Gamba lazidi kuwa hoi bin taabani

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,015
CCM kumng’oa Mukama
• Wabunge nao wakalia kuti kavu

na Mwandishi wetu
Tanzania Daima

MKAKATI wa kumng’oa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilson Mukama, anayedaiwa kushindwa kukiendesha chama umeshika kasi, Tanzania Daima Jumapili limebaini.

Mbali na Mukama, baadhi ya wabunge pia wanataka wenzao waliogoma kuipitisha bajeti ya serikali nao kushughulikiwa kwa kukisaliti chama.
Tanzania Daima Jumapili limedokezwa kuwa baadhi ya wabunge na wanachama wanataka Mukama aachie ngazi au afukuzwe.

Duru za kisiasa kutoka ndani ya chama hicho zinaeleza kuwa matumaini ya wanachama wengi wakiwamo vigogo wa chama hicho waliyokuwa nayo kwa Mukama wakati anaingia madarakani yamefifia.
Katibu mkuu huyo aliyeingia madarakani kwa mbwembwe ndani ya CCM miaka miwili iliyopita, anadaiwa kushindwa kabisa kukijenga chama kama ilivyotarajiwa na badala yake ametengeneza mpasuko mkubwa ndani ya chama.

CCM kwa sasa inakabiliwa na makundi makubwa mawili yenye wafuasi wengi, moja ni lile linaloongozwa na Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, ambaye amebaki na kundi linalojinadi kama wapinga ufisadi na kundi jingine ni lile linaloongozwa na hasimu wake kisiasa, Edward Lowassa, linalopingana na dhana ya kujivua gamba.

Mukama pia anadaiwa kushindwa kukiimarisha chama na kuruhusu wanachama wengi kukihama chama hicho kwa kile kilichoelezwa kutoridhishwa na mwenendo wa mambo ndani ya CCM.

Kiongozi huyo anabebeshwa lawama kuwa ameshindwa kusimamia dhana ya kujivua gamba wakati yeye ndiye aliyeanzisha hoja hiyo kupitia tume aliyoiongoza kufanya utafiti kubaini sababu za CCM kupata kura chache za urais na kupokwa majimbo mengi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

“Unajua, Mukama ndiye aliyekuja na matokeo ya utafiti kwenye Kamati Kuu na Halmashauri Kuu. Alibainisha sababu kadhaa za chama kushindwa, lakini sababu kubwa tume yake ilibaini ni pamoja na chama kukosa mvuto kutokana na baadhi ya makada wake, Edward Lowassa, Andrew Chenge na Rostam Aziz kuhusishwa na ufisadi. Akaja na mapendekezo kwamba makada hao wavuliwe nyadhifa zao.

“Leo ameshindwa kusimamia kile alichokiamini, badala yake chama kimekuwa kikipiga vita ya maneno tu, mara kutoa siku 90, mara tumeongeza, mara haijulikani. Matokeo yake tumezalisha makundi yanayokitafuna chama,” alisema kada mmoja ambaye ni mjumbe wa NEC.

Kada huyo anasema kuwa baadhi ya makada wanaotuhumiwa kwa ufisadi waliandaliwa barua za kutakiwa kuachia nyadhifa zao lakini hilo lilishindikana kutokana na utendaji mbovu wa Mukama.
Makada wengine wanamlinganisha Katibu Mkuu Mukama na mtangulizi wake, mzee Yusuf Makamba, kwamba licha ya kuwa na elimu ndogo ya darasani, amemzidi Mukama kiutendaji.

Dalili za CCM kumchoka Mukama zimejionyesha hivi karibuni katika moja ya vikao vya wabunge wa CCM ambapo baadhi walifikia hatua ya kusema katibu mkuu wao amechoka kimawazo, bora aachie ngazi sasa.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho kilichoongozwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, mjini Dodoma zilisema wabunge walikuja juu wakati walipokuwa wakijadili hali ya kisiasa ndani ya chama chao na kuwekeana msimamo wa kuiunga mkono Bajeti ya mwaka 2012/2013.

Mmoja wa viongozi waandamizi wa CCM, aliliambia gazeti hili kuwa katibu mkuu sasa hashirikishwi katika baadhi ya mambo baada ya kubaini kuwa hana uwezo wa kukiimarisha chama.
“Angalia katika mikutano yote inayofanywa na chama kwa sasa hata ule wa Jangwani ulikuwa na watu wengi, Mukama hakuwepo. Ingawa alikuwa nje ya nchi, lakini hata kama angekuwapo, asingepata nafasi ya kuhutubia kwani hana uwezo wa kuongea hadharani.

Kada mwingine wa CCM alimshmabulia Mukama kwa madai kuwa amekuwa akiropoka vitu ambavyo wakati mwingine hana utafiti navyo.
“ Mfano ni wakati wa kumuaga marehemu Bob Makani. Alitoa historia ya ajabu kuhusu waasisi wa CHADEMA, matokeo yake, Freeman Mbowe, alimuumbua pale alipotoa ufafanuzi kupinga kauli yake,” alisema.

Wabunge walioipinga bajeti kukiona
Tanzania Daima Jumapili, limedokezwa kuwa kuna mpango wa kutaka kuwawajibisha baadhi ya wabunge waliokiuka msimamo wa pamoja wa wabunge wa CCM juu ya kuipitisha bajeti.
Bajeti hiyo ya serikali iliyopitishwa Ijumaa wiki hii kwa kura 225 za ndiyo huku kura 72 zikiikataa, kwa kupiga kura za hapana, zaidi ya wabunge 54 hawakuhudhuria mkutano huo.

Kuna taarifa kuwa wabunge waliogoma kuhudhuria kikao hicho bila taarifa na wengine waliokataa kuipitisha bajeti hiyo huenda wakakumbana na mkono wa chama ambacho katika siku za hivi karibuni kimekuwa kikihaha kujinusuru kutoka katika minyukano ya makundi yanayohasimiana.

Inasemekana baadhi ya wabunge wanataka wenzao wajadiliwe na ikiwezekana wawajibishwe ili kujenga nidhamu chamani pamoja na kudumisha uwajibikaji wa pamoja.

Wabunge hao wanatarajiwa kujadiliwa na kikao cha wabunge wa CCM ambacho kinatarajiwa kufanyika mapema wiki ijayo mara baada ya kuwasilishwa kwa hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Wabunge wanaoonekana kuwasaliti wenzao ni Luhaga Mpina (Kisesa), Deo Filikunjombe (Ludewa) na Kangi Lugola (Mwibara).

Waache wajitafune wao wenyewe,laana ya kuwafanyia watanzania mambo ya ajabu itawamaliza,na bado,sidhani kama huyo dhaifu wao ataendelea kuwapo hapo kitini hadi 2015
 
Magamba bana! Yani ukisimamia maslahi ya nchi unaonekana kukisaliti chama, hivi hawajiangalii wenyewe waone watz tumechoka na mambo yao? Ok ngoja wajipe moyo tu ila hao wanaowaita wasaliti ndo mashujaa kwetu
 
Tukifanikiwa kuondoa viti maalumu, tutawashikisha adabu magamba na wanamipasho wao
 
Sijui hawa watu hawaelewi namna gani?! Tulishawaambia mtu anayepaswa kuvuliwa gamba kwanza ni Mr Dhaifu, halafu hao vingunge wengine ndo watafuata.
Walitegemea Mukama asimamie vipi uvuaji wa gamba wakati mwenyekigoda wa chama ndo fisadi nambari wani?
Walitegemea Mukama atoe wapi uwezo wa kufufua chama wakati chama chenyewe kiko ICU?
Above all: Wakitaka kujisafisha na kujenga chama wamwondoe Dhaifu kwanza; la sivyo chama kutawafia tu.
 
Itakuwa ni habari njema sana kwa waTz tuliochoshwa na hii hali ya nchi yetu!
 
Mukama is just a scapegoat. CCM is already on a sloppy road to self destruction, I do not think any changes in the leadership of the Secretary General will do any good. Bye, bye CCM. Bye bye mafisadi.
 
Naona badala ya kujenga Chama wanachimba kaburi la kujizika na wakati huo huo waziri wao anazika nyeti zake kwa wake watu
 
Nadani hoja ya uwajibikaji ni ndoto kwa CCM, Enzi za mwalimu hii kitu ingeshamalizika zamani.. mtu /mwanachama yeyote aliyeshisiwa ni mnla rushwa au amyekiuka maadaili huondolewa mara moja kwa kisingizio chochote kile ili mradi kuondoa sumu kwenye chama ,,lakini siku hizi CCM makundi ya mafisadi Vs walio mafisadi yanakinzana hadharani pasipo aibu... Hao mapacha watatu nao wameonyesha kwma hawaitakii mema CCM wala watanzania... wanaendelea makundi kwa manufaa yao... kama kweli ni siasa "uchwara: alizodai Rostam Aziz mbona bado anang'ania???
Shame on makundi and divisive elements....
 
Yan wanadhani tatizo ni mkama! Ccm yote hakuna jipya,hata nape mwenyewe hana jipya.

CCCM hawamuwezi lowasa kabisa sasa wanamtupia mzigo mkama wakati chama kizima kina muogopa! Kweli lowasa mwamba ndani ya ccm hadi jk ana muogopa sembuse wasio na hoja nape na mkama.
 
Saisa za Tanzania, hata aibu hazina, hatujifunzi hata kwa wenzetu, haya masuala ya kupitisha vitu muhimu kama bajeti kwa kuangalia maslahi ya chama badala ya uhalisia wa mambo ni kuendeleza umaskini kwa mtanzania. Mbunge ameonyesha kutokurishishwa na bajeti na kukataa kuiunga mkono wewe unasema eti ashughulikiwe. Kama wanataka ccm ife kabla hata ya 2015 waendelee kuchukua mawazo ya watu wenye fikra za mgando kama hawa waliokuja na wazo hili. Kumwondoka Mkama sawa hilo wanaweza kuliongea lakini hili la wabunge wasikuse kabisa.
 
tukisema hiki chama ndiyo kinaaga watu wengine wanajifanya kichwa ngumu eti hawaelewi Hata wakimtoa Mkama aje nani hawezi kukiokoa hiki chama na ugonjwa wa ufisadi unao kiua kwa kasi kubwa
 
Iki chama cjui ndio sikio la kufa?Twiga wetu,madini,ardhi,na sasa umeibuka ufisadi mpya wa wake za watu!tunaipeleka wapi tanganyika yetu?wabunge wa ccm kazi kugonga meza,kuzomea,na kusinzia bungeni
 
CCM kumng’oa Mukama
• Wabunge nao wakalia kuti kavu

na Mwandishi wetu
Tanzania Daima

MKAKATI wa kumng’oa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilson Mukama, anayedaiwa kushindwa kukiendesha chama umeshika kasi, Tanzania Daima Jumapili limebaini.

Mbali na Mukama, baadhi ya wabunge pia wanataka wenzao waliogoma kuipitisha bajeti ya serikali nao kushughulikiwa kwa kukisaliti chama.
Tanzania Daima Jumapili limedokezwa kuwa baadhi ya wabunge na wanachama wanataka Mukama aachie ngazi au afukuzwe.

Duru za kisiasa kutoka ndani ya chama hicho zinaeleza kuwa matumaini ya wanachama wengi wakiwamo vigogo wa chama hicho waliyokuwa nayo kwa Mukama wakati anaingia madarakani yamefifia.
Katibu mkuu huyo aliyeingia madarakani kwa mbwembwe ndani ya CCM miaka miwili iliyopita, anadaiwa kushindwa kabisa kukijenga chama kama ilivyotarajiwa na badala yake ametengeneza mpasuko mkubwa ndani ya chama.

CCM kwa sasa inakabiliwa na makundi makubwa mawili yenye wafuasi wengi, moja ni lile linaloongozwa na Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, ambaye amebaki na kundi linalojinadi kama wapinga ufisadi na kundi jingine ni lile linaloongozwa na hasimu wake kisiasa, Edward Lowassa, linalopingana na dhana ya kujivua gamba.

Mukama pia anadaiwa kushindwa kukiimarisha chama na kuruhusu wanachama wengi kukihama chama hicho kwa kile kilichoelezwa kutoridhishwa na mwenendo wa mambo ndani ya CCM.

Kiongozi huyo anabebeshwa lawama kuwa ameshindwa kusimamia dhana ya kujivua gamba wakati yeye ndiye aliyeanzisha hoja hiyo kupitia tume aliyoiongoza kufanya utafiti kubaini sababu za CCM kupata kura chache za urais na kupokwa majimbo mengi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

“Unajua, Mukama ndiye aliyekuja na matokeo ya utafiti kwenye Kamati Kuu na Halmashauri Kuu. Alibainisha sababu kadhaa za chama kushindwa, lakini sababu kubwa tume yake ilibaini ni pamoja na chama kukosa mvuto kutokana na baadhi ya makada wake, Edward Lowassa, Andrew Chenge na Rostam Aziz kuhusishwa na ufisadi. Akaja na mapendekezo kwamba makada hao wavuliwe nyadhifa zao.

“Leo ameshindwa kusimamia kile alichokiamini, badala yake chama kimekuwa kikipiga vita ya maneno tu, mara kutoa siku 90, mara tumeongeza, mara haijulikani. Matokeo yake tumezalisha makundi yanayokitafuna chama,” alisema kada mmoja ambaye ni mjumbe wa NEC.

Kada huyo anasema kuwa baadhi ya makada wanaotuhumiwa kwa ufisadi waliandaliwa barua za kutakiwa kuachia nyadhifa zao lakini hilo lilishindikana kutokana na utendaji mbovu wa Mukama.
Makada wengine wanamlinganisha Katibu Mkuu Mukama na mtangulizi wake, mzee Yusuf Makamba, kwamba licha ya kuwa na elimu ndogo ya darasani, amemzidi Mukama kiutendaji.

Dalili za CCM kumchoka Mukama zimejionyesha hivi karibuni katika moja ya vikao vya wabunge wa CCM ambapo baadhi walifikia hatua ya kusema katibu mkuu wao amechoka kimawazo, bora aachie ngazi sasa.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho kilichoongozwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, mjini Dodoma zilisema wabunge walikuja juu wakati walipokuwa wakijadili hali ya kisiasa ndani ya chama chao na kuwekeana msimamo wa kuiunga mkono Bajeti ya mwaka 2012/2013.

Mmoja wa viongozi waandamizi wa CCM, aliliambia gazeti hili kuwa katibu mkuu sasa hashirikishwi katika baadhi ya mambo baada ya kubaini kuwa hana uwezo wa kukiimarisha chama.
“Angalia katika mikutano yote inayofanywa na chama kwa sasa hata ule wa Jangwani ulikuwa na watu wengi, Mukama hakuwepo. Ingawa alikuwa nje ya nchi, lakini hata kama angekuwapo, asingepata nafasi ya kuhutubia kwani hana uwezo wa kuongea hadharani.

Kada mwingine wa CCM alimshmabulia Mukama kwa madai kuwa amekuwa akiropoka vitu ambavyo wakati mwingine hana utafiti navyo.
“ Mfano ni wakati wa kumuaga marehemu Bob Makani. Alitoa historia ya ajabu kuhusu waasisi wa CHADEMA, matokeo yake, Freeman Mbowe, alimuumbua pale alipotoa ufafanuzi kupinga kauli yake,” alisema.

Wabunge walioipinga bajeti kukiona
Tanzania Daima Jumapili, limedokezwa kuwa kuna mpango wa kutaka kuwawajibisha baadhi ya wabunge waliokiuka msimamo wa pamoja wa wabunge wa CCM juu ya kuipitisha bajeti.
Bajeti hiyo ya serikali iliyopitishwa Ijumaa wiki hii kwa kura 225 za ndiyo huku kura 72 zikiikataa, kwa kupiga kura za hapana, zaidi ya wabunge 54 hawakuhudhuria mkutano huo.

Kuna taarifa kuwa wabunge waliogoma kuhudhuria kikao hicho bila taarifa na wengine waliokataa kuipitisha bajeti hiyo huenda wakakumbana na mkono wa chama ambacho katika siku za hivi karibuni kimekuwa kikihaha kujinusuru kutoka katika minyukano ya makundi yanayohasimiana.

Inasemekana baadhi ya wabunge wanataka wenzao wajadiliwe na ikiwezekana wawajibishwe ili kujenga nidhamu chamani pamoja na kudumisha uwajibikaji wa pamoja.

Wabunge hao wanatarajiwa kujadiliwa na kikao cha wabunge wa CCM ambacho kinatarajiwa kufanyika mapema wiki ijayo mara baada ya kuwasilishwa kwa hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Wabunge wanaoonekana kuwasaliti wenzao ni Luhaga Mpina (Kisesa), Deo Filikunjombe (Ludewa) na Kangi Lugola (Mwibara).
Poleni sana wanaojidanganya Mukama kuwa ni tatizo. Ata mkitaka muwe na katibu mpya kila baada ya week moja hakuna mabadiliko yoyote. CCM mmenshakuwa kichefuchefu sana kwa watu na kama kuna wanaowashahabikia ni wale wanaopata makombo au uchakavu unaotokana na ufisadi wenu. Mnakaa mnapitisha budget ambayo haimsaidii wala kumpatia matumaini mtanzania wa kawaida then mseme Mukama hajafanya kazi ya kuimarisha Chama. Mtu anaimarisha chama ambacho watu wanakipenda na kinawajari wananchi. Muda wenu umekwishwa kaeni pembeni! Mungu ibarikia Africa Mungu ibarika Tanzania na Munge endelea kuyaumbua na kuyapukutisha Magamba
 
CCM bwana wanafikiri tatizo ni Mkama, mkama siyo ishu ndani ya CCM, tatizo ni yule dhaifu sijui kwa nini wanashindwa kupaza sauti na kusema JK aachie ngazi ili chama kijiendeshe. Wanaomtetea Jk wanamaslahi naye na ndio maana hawathubutu kumtaja. Lakini any way chama ndo kinakufa kwa kasi, wananchi wamepoteza imani kwa chama, rais na serikali yake. RIP CCM
 
Sijui hawa watu hawaelewi namna gani?! Tulishawaambia mtu anayepaswa kuvuliwa gamba kwanza ni Mr Dhaifu, halafu hao vingunge wengine ndo watafuata.
Walitegemea Mukama asimamie vipi uvuaji wa gamba wakati mwenyekigoda wa chama ndo fisadi nambari wani?
Walitegemea Mukama atoe wapi uwezo wa kufufua chama wakati chama chenyewe kiko ICU?
Above all: Wakitaka kujisafisha na kujenga chama wamwondoe Dhaifu kwanza; la sivyo chama kutawafia tu.

Mkuu magamba wana "utamaduni" wao wa kuachiana hata kama DHAIFU anavurunda ni lazima amalize awamu zake.
 
Sasa mbona wanataka kumbebesha Mukama udhaifu wa mtu mwingine? Bila kumwondoa dhaifu kwanza chama hakiwezi kufufuka, lazima kitawafia tu.
 
maneno mengi humu , ikifika uchaguzi mnatupiwa crate za bia ,machangu doa lori mbili, tatu , nyama kidogo ya kuchoma , wale kinamama wanaangushiwa vipande viwili vya kanga na wale wazee wanaangushiwa vikoi wote mnaziba midomo yenu

Lilobaki ni kuingia jikoni kuchakachua kura tu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom