Gari kwa mkopo

fimboyaasali

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
8,452
8,003
Kama kuna mdau hapa,ana taarifa juu ya namna ambavyo mtu anayeanza kazi anaweza kupata mkopo wa gari,bila ya kuwa na pesa taslim,ila awe anakatwa kila mwisho wa mwezi.je afanyeje kupata mkopo wa hivyo?
 
Hapa ndipo mnapofeli waajiriwa, leo utatamani gari, kesho nyumba, keshokutwa biashara, vyote utahitaji kuchukua mkopo, mwishoe utaona kazi mbaya haina mshahara mzuri kumbe wewe ndiyo mbaya. Utajili utabaki kwa wachache tu.
 
Kwanza asante kwa majibu yako,pili jitafakari sana wewe mwenyewe,jinsi ulivyosoma maelezo yangu na jinsi ulivyojibu,inaonesha waziwazi kuwa una ugonjwa mbaya sana.Kama huna jibu ya swali analouliza mtu jifunze kunyamaza tu
 
Kama tayari una salary slip 3 zama NMB, NBC au CRDB ukakope mkopo ambao makato yake hayaendi zaidi ya miaka mitatu.
NB: Pata gharama halisi za kununua hiyo gari toka Japan na ushuru wake na bima na takataka ndogondogo ili ujue unahitaji mkopo wa shilingi ngapi. Usinunue gari iliyotumika bongo kwa hela ya mkopo, utalia.
Kuna yard ipo pale manzese kona ya kuingia mabibo wanakopesha gari. Nadhani wanaitwa africars
 
Kama tayari una salary slip 3 zama NMB, NBC au CRDB ukakope mkopo ambao makato yake hayaendi zaidi ya miaka mitatu.
NB: Pata gharama halisi za kununua hiyo gari toka Japan na ushuru wake na bima na takataka ndogondogo ili ujue unahitaji mkopo wa shilingi ngapi. Usinunue gari iliyotumika bongo kwa hela ya mkopo, utalia.
asante sana
 
Search Google nilikuwa nawaangalia jamaa wanaitwa Magari chap chap wanakupa gari kwa kulipia nusu then iliyobaki utalipia ndani ya miaka miwili. Unawaachia kadi mpaka utakapomaliza deni lao.
 
Kwanza asante kwa majibu yako,pili jitafakari sana wewe mwenyewe,jinsi ulivyosoma maelezo yangu na jinsi ulivyojibu,inaonesha waziwazi kuwa una ugonjwa mbaya sana.Kama huna jibu ya swali analouliza mtu jifunze kunyamaza tu
Acha kujibu watu fyongo! Kama unajitambua si uende benki ukakope? Hela huna!
 
Utaratibu wa Mkopo navyofahamu uko hivi Mala nyingi unaenda Bank unapewa form unajaza kisha kuna sehemu anakuja kujaza muajiri wako(MKUU WA IDARA NA HR) kisha inarudi bank kwa mchakato wa Mkopo.

Ila kama ndiyo unaanza kazi basi subiri hadi umalize Probation period yaani uthibitishwe kazini (hii ni Miezi 12 kwa Sasa) ndipo taratibu zitakuruhusu kukopa Mtaalamu,zaidi nenda kwa HR wako atakupa muongozo bila shida.

Pia sikushauri ukope mkopo wa Gari(Kadi haitakuwa na Umiliki wako hadi umalize Mkopo),nakushauri ukope Hela ili ukanunue Gari unayotaka.
 
Kama kuna mdau hapa,ana taarifa juu ya namna ambavyo mtu anayeanza kazi anaweza kupata mkopo wa gari,bila ya kuwa na pesa taslim,ila awe anakatwa kila mwisho wa mwezi.je afanyeje kupata mkopo wa hivyo?
Nenda benki ya PBZ ndio wana dar/Dom ktk matawi yao, hao ndio wanao huo utaratibu wa kukupatia/kukukamilishia lengo la mkopo wako.
 
Hapa ndipo mnapofeli waajiriwa, leo utatamani gari, kesho nyumba, keshokutwa biashara, vyote utahitaji kuchukua mkopo, mwishoe utaona kazi mbaya haina mshahara mzuri kumbe wewe ndiyo mbaya. Utajili utabaki kwa wachache tu.
Bro amekuambia yeye muajiriwa, amekwambia hana biashara Au hana nyumba na anataka gari ya mkopo?
 
Utaratibu wa Mkopo navyofahamu uko hivi Mala nyingi unaenda Bank unapewa form unajaza kisha kuna sehemu anakuja kujaza muajiri wako(MKUU WA IDARA NA HR) kisha inarudi bank kwa mchakato wa Mkopo.

Ila kama ndiyo unaanza kazi basi subiri hadi umalize Probation period yaani uthibitishwe kazini (hii ni Miezi 12 kwa Sasa) ndipo taratibu zitakuruhusu kukopa Mtaalamu,zaidi nenda kwa HR wako atakupa muongozo bila shida.

Pia sikushauri ukope mkopo wa Gari(Kadi haitakuwa na Umiliki wako hadi umalize Mkopo),nakushauri ukope Hela ili ukanunue Gari unayotaka.
Naona probation now days imepungua... naona it's 9-12 months only
 
Kama unataka kukopa kopa bank
Usikope microfinance au kampuni ya mtu
Huko utatapeliwa utalipa mil 30 gari ya 15 m
 
Watu kama hao , huwa wanataka uwe na nusu ya hela ya thamani ya gari.... Halafu wanaweza kukupa mwaka au zaidi kulipa mkopo uliobakia

Back
Top Bottom