Gadafi anafaa kuiongoza afrika kweli?

Exaud J. Makyao

JF-Expert Member
Nov 30, 2008
1,518
22
Rais Muamar Gadafi kachaguliwa kuwa mkuu wa Umoja wa afrika.Hivi kweli anafaa kuiongoza Afrika wakati nchi yake inamshinda?Kwani kuwa mkuu wa Umoja wa Afrika kunahitaji sifa gani?Au hakuna kigezo?Mimi sijui.
 
Mimi nina wasiwasi kama alichaguliwa na watu wenye kuona mbali? Raisi wa Africa anatakiwa mtu mwenye maono ya kufikiria mbali sio kama huyu Mzee Gadaf.

Au ni ile imani kwamba ukishakuwa raisi wa nchi yoyote hata iwe imekushinda unaweza kupewa cheo kilichopo juu ya uraisi wa nchi ambao mimi naona ni kuwa Rais wa Bara au muunganiko wa nchi zaidi ya moja kama jumuia ja Africa Mashariki.

Tusikubali hali hiyo.
 
gadaffi hana sfa za kuwa kiongozi; ukuacha alyoyasema siku nyingi nyuma hebu kumbuka aliyoyasema Uganda wakati akizindua msikiti pale Kampaala. Eti Mugabe na Museveni wanastahili waendelee kutawala hadi wafie madarakani na pia kwamba dini ya kweli ni Uisilamu pekee kwani ukiristo ni ya uongo.

Hatutaki kiongozi ambaye ni Immotional kwani aliyasema hayo kwavile tu yeye ni Muimla (dikteta) kama Mu7 na Mbabe na pia ni Muislam.
 
Mhache acha mambo hayo kwani unaujua upeo wake Gadaffi ?AU unasimamia kwenye propaganda za Mwalimu bado.Uliwahi kusikia Libya ikiomba misaada?Kuingia kwenye janga la njaa?AU Vita?Libya is economically stable country in Africa.Sasa unataka nini.Ukiingia mjini Tripoli na Vijiji vinvyouzunguka mji wa Bengaz huwezi ona tofauti. Isitoshe wako wapi waarabu wa kutoka Libya wanaohangaika na umachinga Karakoo?

Mbona Mwenyekiti aliyetoka hakuonyesha upeo wowote?Mwacheni Colonel Gaddafi alete Mungano wa kweli Afrika ,Ndoto ambayo wengi wa marais wenye uchu wa madaraka walishindwa kuuleta.

Ni kiongozi asiye na makuu tena ni mcha Mungu.Pale Addis wakati viongozi wengine wanavinjari na vimwana vyao kwenye mahoteli ya kitalii,Yeye yuko kwnye hema lake akimwomba Mungu.Wengine wakikwea midege ya gharama mwenzao anakatiza kwa msafara wa magari kurdi nchini kwake.Ni mara ngapi umesikia Colonel Gaddafi akizurura zurura kwenye nchi za kigeni kuomba omba misaada kwa ajili ya nchi yake?

Nina imani kuwa akishika uenyekiti mbali ya kuunganisha bara la Afrika pia atahakikisha vita barani pamoja na njaa vinatokomezwa haraka.
 
Gaddafi siku zote anaongozwa na maono yake binafsi. Kumbuka kuwa ndiye aliyewahifadhi na kutoa mafunzo ya kijeshi kwa baadhi ya madikteta na watawala kati katika Afrika kama vile Charles Tylor.

Siamini kama Gaddafi ana maono yoyote kwa ustawi wa Afrika zaidi ya kutaka kuwa Mfalme wa Afrika
 
real ,That an old senior Cornel can not lead today africa! we need New Leader with current vission to lead africa not a man in transition to lead Africa.
 
Nadhani inategemea hapo kuhusu hilo swala maana inawezekana anaweza kuwa anafaaa maana nchi yake ipo sehemu nzuri sana na anafanya vitu vingi na vya maana zaidi so anaweza kuingoza africa au sijui kuna kiongozi mwingine anayeweza kufaa hapo??
 
real ,That an old senior Cornel can not lead today africa! we need New Leader with current vission to lead africa not a man in transition to lead Africa.

I think he can, cause the important issue is not his age or his past, is what the most african need to see one day, that the Africa will trully Unite, And he have at least shown that he have an idea, Who realy you think can fit? For me Its rirght time 4 him to be our African Leader
 
Mimi nina wasiwasi kama alichaguliwa na watu wenye kuona mbali? Raisi wa Africa anatakiwa mtu mwenye maono ya kufikiria mbali sio kama huyu Mzee Gadaf. Au ni ile imani kwamba ukishakuwa raisi wa nchi yoyote hata iwe imekushinda unaweza kupewa cheo kilichopo juu ya uraisi wa nchi ambao mimi naona ni kuwa Rais wa Bara au muunganiko wa nchi zaidi ya moja kama jumuia ja Africa Mashariki. Tusikubali hali hiyo.

Sio kweli kaka,Gadaf hajashindwa katika Nchi yake, Tumunge mkono jamani, Huyu mzee ana mawazo mazuri sana, ni kiongozi gani aliyebaki afrika mwenye nia ya kuiona Africa inakuwa taifa moja lenye nguvu, bila shaka ni Gadaf! Msichukulie ugomvi wake na mataifa ya Kimagharibi ndo sababu ya kudissgrade, hata hivyo amekwisha elewana nao, lakini kuhusu kuongoza nchi yake amefanikwa sana. au nikupe mifanio mzee
 
Wengi wamemchukia alipousema vibaya Ukristo na sio zaidi ya hapo, hayo mengine ni propaganda tu, kuficha ukweli wa chuki kuwa ni kutokana na kuusema vibaya dini yao.

Kwa viongozi wa kiafrika walioongoza vema yeye ni mmoja wapo, tena mzowefu wa masuala ya kimataifa. amewahi kushika uongozi wa OAU mara kibao sasa alipopata AU sio mbaya, anastahili na anaweza.
 
Yangu macho na masikio.Kama amewahi kusema dini za wengine vibaya,Nahisi kama Afrika haiko kwenye mikono sahihi.
Naiombea heri Afrika.
 
Rais Muamar Gadafi kachaguliwa kuwa mkuu wa Umoja wa afrika.Hivi kweli anafaa kuiongoza Afrika wakati nchi yake inamshinda?Kwani kuwa mkuu wa Umoja wa Afrika kunahitaji sifa gani?Au hakuna kigezo?Mimi sijui.

Huyu hafai kuongoza Afrika kwa sababu ni dikteta aliyeng'ang'ania madarakani miaka chungu nzima sasa. Sijui viongozi wa Afrika walikuwa wanafikiria nini walipomteua dikteta kuwa Mwenyekiti wa AU.
 
Rais Muamar Gadafi kachaguliwa kuwa mkuu wa Umoja wa afrika.Hivi kweli anafaa kuiongoza Afrika wakati nchi yake inamshinda?Kwani kuwa mkuu wa Umoja wa Afrika kunahitaji sifa gani?Au hakuna kigezo?Mimi sijui.

nakuonea huruma sana

kwani kikwete alikuwa anaweza au amewza kuiongoza tanzania

mbona alikuwa rais wa AU
 
kadri yako dikteta ni nani,,,unafuata mfumo wa magharibi nini

Kiongozi yeyote asiyetaka kuruhusu mabadiliko ya juu katika uongozi wa nchi yake ni dikteta. Mu7 na Ghadaffi wote ni madikteta ambao hawataki kuachia madaraka. Viongozi kama hawa ni waroho wa madaraka.
 
Rais Muamar Gadafi kachaguliwa kuwa mkuu wa Umoja wa afrika.Hivi kweli anafaa kuiongoza Afrika wakati nchi yake inamshinda?Kwani kuwa mkuu wa Umoja wa Afrika kunahitaji sifa gani?Au hakuna kigezo?Mimi sijui.

Let's give the man a chance to prove himself.
Let's see what he will do about
Mugabe-Zimbabwe
Bashir-Sudan
Congo crisis?
Somalia??
Let's see if he will come up with new ideas and solutions.

That, Gaddafi, has nurtured an overt ambition to be the first african head Or to be the head of all Africa countries united is clear.

Let us hope that in his quest to realise his dream, the trickle down effect might have benefits for that all African countries. Unity, end of ceaseless wars, enough food, sincere fight against Malaria, and AIDs. This is my Utopia.
Let's wait and see...
 
Back
Top Bottom