Gari kudai gia

Mpigadili Tz

JF-Expert Member
May 4, 2015
1,054
1,886
Habari zenu wakuu? Jana katika pita pita zangu kuna Rafiki yangu aliniambia hivi ''Gari yangu ina gia tano lakini nashangaa nikiwa katika mwendo na natembelea namba tano huwa inadai gia wakati gia nishamaliza'' nikawa najiuliza hivi hii inawezekana au labda kuna mtu aliiharibu? Msaada wenu tafadhari AHSANTENI
 
Hiyo gari ni auto au manual?
 
Wakati mwingine ni mzuka tu,mtu ukiwa unaendesha manual kuna muda mzuka huwa unapanda unatamani uendelee kutia gia tu wakati ushamaliza zote...sasa huenda jamaa yako anamizuka yake afu anasingizia gari bado inadai gia...mwambie aache mizuka ataingia mtaroni
 
Inategemea iyo gia no 5 yuko kwenye speed ngap?maana kama gia no 5 uko speed 60,80 lazma idai gia nyingine wakat ndio mwisho wake hapo
 
Inategemea iyo gia no 5 yuko kwenye speed ngap?maana kama gia no 5 uko speed 60,80 lazma idai gia nyingine wakat ndio mwisho wake hapo
Ahsante sana, au inawekana giabox na mashine vikawa tofauti yaani mfano giabox ya rav4 mashine ya v8?
 
Hiyo hutokea pale ambapo unaingiza gia kwa pupa kabla gari haija changanya vizuri mfano ndani ya km moja umesha jaza gia zote zote nalo huwa lina sababisha hiyo hali ya gari kuwa kama inahitaji kuongeza gia nyingine wakati zimeisha ,kikubwa ni kuendesha gari kwa kufuata taratibu za gari husika . lakin pia labda kama wamesha fanya utundu kwenye gearbox na clutch plates zake.
 
Ni hali ya engine kutoa mlio wa kukera kutokana na gari kutembelea gia isiyostahili au matumizi mabaya ya accelerater pedal. Sasa kama gari ina gia 5 umemaliza zote bado engine inalalamika muhimu ni kuzingatia matumizi sahihi ya accelerater pedal (mshale wa tachometer/rotation usivute green mark)
 
Ni kweli mkuu.. Hasa gari za Diesel lama Nissan Hardbody ukishafika 120, na uko gia namba tano inakuwa inadai gia ya sita.. Hiyo gari ya jamaa ako ni gari mahususi kwa mizigo sio kwa spidi...
 
Back
Top Bottom