilo aina Eicher lenye namba za usajiri T 894 DSH lilikamatwa jana majira ya jioni ambalo bado linashikiliwa katika halmashauri hiyo.

Chacha alisema kuwa kampuni hiyo ya Pepsi ya jijini Arusha kwa muda mrefu wamekaidi kulipa kodi ya huduma(Service levy)katika wilaya hiyo licha ya uongozi kuwaandikia barua marakadhaa kwa njia ya kawaida na barua pepe (email) lakini walikuwa wakipiga chenga na kudharau.

"Hii kampuni ya Pepsi ni wasumbufu sana hawajatulipa kwa zaidi ya miaka sita au saba , kila tukijaribu kuwatafuta wanatupiga chenga tukaamua kuwandikia demand note lakini pia haikuzaa matunda ndio maana jana tukaamua kukamata gari lao"

Alisema kuwa kampuni hiyo ilipaswa kulipa kodi ya huduma 'service levy' kila baada ya miezi mitatu ,lakini katika kipindi cha miaka saba haikuwahi kulipa jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

'Baada ya kukamata gari lao viongozi wa kampuni hiyo walifika ofisini leo asubuhi na kutakiwa kulipa kodi hiyo baada ya kuleta mahesabu yao ya mauzo kutoka mamlaka ya mapato Tanzania TRA ambapo halimashauri hiyo huchukua asilimia 0.3 ya mauzo'

Hadi gazeti hili linaondoka katika halimashauri hiyo gari hilo likiwa na shehena ya soda lilikuwa bado linashikiliwa katika ofisi za halimashauri hiyo.

Kwa upande wake meneja Rasilimali watu wa kiwanda hicho aliyejitambulisha kwa jina la Edwin Abogasti alisema kuwa hana taarifa za kushikiliwa kwa gari la kiwanda chao akidai kwamba halmashauri hiyo haiwadai chochote kwa kuwa wao ni walipa kodi wazuri.

"Sisi ni walipakodi wakubwa na ndio maana tulishawahi kuzawadiwa cheti na TRA na hizo taarifa za kushikiliwa kwa gari letu wewe ndio unaniambia"

Taarifa za ndani kutoka halmashauri hiyo zinadai kwamba majira ya asubuhi uongozi wa SBC kutoka jijini Arusha ulitua katika halmashauri hiyo wakihaha kukomboa gari hilo lililokuwa limesheheni soda za mauzo.

Hata hivyo baadaye pande zote mbili waliingia kwenye kikao cha mazungumzo ili kuona namna bora ya kulipa deni hilo ambalo bado halikuwekwa wazi mpaka mahesabu ya mauzo yapatikane kutoka TRA.

Hata hivyo chacha aliongeza kuwa baada ya mazungumzo hayo,Kampuni hiyo imeonesha nia ya kulipa deni hilo na kuahidi kila baada ya miezi mitatu watakuwa wanalipa kodi hiyo ya huduma bila usumbufu wowote.

IMG-20221013-WA0004.jpg
 
Tusisumbue wawekezaji... hizi kodi za muda mrefu mama nazani alizisamehe kama sijakosea...

Au alisamehe baadhi na zingine bado zina hitajika kulipwa ata kama ni za muda mrefu
 
Kama ni Pepsi sawa tu maana wanaingiza hela nyingi ila kwa wafanyakazi sijui kama wanalipwa pesa nzuri kama coca-cola
 
Wataalam wa kodi mnipe ufafanuzi tafadhali; hivi hii kodi ya service levy (kodi ya huduma) ni kodi ya aina gani!

Maana unaenda Halmashauri kulipia leseni ya biashara, unakutana kimeo kingine cha kulipia cha service levy! Kwa sababu ya msongamano na foleni, unaamua kulipa huku ukiwa hujui chochote! Na hapo ni tofauti kabisa na kodi nyingine ya mapato ya TRA!
 
Back
Top Bottom